- Thread starter
- #21
Upo sawa ,napenda mtambuwe kiujumla ,hadi sasa hakuna wananchi au mwananchi analalamika ,zaidi ya hawa (Vyama) wakuu wa vyama vya upinzani,hamna.Mfalme Nebuchadnezzar alipoanza kujivunia nguvu zake baada ya kuwashinda maadui unajua nini kilimkuta ???
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ Danieli 4: 30-33 ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Vizuri mtambuwe kuwa hivyi vyama vinavyojiita vya upinzani havina tofauti na mashetani,mabilisi na CCM ni Mtawala alieletwa na Mwenyezi Mungu.
Msitegemee mwenyezi Mungu atawakumbatia mashetani na kumwacha mja wake mwema CCM ,sahauni kuiongoza Tanzania kutakuja siku kuangukie kwa Vyama vinavyojiita vya Upinzani.
Kama mja mwema CCM hupokea mitihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu na baadhi yake huwa inafeli na mingi inayopasi ,hivyo mitihani katika maisha ni kawaida.
Tatizo kubwa lililozuka sasa ni hawa jamaa zangu kuamini ikiwepo Tume huru na katiba mpya ndio wao wataweza kushika hatamu za nchi hii,wanajidanganya na huku ni kujaribu kujenga hoja ili kuwaghilibu wananchi ,wapinzani hawa waliojipachika wapinzani wakuu ,wameiteka hoja hii na kuwa ndio kamba yao ya mwisho kuishikilia na kwa maana nyingine kamba hii ikikatika bazi ndio wamezama na hawazuki tena.
CCM tunajua kuwa hii ndio ncha walioikamata na wanajitahidi isiwaponyoke wala isitekelezwe maana ni wrong turn nyingine kwa wapinzani.