Beki 3 Wangu

Wengi hapa tunamshambulia tu huyu mtoa mada, nadhani amejaribu kuhusianisha na hali halisi majumbani mwetu, kitu cha msingi ni kujitambua,inawezekana ukamuamini sana mkeo/mumeo lakini tutambue dunia imebadilika sana,huyo huyo unaemuamini ndio anamtafuna binti wako wa kazi!
 
Mkuu nilikuomba huyo Binti, nina muhitaji sana sana
 

Hakuna neno kaka, ila ningeomba kuliko kumrudisha kwao uniletee mimi kwangu sina house gal :biggrin1:
 
kwanini umrudishe si tuwasiliane tu kwa sisi tusiokuwa na wake
 
Umeongeza matatizo kwa Beki 3 wako na kwako pia. Beki 3 umemtimua ghafla namna hiyo bila notice ya muda.
Je ? umemlipa fidia na haki zake zote kwa kumsimamisha kazi ghafla, au ndio kunya anye kuku na akinya bata kah.........
Bila shaka ulitafuta beki 3 7bu kazi ziliwazidi hapo home, Je? zimeisha kazi.

Wife umempa 7bu gani za kumuondoa beki 3 kama hujamwambia uongo kibao ili kumshawishi akubali ...
Angalia sana maana kila liendalo huwa halikosi kurudi hata kama si kwa njia ileile
 
Hapa kubwa ni kukuombea kwa nguvu zote lakini nawe ufunge na kuomba si kisanii bali kiukweli! Nachelea kukubaliana na ushauri wako wa grace period ya miezi 6 kwa kuwa bado wewe hujashinda katika jaribu hili ulilonalo. Hivyo ukishashinda au kushindwa, tafadhali tupatie mrejesho na hasa namna ulivyoweza kumshinda huyo mwovu sheitwan! Ila aombaye kwa imani hupata anachoomba, lkn ukiomba kwa macho ya mashaka-mashaka, wewe mwenyewe ndiye utakuwa umekuwa sheitwan!

Ushauri tu wa bure, mwambie wife huyu binti ende zake tu maana ukweli anakutia majaribu maana imeandikwa tusiikaribie zinaa, wala husije kujidanganya kwamba utaishinda zinaa kwa maombi wakati iko hapo pembeni yako.... mtimue tu utakuwa salama sana.
 

Hiyo hali huwa inawatokea wanaume wengi sana hasa wenye ndoa hivyo sikushangai sana kutokea kwako zaidi ni kwamba nikupongeze tu kwa kusema hisia zako kwa beki 3 wako. Kumuomba Mungu ni jambo la maana ingawa hatuwezi kumshirikisha Mungu kwa kila Jambo hasa yale ambayo ametupa uwezo wa kutambua kuwa ni mabaya na akili ya kuyashinda kama hili la kwako. kitu cha unatakiwa kuelewa kuwa kama wewe ni baba wa familia hivyo basi na binti wa kazi ni mtoto wako kwani ni sehemu ya familia yako hivyo kitendo cha kumtamani ni tabia chafu ambayo ikijijenga ipo siku utamtamani hata mwanao wa kuzaa. Kitu cha pili nina wasiwasi na mahusiano yako na mkeo kama yapo thabiti kweli. nashangaa unapata wapi muda wa kuangalia maungo ya binti wako wa kazi kama kweli mahusiano yako na mkeo ni mazuri. Jenga tabia ya kuwa karibu na mkeo na jitahidi sana kuepuka hayo mawazo potofu pia ni lazima uwe na mipaka kati yako na binti wa kazi na tafuta cha kufanya hasa unapokuwa nyumbani jioni. Kumbuka kuwa huwezi kumfukuza binti wa kazi kwa makosa na tamaa za ngono za kwako, kwa maelezo yako inaonesha ndio tabia yako kuwafukuza mabinti wa kazi kwa upuuzi wako kitu ambacho ni kinyume na haki za msingi za mwanadamu na kutoheshimu utu wa mwanamke.
 

acha kusema uongo wewe, hapo kwenye red. kwani hujui kuwa uongo nao ni dhambi. we endelea kuangusha udenda tuuuuu .... afu utavuna unachopanda.
 
Haujaambiwa ukemee zinaa, imeandikwa "ikimbieni zinaa. So hata ukifunga na kuomba, utajitesa buuuree zinaa haikemewi. Jogoo akishawika utamkemea aache?? Hakuna kitu kama hcho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…