Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,233
- 138,749
Mwanasiasa na mchambuzi wa mambo ya kidiplomasia na mwana JamiiForum mwenzetu Kamanda Ben Saanane amehojiwa leo na kituo cha Clouds Fm.Pamoja na mambo mengine Mkuu Ben Saanane amechambua nini hasa maana ya utawala wa kijeshi "mtanziko wa kisiasa katika tawala za kijeshi"
Haya hapa ni maelezo yake baada ya mahojiano na Clouds FM
Nilikua Hewani kwa mahojiano na Clouds FM muda mfupi Uliopita kuzungumzia mtanziko wa Kisiasa nchini Burundi na mamlaka za kijeshi kushika hatamu za uongozi katika Serikali za Kiraia
Ndani ya kitabu cha "Mtanziko wa Kisiasa katika Tawala za Kijeshi(The Political Dillemmas in Millitary Regimes) ,Waandishi Christopher Clapham na George Philip walielezea kiutafiti juu ya miundo ,sababu na aina ya Tawala za Kijeshi .
Kwa Ufupi tu ;
-Utawala Turufu wa Kijeshi: Huu ni utawala ambao unaingia madarakani kijeshi kulinda hali/maisha ya kila siku kijamii yaliyozoeleka kuwa ndio utamaduni wa nchi au jamii fulani(Social Order) na Ikiwa Utawala wa Kiraia utaelekea kubadilisha hali hiyo Jeshi linachukua hatua.Utawala huu kwa kawaida hugeuka kuwa utawala kandamizi
-Utawala Mpenyo (Breakthrough) wa Kijeshi: Hapa jeshi linaasi na kunyakua mamlaka dhidi ya utawala wa kiraia kupinga hali au mwenendo wa kawaida kijamii na utamaduni uliopo kisiasa na kijamii kupinduliwa hasa pale unapohatarisha maslahi ya jeshi .Pia utawa huo ni Kandamizi kwa asili yake
-Utawala Simamizi(Moderation) wa Kijeshi: Hapa jeshi linachukua nchi ikiwa kuna mtanziko na sintofahamu ya kisiasa na kujaribu kuziba ombwe la utawala dhaifu wa Kiraia.Mara nyingi utawala wa aina hii huchukua mamlaka na kuleta udhibiti kwa muda kisha hurudisha utawala wa Kiraia na misingi yote ya kidemokrasia. Mwaka Jana Jeshi la Thailand lilifanya hivyo .
Na hata kipindi hiki nchini Burundi ,inawezekana wanamapinduzi wakajitetea kwa hoja hii.Kwa kawaida utawala wa aina hii sio kandamizi
-Utawala Jumuishi wa Kijeshi: Huu ni Utawala unaoingia mamlakani kwa Jeshi kuunga mkono baadhi ya vyama au wanasiasa au kundi la wanaharakati wanaoshabihiana kiitikadi au msimamo kuuangusha utawala wa Kiraia uliopo kama ilivyotokea kule Madagascar pale ambapo Meya wa Jiji la Antananarivo ,Andy Rajoelina alipoongoza maandamano na kuungwa mkono na jeshi kumpindua Rais Marc Ravalomanana.
Kwa kawaida utawala huu sio Kandamizi sana
Katika historia ya mapinduzi ya Kijeshi mara nyingi hapa Afrika Afisa wa Jeshi amekua akitangulizwa mbele kunyakua mamlaka na kuwa kiongozi mkuu wakati Latin America na Bara Asia baada ya mapinduzi kamati maalumu au baraza la uongozi maarufu kama "Junta" hushika usukani katika kutawala
Tangu baada ya vita kuu ya pili ya Dunia wakati nchi za Afrika zinatafuta na kupata uhuru kuanzia miaka ya 1960 na kuendelea ,Dunia ilishuhudia tawala nyingi za kijeshi kunyakua mamlaka.
Mwaka 1979 kwa Afrika Pekee,Tawala 14 za kijeshi zilishika Hatamu
Udhaifu wa kiutawala kwa nchi ambazo ndio zilikua zinepata uhuru tu,Vita Baridi na kambi za Madola makuu mawili ya mhimili wa Utawala wa kisiasa na Kiuchumi Duniani yaani Usovieti na Kambi yake ya Mashariki kwa Upande Mmoja na Marekani na Kambi ya Magharibi ilichochea mapinduzi ya kijeshi hasa kwa Afrika na Latin America
Nakumbuka Katika kitabu cha "The States and Millitary in Latin America" ,Alain Roquie alisema Tawala za kijeshi zilipata umaarufu na kuungwa mkono na wananchi kwa kuwa waliahidi kuwa wataboresha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kama alivyofanya Augustino Pinochet kule Chile mwaka 1974 .
Hata hivyo imani ya wananchi ilipungua baada ya ukandamizaji kukithiri na pia utawala wa kijeshi kushindwa kutekeleza ahadi
Pia mara nyingi Tawala za kijeshi ni rahisi kutumika na mataifa ya nje kwa maslahi yao na pia uzoefu unaonyesha tawala za kijeshi hushindwa kusimamia sera za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.Mara nyingi huishia kununua Silaha na kuimarisha Jeshi
Kwa hiyo ni busara ya kisiasa kutoruhusu hali ifikie huko ambako jeshi linashika hatamu za uongozi kwa sababu sio njia ya uhakika ya kustawisha Demokrasia,Maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Jumuiya ya kimataifa ina wajibu wa kuhakikisha watawala wanaochezea Katiba wanadhibitiwa mapema ili kuepusha hali kama iliyopo Burundi inayotoa mwanya kwa majeshi kuacha jukumu la msingi la kulinda mipaka na kuingia katika masuala ya kisiasa
Kuna mapungufu makubwa ya kidiplomasia kwa jumuiya ya kimataifa katika kupambana na chanzo cha machafuko kwa nchi zinazoendelea
Mikataba ya EAC na AU kwa mfano imeweka vipengele vya kuzibana nchi wanachama kuheshimu haki za kiraia na utawala bora wa Sheria .Pia mapinduzi ya kijeshi hayatambuliki lakini watawala waliopo madarakani wanapochezea katiba au wanapofanya udanganyifu katika uchaguzi hawachukuliwi hatua kali za kidiplomasia ikiwepo kuwawekea vikwazo,Kuwatenga(Isolation) na pia Hatua za Kijeshi kuondoa tawala dhulumati kwa Raia wake ili kuimarisha amani ya kikanda na Ulimwenguni .
Huu ni udhaifu mkubwa kwa taasisi hizi za kidiplomasia
Burundi inahitaji kusaidiwa na jumuiya ya kimataifa.Ikiwa Jeshi litafanikiwa kudhibiti Televisheni ya Taifa na Redio ;pamoja na kufunga Uwanja Wa Ndege na kambi muhimu za jeshi la anga na Ardhini basi Nkurunzinza atakua amepinduliwa Rasmi.
Jumuiya ya kimataifa isaidie serikali ya kijeshi kuunda serikali ya mseto ili iweze kuurejesha utawala wa kiraia na kuandaa Uchaguzi Huru na Wa Haki.
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Robert Mugabe amechelewa sana hadi sasa kutoa mwelekeo wa Kidiplomasia baada ya Maazimio ya EAC jana
Aluta Continua,Victory Ascerta...