Benjamin Mkapa Stadium una Taa zaidi ya 200 vipi hivi viwanja vingine?

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Je ni salama kwa wachezaji ? ukiangalia uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa una taa karibia 200 na ushee kwa ajili ya gemu za usiku ila kuna hivi viwanja vingine vina taa hata 5 hazifiki na mpira unapigwa kama kawaida.

Hii imekaaje kitaalamu je hizo taa 4 zinauwezo mkubwa kuliko zile 200 za taifa na je ni mazingira rafiki kwa hizi gemu za usiku au ndio kuumiza macho ya wachezaji, kuna mechi moja imemalizika binafsi nimeona kama mwanga ulikua hautoshi kuna pande zina mwanga mkali na zingine zina mwanga hafifu.

Bila shaka mpira wetu umekua, tumeamua kuwa serious na mpira lakini pia ni vema tukaangalia na usalama wa wachezaji na mashabiki pia kwa kuboresha miundombinu zaidi wataalamu mtujuze kama taa husika ni salama kwa wachezaji wetu.
 
Naomba ufafanuzi kwa wewe ambaye umeishafika hapo uwanja wa taifa. Inaposemwa uwanja wa taifa una taa 200, je zote ni kwa ajili ya kumulika ile pitch ya kuchezea mpira au ni mpaka taa za chooni zimehesabiwa?

Binafsi sijawahi kushuhudia mechi ya usiku Taifa, lakini ukiangalia kwenye TV kuna zile taa kubwa zipo kwenye kama frame za majukwa huwa zinamulika kwenye pitch, je hizo ukizihesabu ndio zinafika 200?
 
Naomba ufafanuzi kwa wewe ambaye umeishafika hapo uwanja wa taifa. Inaposemwa uwanja wa taifa una taa 200, je zote ni kwa ajili ya kumulika ile pitch ya kuchezea mpira au ni mpaka taa za chooni zimehesabiwa?

Binafsi sijawahi kushuhudia mechi ya usiku Taifa, lakini ukiangalia kwenye TV kuna zile taa kubwa zipo kwenye kama frame za majukwa huwa zinamulika kwenye pitch, je hizo ukizihesabu ndio zinafika 200?
Kumuongezea swali, muulize mkapa stadium una capacity ya 60,000 na hizo taa 200.

Je mkwakwani ambayo ni chini ya 10,000 itahitaji hizo taa 200?
 
Je ni salama kwa wachezaji ? ukiangalia uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa una taa karibia 200 na ushee kwa ajili ya gemu za usiku ila kuna hivi viwanja vingine vina taa hata 5 hazifiki na mpira unapigwa kama kawaida...
Una hoja usikilizwe.
 
Taa zile 200 zinazozima pale Yanga au Taifa Stars ikicheza na kuliabisha taifa?

Nafikiri wasiishie kwenye taa bali wahakikishe viwanja vyote vya ligi kuu vina nyasi bandia maana kutunza ukoka hatuwezi. Waendelee tu kuiba ila basi watuongezee japo taa na nyasi tu huko mikoani!!

Nakumbuka Rais wa mawe aliwahi kusema bungeni ataweka nyasi bandia viwanja vitano, sijui kama anafahamu tulikariri suala Hilo na tunamdai maana hatuna Raha ingine njaa inatupiga, mgao wa umeme unatupiga, petrol Iko juu! Yaani kuishi bongo michosho sana Bora kuhamia Burundi tu!!
 
Kuna standard ya FIFA ni kiasi gani cha mwanga unaotakiwa on the pitch,sio kwamba wanajifungia tu taa wanavyojisikia wao.
 
Taa 5?

Tabu lala sasa (tabulalasa)

shida sio wewe ni chama unachoshabikia i predict ukizeeka wewe lazima ushikwe uchawi.

hesabu taa za mkwakwani zipo ngapi, hesabu taa za Kaitaba zipo ngapi, hesabu taa za Jamhuri zipo ngapi ndio uje ulete ujinga wako hapa
 
Back
Top Bottom