Ben Saanane ahojiwa kuhusu Mapinduzi ya Burundi

nimemfuatilia kitambo huyu kijana , kiukweli siku hizi ameiva sana .
 
Mkuu Ben Saanane nisaidie katika hili suala ambalo naona kama linaweza kuleta mtanziko wa kidiplomasia:

Tunaambiwa kwamba Maj. Gen Godefroid Niyombare ambaye anasemekana kuipindua serikali ya Nkurunzinza alikuwa mkuu wa idara ya Ujajusi ya Burundi kabla hajatimuliwa na Rais Nkurunzinza na kabla ya hapo alikuwa mkuu wa majeshi. Tunaambiwa alitimuliwa mwezi February 2015 baada ya kumuandikia Rais Nkurunzinza akimuonya juu ya mpango wake wa kutaka kugombea urais term ya tatu.

Tukirudi Uganda, tunaambiwa Rais Gen. Museveni alimfukuza Gen. Sejusa (Tinyefunza) baada ya huyu jamaa ambaye alikuwa mkuu wa idara ya ujajusi ya Uganda kumwandikia Rais Gen. Museveni akimuonya juu ya Museveni kumuandaa mwanaye yaani Brgd. Gen. Muhoozi kuchukua nafasi ya Museveni pindi akiondoka madarakani.

Pia tunaambiwa Gen. Kagame naye alishafarakana na wakuu wake wa Ujajusi wakimpinga juu ya kujifanya mfalme wa Rwanda. Akina Kayumba wakatimuliwa na wengine wakauawa.

Pierre Nkurunzinza, Gen. Kagame na Gen. Museveni wanashabihiana kwa mambo mengi: Wote ni askari, kabla ya kutawala walitokea msituni, wote ni kotapini waliingia kwa nyundo na watatolewa kwa nyundo.

Tunaambiwa ya kwamba Gen. Kagame na Gen. Museveni wana tamaa ya kuendelea kutawala nchi zao ima faima iwe kwa kubadili katiba ama la lakini wanataka kuendelea kutawala kama alivyokuwa anataka kutawala Pierre. Sasa hapa wakikaa viongozi wetu hawa wa EAC kuna utashi wa kumkemea Nkurunzinza? Gen. Kagame anaweza kweli kumkemea Nkurunzinza kwa kuwa kumkemea ni sawa na kujikemea mwenyewe.

Museveni ambaye yupo mamlakani tangu January 1986 anaweza kweli kumkemea Nkurunzinza juu ya kutaka kuendelea kutawala?

Tanzania tunamkemea kwa kuwa tuna moral authority. Kwa maana nyingine ni kwamba Lt. Col. Kikwete akimkemea Nkurunzinza anakuwa anawakemea akina Gen. Kagame na Gen. Museveni in advance. Hii haileti sintofahamu ya kidiplomasia ndani ya EAC? EAC inapita katika tanuru lenye moto mkali
 
Ni uhaini wa demokrasia kwa mtu anaejiita mchambuzi kuendelea kumuunga mkono Piere Nkrunziza. Jumuiya ya kimataifa inawajibu wa kumsaidia Godfroid kumuondoa huyu Dikteta madarakani ili machafuko yakome na hatimae amani irejee Bujumbura.

Haihitaji PhD kujua kwamba PN hahitajiki tena Burundi, bila kujali wanaompinga ni wachache kiasi gani. Ameshaongoza miaka 10 ya kikatiba akae pembeni.

Anang'ang'ania Ikulu kufanyaje leo wakati ameishi hko miaka 10
???

mkuu, Nkurunzinza anasema kwamba kweli katiba inataka atawale vipindi viwili. Lakini pia anasema kile kipindi cha kwanza kilikuwa cha mpito na hakuchaguliwa na wananchi kwenye popular vote bali alichaguliwa na Bunge. Hivyo kwake yeye kipindi cha kuongoza kinaanza pale alipochaguliwa na popular vote. Hivyo anasema bado kipindi kimoja, unasemaje mkuu?
 
mkuu , asante kwa kupanua mjadala .
 
Sasa huyu ben muda 8 badala ya kueleza hali ya burundi yeye anatapika makasa aliyomeza miaka nenda rudi...siku nyingine kijana ukipata muda kama huo usiuchezee kama ulivyouchezea leo..notice za darasani mara nyingine hazifanyi kazi ipasavyo kwenye real life.

Aidha nampongeza ben kwa uwezo wa kumeza vitabu na kukumbuka waandishi...thts scholary work.
 
Mkuu Ben Saanane nisaidie katika hili suala ambalo naona kama linaweza kuleta mtanziko wa kidiplomasia:

Tunaambiwa kwamba Maj. Gen Godefroid Niyombare ambaye anasemekana kuipindua serikali ya Nkurunzinza alikuwa mkuu wa idara ya Ujajusi ya Burundi kabla hajatimuliwa na Rais Nkurunzinza na kabla ya hapo alikuwa mkuu wa majeshi. Tunaambiwa alitimuliwa mwezi February 2015 baada ya kumuandikia Rais Nkurunzinza akimuonya juu ya mpango wake wa kutaka kugombea urais term ya tatu.

Tukirudi Uganda, tunaambiwa Rais Gen. Museveni alimfukuza Gen. Sejusa (Tinyefunza) baada ya huyu jamaa ambaye alikuwa mkuu wa idara ya ujajusi ya Uganda kumwandikia Rais Gen. Museveni akimuonya juu ya Museveni kumuandaa mwanaye yaani Brgd. Gen. Muhoozi kuchukua nafasi ya Museveni pindi akiondoka madarakani.

Pia tunaambiwa Gen. Kagame naye alishafarakana na wakuu wake wa Ujajusi wakimpinga juu ya kujifanya mfalme wa Rwanda. Akina Kayumba wakatimuliwa na wengine wakauawa.

Pierre Nkurunzinza, Gen. Kagame na Gen. Museveni wanashabihiana kwa mambo mengi: Wote ni askari, kabla ya kutawala walitokea msituni, wote ni kotapini waliingia kwa nyundo na watatolewa kwa nyundo.

Tunaambiwa ya kwamba Gen. Kagame na Gen. Museveni wana tamaa ya kuendelea kutawala nchi zao ima faima iwe kwa kubadili katiba ama la lakini wanataka kuendelea kutawala kama alivyokuwa anataka kutawala Pierre. Sasa hapa wakikaa viongozi wetu hawa wa EAC kuna utashi wa kumkemea Nkurunzinza? Gen. Kagame anaweza kweli kumkemea Nkurunzinza kwa kuwa kumkemea ni sawa na kujikemea mwenyewe.

Museveni ambaye yupo mamlakani tangu January 1986 anaweza kweli kumkemea Nkurunzinza juu ya kutaka kuendelea kutawala?

Tanzania tunamkemea kwa kuwa tuna moral authority. Kwa maana nyingine ni kwamba Lt. Col. Kikwete akimkemea Nkurunzinza anakuwa anawakemea akina Gen. Kagame na Gen. Museveni in advance. Hii haileti sintofahamu ya kidiplomasia ndani ya EAC? EAC inapita katika tanuru lenye moto mkali

Mkuu maswali yako utadhan uliingia kichwani mwangu. Kwamba ukiondoa Rais Kikwete na Rais Uhuru Kenyatta,wengine wote watatu wanaounda EAC wote kila sifa wanafanana na PN,iwe PK,YKM7,na cha kukatisha tamaa kama kweli Rais anaeshikilia usukani ni mzee wetu yuleee Robert,basi nikiangalia naona giza totoro kuhusu suala hili la Jirani zetu wa Burundi!

Kaz siyo nyepesi,I could think kaka Ben Saanane atasaidia. Lakini kama Salim Kikeke wa BBC ni memba humu JF, tunaomba utafutwe huko BBC Dira ya Dunia mjadala kuhusu aina hizi za viongoz wanaopenda kung'ang'ania madaraka kwa nini haishi tu Afrika? Kwa nini Waafrika tunaendekeza mambo haya ya Tawala za kiimla!?
 
Hii ni tunu nyingine ila wengi hawajaijua, Ben ni zaidi ya kipaji.maCcm wasimlaghai tu kama kiongozi wetu wa chama(wazalendo).

Ben ni mtanzania, Chadema ni combo cha safari yake ndefu, Tanzania First Party second
 
huyu ben saa nane agombee ubunge ni kijana anayejitambua na ameiva sana.
 
Sasa huyu ben muda 8 badala ya kueleza hali ya burundi yeye anatapika makasa aliyomeza miaka nenda rudi...siku nyingine kijana ukipata muda kama huo usiuchezee kama ulivyouchezea leo..notice za darasani mara nyingine hazifanyi kazi ipasavyo kwenye real life.

Aidha nampongeza ben kwa uwezo wa kumeza vitabu na kukumbuka waandishi...thts scholary work.

Mkuu nakuunga mkono. Katika hali kama hii Mchambuzi anatakiwa kuoanisha hizo theories na hali halisi iliyopo. kwa maana hiyo Ben angeoanisha hizo theories na hali halia ya Burundi hapo nyuma na kwa sasa. Nini kimeifikisha Burundi hapo ilipo? Huyu Nkurunzinza aliingiaje hapo? Historia yake ikoje juu ya utawala? Tungekumbushana pia jinsi Nkurunzinza alivyompoka uongozi bwana Leonard Nyangoma ndani ya CNDD/FDD; tukumbushane jinsi Nkurunzinza alivyomzingua mwenzake ambaye walikuwa wote msituni yaani Bwana Hussein Rajabu, nk.

Mjadala kuhusu mapinduzi ya kijeshi katika dunia na hususan Afrika ni mjadala mtamu na mrefu. Siku nikiwa na wasaa nitatoa makala ndefu juu ya mapinduzi katika dunia na Afrika.

Back
Top Bottom