Benki kupiga mnada Mgodi wa Kiwira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Benki kupiga mnada Mgodi wa Kiwira

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nonda, Mar 13, 2011.

 1. N

  Nonda JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  WanaJF
  Kweli Tanzania ni shamba la bibi.


  Madeni hayo kwa mgodi huo yalibainika wakati Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF, Yakubu Kidula, alipokuwa akitoa taarifa juu ya pendekezo la NSSF la kuchukua kampuni ya Kiwira Coal and POWER Limited kwa wabunge wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAOC).

  Alisema kutokana na hali hiyo, Benki ya CRDB imechukua hatua ya kuiandikia barua serikali ikielezea kusudio la kutaka kuupiga mnada mgodi huo kwa kushindwa kulipa deni hilo ambalo mwekezaji huyo alikopa Dola milioni saba kwa lengo zitumike kuzalisha umeme megawati 50.
  :: IPPMEDIA

  Kiwira ni mradi wa nani?
  Hizo fedha za mkopo zimetumika vipi?
  Kwa sababu gani hii kampuni imeshindwa kurejesha mkopo?

  Serikali ya Mkapa iliuza Kiwira. Serikali ya Kikwete imesema imeurejesha serikalini.
  Kwenye habari ya IPPMEDIA inasema :-

  Mgodi huo ambao hadi sasa upo chini ya mwekezaji wa kampuni ya Kiwira Coal and Power Limited (KCPL) licha ya serikali kupitia Waziri wa Nishati na Madini, William Ngereja, kutoa taarifa kuwa umerejeshwa serikalini,

  Mgodi una deni la zaidi ya Sh.28 bilioni.

  Maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana!
   
 2. N

  Nonda JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, amesema kauli iliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja, kwamba serikali inamiliki mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ni ya kisiasa na imekwenda kinyume cha taratibu za mikataba ya uendeshaji wa mashirika ya serikali.

  Zitto amuumbua Waziri Ngeleja
   
 3. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Huyo waziri hafai ajiuzulu kila mara anatumia siasa kwa masuala ya msingi,mgao wa umeme alisema umekwisha ndo unaongezeka!nahisi ana maslahi binafsi
   
 4. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  isome signature yangu:A S-coffee:
   
Loading...