Bendera ya uhuru wapi wanaipeleka wanasiasa

Bendera ya uhuru wapi wanaipeleka wanasiasa

Mohamed R

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2013
Posts
2,232
Reaction score
426

NINI MAANA YA BENDERA YETU KUPEPEA?

​
Mnamo mwaka 1961 Tanzania ilibahatika kupeperusha bendera yake mpya ikiimanisha kupata uhuru tena kwa heshima na taadhima kutoka kwa watu ambao tuliamini ni wanyonyaji na hawakupaswa kutuongoza.
Hata hivyo bendera yetu imeendelea kupepea vizuri, tena kwa bahati nzuri Mwalimu J.K aliipandisha juu tena katika eneo ambalo ni pembeni tu mwa Bahari hivyo upepo mwanana wa Bahari kila upitapo bendera yetu ilipepea kuja nchi kavu na kila mmoja alifurahia ilivyopepea kwa upepo huku ikiendelea kuashiria uhuru wetu tena uliokamilika, kwani hata ingetokea tatizo kubwa la kitaifa kama msiba wa kitaifa ingepepea nusu. Jinsi mungu alivyoumba dunia, mara upepo umebadilisha uelekeo na sasa unatoka nchi kavuukielekea baharini hivyo bendera yetu kupepea kuelekea baharini. Kwa kuwa ilipandishwa juu ili ipepee kwa upepo sasa kubadilisha Uelekeo imekuwa tatizo kwa viongozi wetu wanaotaka ipepee kuelekea nchi kavu. Kuuzuia upepo haiwezekani na kuiamuru isifuate uelekeo wa upepo isingekubali maana inatii amri iliyoamiriwa ya kupepe kulingana na uelekeo wa upepo, matokeo yake wameamua kuishikilia isipepe kwenda baharini na hivyo haipepei tena na kwa ushindani uliopo huenda ikachanika.

Kushikiliwa huko inanipa picha mbili

1. Kwa kushikiliwa na kutopepea inaashiria uhuru tulioupata sasa umeshikiliwa na hivyo kukwamisha matunda yaliyotarajiwa na kuwaacha wanauhuru na nembo tu ya kuwa walipataga uhuru.

2. Kama itachanika huenda ndio ikawa mwisho wa uhuru wetu.

Ee Mola tuepushe na haya, au ungewajaalia uwezo wa kufikiria na kutambua hawa wanaoizuia kupepea bendera yetu basi waihamishe na kuiweka chumbani ipulizwe kwa feni na iende uelekeo wautakao pekee, kwani kwa hali ya kawaida kwa upepo unaouongoza wewe mungu lazima tu itageuka, Japo ndio watakuwa wameweka uhuru wetu vyumbani mwao.
Wana JF ni jambo la busara kujadili na kushauri washikilia bendera nini cha kufanya bendera yetu iendelee kupepea kwa utaratibu wa awali na idumishe bila kudumaza uhuru wetu.
​

Ni mtizamo wangu tu, lakini pia inaeleweka kuwa hakuna harusi iyokuwa na wasindikizaji.
 
Acha kukaa kwenye hiko kijiwe cha Kahawa ulichozoea kukaa.
 
Back
Top Bottom