Acha uongo wewe hapo mwanzoni unasema ulihamasika hadi ukajiunga afu mwishoni mwa uzi huu unasema umestuka kwamba hujajiunga na hii inshuWadau wenzangu wa BI, leo kuna rafiki yangu alinialika kwenye Mkutano mmoja a So Called D9 Tanzania Group, Pale Kebbys Hotel Bamaga. Nikaingia kwenye Darasa na Kusikiliza, Mafunzo niliyoyapata ni Mazuri mpaka nikahamisika Kujiunga, sasa tukiwa katika Hatua za Mwisho kumaliza Darasa, Kumbe Miongoni mwa wanafunzi wenzangu Kama Sita hivi, Kumbe walikua ni Maafisa wa Usalama, na wamekua wakihudhuria hayo Mafunzo karibia Week 2. Sasa kilichotokea wakawakamata Viongozi wa hiyo D9 akiwemo mwanzilishi wa hapa Tanzania, ambaye ni Kijana tu mdogo anaitwa Benny, kiukweli kwa alivyo tueleza Jamaa ana hela na Amefanikiwa sana. Mara tukaambiwa tushuke Chini, Jamaa wakaanza kuzozana wakatiwa Nguvuni Mpaka kwenye Magari ya Polisi pale chini, Moja ya vitu jamaa walivyoulizwa ni, Waonyeshe Ofisi zao, Usajili wa hiyo D9 kwa hapa Tanzania, Account za Bank vyote jamaa Hana, kumbe pesa anaingiziwa kwenye personal account, halafu hana Usajili, watu tukabaki tumeraharuki hapo hatujui nn tufanye, Jamaa wakaondoka nae. Sasa nikabaki na maswali Mengi hivi inakuaje mtu unafanya Biashara ya Mamilioni yote hayo mpaka $ 60,000/= Kila week anaingiza kama faida na zinaingia kwenye accounts yake halafu Fedha nyingine anatuma kwa huyo Mwanzilishi wa D9 Africa ambaye ni Mganda, nae anatumiwa kwa personal account. Sasa watu wamebaki hapo hawajui hatma yao, na mm kesho nilikua nategemea Kuanza ila Nimesita kutokana na hili lililotokea Leo. Najua kama kuna mwana BI humu na ni Member atakua amesikia hii ishu Jioni hii. Nimetoa tu hii taarifa kwa nia Njema wala si kuwakatisha tamaa ila nimeshuhudia kwa macho na Masikio yangu. Asanteni(COPPIED FROM MAIN SOURCE)