Bendera ya CCM haitaanguka Chini

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,942
3,819
Bendera ya CCM haianguki na hatoigusa mchanga, kabla haijafika chini mwengine anaikamata na kazi inaendelea.

Wapinzani jifunzeni kukata tamaa maana hampo hata kwenye stage za kiushindani ,kama ni uzito basi uzito wenu ni mwepesi sana na bado kabisa kuingia katika ulingo wa mashindani ,mtabomolewa kila siku.

Samahanini kidogo ,ni mfano tu na sifananishi wala sithubutu kuwaweka aina hio ni ile mantiki ndio muhimu kuizingatia.

Sote tunawajua wale wanaoitwa Mbwa koko ,iwe usiku au mchana ukikutana nae ukamtisha basi mbio anazoondoka hapo si za kawaida na ukiokota jiwe ukamlenga nalo halafu limpate kidogo tu hizo kelele zake utasema haponi na ni kama amepigwa risasi.

Mbwa hawa huwa hatarishi pale wanapopata kichaa huwezi kumtisha wala kumtuliza ila kwa kutumia nguvu za ziada.

Vyama vyenu vya upinzani, huo ni mfano hai kimantiki na wanapocharuka inabidi tupate vyombo vya ulinzi na usalama kuwatuliza.

Hivi vyama vya upinzani vimepoteza muelekeo na havina tena dira ni kama viwiliwili vya nyoka waliokatwa vichwa vinasubiri kufa.

Humu CCM tuna taratibu zetu na mambo yetu yamekamilika kabisa,tunalinda utamaduni wa Chama Chetu inapotokea migogoro ya ndani tunasawazishana na wananchi wanatuelewa, na kama haitoshi wanazidi kutuunga mkono na sote tupo pamoja katika kuisimika bendera ya CCM,na Bendera hii haitogusa mchanga na kuanguka ,wapo tupo tutaidaka na kuisimamisha .
 
Awamu hii wapinzani wakiweka Mgombea anayeeleweka wanapata ushindi mapema,we endelea kusujudia iyo bendera
 
Huyu naye anafaidi Mali za nchi hii hila jasho. Siku akiwekwa pembeni akili inarudi anaanza kuongea Kwa mdomo wa kawaida.
 
Awamu hii wapinzani wakiweka Mgombea anayeeleweka wanapata ushindi mapema,we endelea kusujudia iyo bendera
Lini mliweka ? Unajua kumbe hata hamna mgombea anaeleweka,mmekuw kama mikuku yenye njaa ,CCM wakiwatupia kiaina mnaona ndio anaefaa akina Lowasa,Jasusi Mbobezi.

Niliwekeza hapo kuwa nyinyi ni wepesi sana na haya mambo sio saizi yenu,
 
Pole sana.
Majibu ni haya
Mgombea wa upinzani anayeeleweka.
Wao wanaongeza mbinu za wizi zinazoeleweka.

Suluhisho:
Vyama pinzani viweke msimamo mapema kutoshiriki uchaguzi wowote bila Katiba bora na Tume huru.
Vyama pinzani vimeweza kumdharau msajili wa vyama na IGP kususia mkutano wao.
Wakiungana kwa hoja vyama pinzani vitasaidia kupunguza chawa wa CCM
 
Sidhani kama watakuelewa. Tenda wema nenda zako. Siku akili zikiwarudia wataukumbuka huu ushauri.
 
Lini mliweka ? Unajua kumbe hata hamna mgombea anaeleweka,mmekuw kama mikuku yenye njaa ,CCM wakiwatupia kiaina mnaona ndio anaefaa akina Lowasa,Jasusi Mbobezi.

Niliwekeza hapo kuwa nyinyi ni wepesi sana na haya mambo sio saizi yenu,

Hamna chama kinaitwa ccm, bali kuna vyombo vya dola vilivyovaa koti liitwalo ccm ili kufanya siasa. Ccm kama ccm ni chama cha karne iliyopita na kwa sasa haina ushawishi tena kwa kizazi hiki. Hivyo vyombo vya dola pekee ndio imebaki nguzo ya hilo genge liitwalo ccm. Na kama huamini kuwa hamna watu, jaribu kuangalia chaguzi sasa hivi mmeachiwa na mapandikizi yenu lakini hakuna wapiga kura.
 
Hata bendera ya utawala Wa rumi walisema haitaanguka.farao nao waliamini hivyo... Na hata umoja wa Soviet uliamini utatawala dunia.hivyo basi MLETA mada upo sahihi kuwaza hivyo kwamba ccm haitaanguka
 
Bendera ya CCM haianguki na hatoigusa mchanga, kabla haijafika chini mwengine anaikamata na kazi inaendelea.
Wapinzani jifunzeni kukata tamaa maana hampo hata kwenye stage za kiushindani ,kama ni uzito basi uzito wenu ni mwepesi sana na bado kabisa kuingia katika ulingo wa mashindani ,mtabomolewa kila siku.

Samahanini kidogo ,ni mfano tu na sifananishi wala sithubutu kuwaweka aina hio ni ile mantiki ndio muhimu kuizingatia.
Sote tunawajua wale wanaoitwa Mbwa koko ,iwe usiku au mchana ukikutana nae ukamtisha basi mbio anazoondoka hapo si za kawaida na ukiokota jiwe ukamlenga nalo halafu limpate kidogo tu hizo kelele zake utasema haponi na ni kama amepigwa risasi.

Mbwa hawa huwa hatarishi pale wanapopata kichaa huwezi kumtisha wala kumtuliza ila kwa kutumia nguvu za ziada.

Vyama vyenu vya upinzani, huo ni mfano hai kimantiki na wanapocharuka inabidi tupate vyombo vya ulinzi na usalama kuwatuliza.

Hivi vyama vya upinzani vimepoteza muelekeo na havina tena dira ni kama viwiliwili vya nyoka waliokatwa vichwa vinasubiri kufa.

Humu CCM tuna taratibu zetu na mambo yetu yamekamilika kabisa,tunalinda utamaduni wa Chama Chetu inapotokea migogoro ya ndani tunasawazishana na wananchi wanatuelewa, na kama haitoshi wanazidi kutuunga mkono na sote tupo pamoja katika kuisimika bendera ya CCM,na Bendera hii haitogusa mchanga na kuanguka ,wapo tupo tutaidaka na kuisimamisha .
Yaani kuna watu sijui mnatumia nini kufikilia anyway ccm itatoka tu madarakani iwe kwa kura au kwa bunduki ni swala la muda
 
Kimsingi na kama mtu una akili timamu CCM imeishakufa kabisa.
Kinachoendelea ni Uvamizi dhidi ya nchi yetu kwa kutumia jina la CCM
 
CCM ndugu haiondoki ila wanaCCM wataondoka na niliwekeza kwenye msemo bendera ya CCM haitagusa mchanga ,itadakwa kabla haijaanguka na kazi iendelee.

Alipofariki Magufuli mliona njia nyeupe kuelekea Ikulu ,Yaguwjuu ,Raisi Samia Suluhu Hassan, ameudaka mlingoti na bendera ya CCM inazidi kupepea.

CCM tuna utamaduni wetu na njia zetu ,tena za uhakika ,wandugu nakuombeni mtafute kazi ya kufanya au subirini tuwagawie hela ya ruzuku angalau mpate kuibiana ,mara ngapi mnapiga makelele viongozi wenu wamekula hela ya ruzuku.

Huku CCM mmeona utaratibu wetu ulivyoa na mizizi ya nguvu,haitetereki ,wangapi walishughulikiwa,wangapi walitoka huku na kuja kwenu mwisho wa siku nini kimetokea,wamerudi wenyewe na wamekubali walipotea njia,wana kamsemo kanachowatia uchungu wapinzani koko....Tumerudi Nyumbani.

Tunawapokea hasa pale wanaposema walipotea njia ,kuwepo ndani ya Chama cha upinzani ni sawa na kuchukua Wrong Turn. Kuweko huko ni kupotea na si vinginevyo.
 
Hayo ni maneno ya mpiga makelele anaekufa maji ,hamna tena hoja hicho ndio kilio kile nilichokipa mfano wa Mbwa koko ,mnapiga makelele na mayowe ,,,CCM haipo ishakufa...hairudi tena...leteni tume huru...leteni katiba mupya tuone ..!

Nimakelele hayo kwa hayo miaka nenda miaka rudi na bado Bendera ya CCM haijatetereka maana haina wa kushindana nae.
 
Bendera ya CCM haianguki na hatoigusa mchanga, kabla haijafika chini mwengine anaikamata na kazi inaendelea.
Wapinzani jifunzeni kukata tamaa maana hampo hata kwenye stage za kiushindani ,kama ni uzito basi uzito wenu ni mwepesi sana na bado kabisa kuingia katika ulingo wa mashindani ,mtabomolewa kila siku.

Samahanini kidogo ,ni mfano tu na sifananishi wala sithubutu kuwaweka aina hio ni ile mantiki ndio muhimu kuizingatia.
Sote tunawajua wale wanaoitwa Mbwa koko ,iwe usiku au mchana ukikutana nae ukamtisha basi mbio anazoondoka hapo si za kawaida na ukiokota jiwe ukamlenga nalo halafu limpate kidogo tu hizo kelele zake utasema haponi na ni kama amepigwa risasi.

Mbwa hawa huwa hatarishi pale wanapopata kichaa huwezi kumtisha wala kumtuliza ila kwa kutumia nguvu za ziada.

Vyama vyenu vya upinzani, huo ni mfano hai kimantiki na wanapocharuka inabidi tupate vyombo vya ulinzi na usalama kuwatuliza.

Hivi vyama vya upinzani vimepoteza muelekeo na havina tena dira ni kama viwiliwili vya nyoka waliokatwa vichwa vinasubiri kufa.

Humu CCM tuna taratibu zetu na mambo yetu yamekamilika kabisa,tunalinda utamaduni wa Chama Chetu inapotokea migogoro ya ndani tunasawazishana na wananchi wanatuelewa, na kama haitoshi wanazidi kutuunga mkono na sote tupo pamoja katika kuisimika bendera ya CCM,na Bendera hii haitogusa mchanga na kuanguka ,wapo tupo tutaidaka na kuisimamisha .
Kwa aina ya katiba tuliyo nayo , Kiongozi wa timu pinzani ndiye anachagua referee (tume ya uchaguzi), ni kweli unachoongea
Na mtu asiyetumia akili vizuri ndiye anaweza kujisifu
 
CCM ndugu haiondoki ila wanaCCM wataondoka na niliwekeza kwenye msemo bendera ya CCM haitagusa mchanga ,itadakwa kabla haijaanguka na kazi iendelee.

Alipofariki Magufuli mliona njia nyeupe kuelekea Ikulu ,Yaguwjuu ,Raisi Samia Suluhu Hassan, ameudaka mlingoti na bendera ya CCM inazidi kupepea.

CCM tuna utamaduni wetu na njia zetu ,tena za uhakika ,wandugu nakuombeni mtafute kazi ya kufanya au subirini tuwagawie hela ya ruzuku angalau mpate kuibiana ,mara ngapi mnapiga makelele viongozi wenu wamekula hela ya ruzuku.

Huku CCM mmeona utaratibu wetu ulivyoa na mizizi ya nguvu,haitetereki ,wangapi walishughulikiwa,wangapi walitoka huku na kuja kwenu mwisho wa siku nini kimetokea,wamerudi wenyewe na wamekubali walipotea njia,wana kamsemo kanachowatia uchungu wapinzani koko....Tumerudi Nyumbani.

Tunawapokea hasa pale wanaposema walipotea njia ,kuwepo ndani ya Chama cha upinzani ni sawa na kuchukua Wrong Turn. Kuweko huko ni kupotea na si vinginevyo.
Kazi za kufanya tunazo ila tumia tu akili za kawaida na angalia mvumo wa upepo ni bora mkajiaanda kisaikolojia inaweza kuwa wasiwe wakina mbowe ila ccm itatoka hata kwa mtutu
 
Angalia mnavyoenda mbali sana,kama mlishindwa maandamano mtaweza mtutu ? Mkiambiwa mpo wepesi sana kubalini tu,sio mnaingiza sababu za ajabu ajabu,eti hata kwa mtutu,wapinzani ? Mara hii mshakuwa na nguvu za kutuma mtutu ? mlizani siasa ni kukata viuno.

Hizo mbinu za kututuana tumieni huko huko kulisuana na kuwangweana,ila shabah zetu hamziwezi, Raisi aliwahi kuwambia huwa askari WETU hawakosei shabaha.

Halafu yote yanini hayo ? Vyama havina hata Mgombea wa kueleweka ,yaani kama nawaona badala ya watu kuchukia mambo yenu itawabidi wacheke mnavyo okoteza wagombea,mnawachosha sana wananchi .

Mnatafuta huruma kwa CCM ,Oneni alikuwepo Kinana kawapelekesha ,akingia Polepole na Bashiru wakawahenyesha mpaka vyama vingine vikavunjika sasa yupo Shaka huyu mstaarabu kidogo ,hana wakati na kupigashana kelele na wapinzani maana kaona wapinzani hawabebeki ni mzigo ,kaviachia vyombo vya ulinzi na usalama vishughulikie hizi nasari zinajiita vyama vikuu vya upinzani,
Labda niweke hivi
Hivi ukuu gani mlionao ? Hata mkajipachika vyeo eti Chama Kikuu cha Upinzani ! Nina hakika hamna sifa hata moja ya kuitwa Chama kikuu au vyama vikuu labda muongezee vikuukuu,vilivyochakaa ,yaani vinayoelekea kufa. Hamfai hata kupewa ruzuku maana hamna shukurani,siasa zenu hazionekani mpo mnakula hela ya walala hoi bureee !

Ni vyema kabisa sasa mnaonekana si kuwa mpo kama vyama vya siasa bali ni Vyama vya waganga njaa makelele mengiii wakati wa kampeni madebe mabovu, halafu eti ndio mnajipanga kuiangusha CCM.

Hivi mnaijua CCM nyinyi ? nawambieni tena tafuteni kazi za kufanya ila kama unahemea ruzuku kaza kamba usije ukapunjwa na viongozi wako Nina wasiwasi mnaposikia ikisemwa mlingoti chuma na bendera chuma basi huwaga hatutanii,tuna taratibu zetu na mambo yetu huamuliwa kwenye vikao vya ndani ,nyie kimbilieni kwenye vyombo vya habari ,mkimwaga sera 🤓.
 
Hahaha hahaha muda ni mwamuzi mzur soon or later tutakuwa wakimbizi tu
 
Awamu hii wapinzani wakiweka Mgombea anayeeleweka wanapata ushindi mapema,we endelea kusujudia iyo bendera
Hakuna kushinda hata iweje usiwadanganye wapinzani bila tume huru na katiba mabadiliko nchi hii hayawezekani. Nilikwisha sema wapinzani walikosea tangu mwanzo kukubali kuanzisha vyama bila kubadili katiba. Katiba ya chama kimoja nchi ya vyama vingi. Suprimacy of party and president say it all.
 
Mfalme Nebuchadnezzar alipoanza kujivunia nguvu zake baada ya kuwashinda maadui unajua nini kilimkuta ???
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ Danieli 4: 30-33 ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
 
Back
Top Bottom