LACHERO
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 478
- 278
=======
Ben Saanane aibuka
Wakati hofu ikitanda kwamba huenda mwanasiasa Kijana Ben Saanane ameuawa, simu yake imeibuka na kutumika kwenye mitandao ya kijamii, Tanzania Daima Jumapili limebaini.
Ben ambaye alikuwa msaidizi binafsi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, alipotea katika Mazingira ya kutatanisha tangu Novemba Mwaka jana na hadi leo hajulikani alipo, huku familia yake na baadhi ya Viongozi wa chadema wakihofia kwamba huwenda ameuawa.
Hofu kuwa Saanane amekufa iliwahi kutolewa pia na Waziri mkuu Kassim Majaliwa, kwamba hana hakika kama Mwanasiasa huyo chipikizi yupo hai ama ametangulia mbele ya haki. Hofu ya Waziri Mkuu na wengine inatokana na ukweli kwamba hakuna taarifa zozote za kiintelegensia na hata Polisi zinazoonyesha kama yupo hai, kwani hapatikani kwenye simu yake na hata kwenye makundi ya mitandao ya kijamii aliyojiunga.
Hata hivyo jana katika hali ya kushangaza, namba ya Simuvya Ben Saanane iliibua taharuki kwenye mitandao mbalimbali ya Kijamii nchini.
Ben kupitia simu yake ya mkononi jana alionekana akijitoa katika makundi yote ya WhatsApp.
Tukio la Ben Kujiondoa "kuleft" kwenye makundi zaidi ya Matatu, lilitokea jana kwenye majira ya saa tatu asubuhi na kuibua mjadala kwani miezi minanw imepita tangu alipotoweka katika mazingira ya kutatanisha.
Giza hilo lilitanda zaidi April 20 mwaka huu, baada ya kauli ya Serikali iliyotolewa bungeni Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipokuwa akijibu swali la kiongozi wa kambi rasmibya upinzani Bungeni Freeman Mbowe.
Majibu ya Waziri mkuu Majaliwa yalizidisha hofu endepo Ben Saanane angali hai, amefariki dunia au anaendelea kushikiliwa na watekaji.
Namba ya Ben saanane iliyojiondoa katika Makundi jana ni 0768078523(ambayo imesajiliwa kwa jina la Ben Saanane) na mabayo amekuwa akiitumia kabla ya kutoweka Mwaka jana. Makundi ambayo namba hiyo imeonekana kujiondoa(kuleft), ni pamoja na Jukwaa la Siasa, chadema Tanzania, Friends of BAVICHA, Tanzania nchi yetu sote na Bantu Politics TZ kwanza.
"Serikali inalichukuliaje hili, leo(jana) saa 9:10 asubuhi kwa saa za tanzania, Ben Saanane ka-left Magroup aliyokuwa ameungwa...hii inajenga picha gani? " mmoja wa wachangiaji katika Magroup hayo aliandika. Katika group la Jukwaa la Siasa baada ya Ben Saanane kujitoa, mmoja wa Washiriki katika kundi hilo aliandika " Mmmh! hii imekaaje tena, namba ya Ben Saanane imeleft saizi".
Mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, Uenezi mambo ya nje wa Chadema John Mrema alisema "hii imetushitua sana kuona mtu alotoweka simu yake inatumika kwa kujitoa kwenye Magroup, polisi wanafanya nini kubaini alipo Ben Saanane au kujua simu yake ipo wapi?".
Mrema aliongeza: "Hata sisi tunalifanyia kazi sasa, lakini ni wakati wa Polisi kutueleza wameshindwa nini kumpata Ben Saanane, Mbona mtu akicomment kwenye Magroup wanamtafuta na kumpata, kwani wameshindwa kumpata Ben au wanajua alipo?".
Tanzania daima pia ilizungumza na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob, ambaye alisema: "tumefuatilia kwa njia zetu, tumebaini kuwa wakatibnamba hiyo inajitoa ikikuwa 'active' lakini kwa sasa haipatikani".
Jacob ambaye pia ni diwani wa Ubungo(CHADEMA) alisema: " Tunachokifanya sasa ni kuwasiliana na Familia yake ili waombe kujua hiyo namba ilitumika katika simu aina gani baada ya hapo tutajua sasa."
Kuhusu kujitoa katika namba hiyo ambayo haijatumika muda mrefu Jacob alisema: "Hilo haliwezekani, mbona namba za Alfonce Mawazo tangu afariki dunia namba yake haijatoka mpaka sasa ipo, hivyo kuna kitu.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA(BAVICHA), Patrobas Katambi, alimtaka mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro aeleze hatua atakazochukua kuhusu alipo Ben Saanane.
Vijana wa Chadema si kwamba hatuwezi kazi ya mumtafuta, lakini tunawaambia Polisi itafika wakati tutaingia wenyewe mtaani na kuanza kumtafuta Ben Saanane mahali alipo, kwani mpaka sasa hakuna jibu lolote kutoka jeshi la Polisi juu ya mahali alipo" alisema Katambi. Gazeti hili jana lilimtafuta IGP Sirro kupitia simu yake ya kiganjani haikupokelewa na hata Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai(DCI) wa jeshi la Polisi Robert Boaz naye simu yake haikupokelewa.
FAMILIA YASHITUSHWA
Tanzania Daima jumapili ililngea na mdogo wake Ben, Erasto Saanane, kuhusu swala hilo ambapo alisema: "Hata katika group letu la Familia ameleft, imetushtua sana kwani hatujui hasa ni yeye au nani anatumia simu yake. Ilikua kama saa 3:04 Asubuhi, lakini nmewasiliana na Marafiki zake wanasema na wao wameshangaa na ameleft mida ya saa 3, ila wengine wanasema kama saa 3:04, wengine na dakika saba na wengine na dakika 10." aliongeza Erasto.
Ndugu huyo wa Ben alisema Jumatano ya wiki hii, alielezwa na rafiki zake Ben kwamba katika ukurasa wake wa Kijamii wa Facebook, ulionekana ukitumikaukionesha yuko Tengeru Mkoani Arusha.
"... Jumatano kuna rafiki zake wametueleza kwamba akaunti yake ya Facebook ilionesha ikitumika tena akiwa Tengeru huko, sasa hatujui anayetumia ni yeye au ni nani, lakini matukio yote hayo yanazidi kutuchanganya na hili la kuleft magroup... " alisema Erasto.
Alisema baada ya kuona amejitoa kwenye Magroup, ameripoti katika kituo cha Polisi Tabata kwa askari anayeipeleleza na kuelezwa kwamba Polisi huyo atawasiliana na wataalam wa Maswala ya teknologia ya habari na mawasiliano wanaoweza kubaini kwa undani.
MAJIBU YA WAZIRI MKUU
Itakumbukwa wakati wa Maswali kwa Waziri mkuu April ya 20waka huu, Mbowe alimuuliza swali Majaliwa akisema kwanini kama vyombo vya ndani vya dola vimeshindwa kujua Saanane wasiombe ushirikiano kutoka nchi nyingine ikiwemo Uingereza kwa kitengo cha 'Scotland Yard' kama Kenya walivyofanya kumsaka kiongozi wa nchi hiyo Robert Owuko aliyefariki Dunia, lakini baada ya kuchunguza wakapata taarifa.
Katika majibu yake, Waziri Mkuu Majaliwa alisema uchunguzi wa Suala la kutoweka kwa Ben Saanane hauna kikomo na mara utakapokamilika Serikali itatoa taarifa yake.
Majaliwa alitoa kauli hiyo ikiwa imepita miezi sita tangu Saanane alipotoweka katika mazingira ya kutatanisha huku vyombo vya dola vikiwa vikikwepa kuzungumzia sakata hilo.