*Beijing Olympics 2008*

oly33.jpg


oly34.jpg

SteveD, hii ya kupigiwa nyimbo ya Taifa na kuona bendera ya Taifa lenu inapandishwa katika closing ceremony ilinigusa sana. Maana washiriki wote na officials wote wa IOC na host country walikuwepo pale. Hongera sana bingwa wa marathon katika 2008 Olympic kwa kuweka rekodi mpya ya Olympic iliyodumu kwa miaka 24.
 
SteveD, hii ya kupigiwa nyimbo ya Taifa na kuona bendera ya Taifa lenu inapandishwa katika closing ceremony ilinigusa sana. Maana washiriki wote na officials wote wa IOC na host country walikuwepo pale. Hongera sana bingwa wa marathon katika 2008 Olympic kwa kuweka rekodi mpya ya Olympic iliyodumu kwa miaka 24.

...Bubu, sitoficha, what an exhilarating moment that was.... so overwhelming machozi membamba ya furaha na shauku yalinitoka!! Kenyans are one proud nation on face of the planet today!
 
Tanzania Usanii mwingi, uroho mwingi, hatuoni mbali. Zamani tuliukuwa na Umishunta, michezo wa majeshi separately, I mean police, JW, JKT, MAGEREZA, JKU etc, then tulikuwa na UMISETA, UMISAVUTA. Nawakumbuka akina Moris Okinda, suleman nyambui, hata Bayi, Isangura, and lods of them. Itw as possible kuchangua team nzuri, sasa hivi team inachaguliwa then wanabeba kete(boxing issue). wengine wanachagulwa hata sijui kwa cliteria gani. je wenye vipaji tutwapata wapi? training ndiyo usanii. lakini ziara za hewa za viongozi world record hata wanjiru na bolt hawaoni ndani. MWINYI ALISEMA TANZANIA KICHWA CHA MWENDA WAZIMU!! watu walicheka lakini maneno yale mpaka leo hii bado yanarindima masikioni mwangu. ni lini basi tutapata matibabu ya kuondoa uenda wazimu? na hii ni kila nyanja kuanzia michezo, siasa ndiyo kabisa ITU, na hata UCHUMI.
 
...hapa natabiri mawili kutokea;

a) ...itaundwa kamati ya bunge kuchunguza kwanini Tanzania imefanya vibaya mno kwenye michezo ya olimpiki, 2008

au

b)...itakuwa funika kombe mwanaharamu apite, kwa kisingizio mw'mungu hakupenda, huenda 2012 tukapeleka timu nzuri zaidi, mw'mungu akipenda.

...upuuzi mtupu. watu wanalojua ni kupelekana mahakamani kugombea madaraka tu ya kuongoza vyama na vilabu, kutafuta ulaji badala ya kubuni mbinu mpya na kuleta maendeleo kwa michezo na wanamichezo wetu.

2012 hadithi itakuwa hii hii, kupeleka washiriki sio wasindani!

inachekesha kweli, lakini kwa bahati mbaya hii ndio reality!!
 
okay na huku nako tasafali mtufungie hii kitu ya olympics maana inatia machungu kuona twashindwa na vinchi ambavyo hata kwenye atlas havipo!
mkuchika kajiendea zake trip kula bata nw he is back n yet no one dares to open domo askin as to hw n wat kimetokea kwa timu yetu kule china its as if nothin kimetokea!

nikiwa na mijihela yangu mingi nitaanzisha olympics yangu ya uongozi mbovu,ufisadi ambako i bliv ndio tutakua twachukua medali zote zote sijui gold,silver n shaba pia!
 
Aibu ya Tanzania katika Michezo ya Olimpiki

WAKATI michezo mikongwe ya kihistoria ya Olimpiki iliyoasisiwa na wazee wa Kigiriki inatimiza karne moja na miaka 10, Tanzania ina miaka 44 katika ushiriki wake.

Lakini tangu Tanzania ianze kushiriki Olimpiki ya Kimataifa kwa miaka hiyo, kwa takwimu hakuna kikubwa cha kujivunia kwani mafanikio yake ni hafifu.

Katika miaka yote hiyo ya ushiriki wa Tanzania, tumekuwa tukishiriki katika michezo ya aina nne tu, ingawaje mashindano hayo hushindanisha michezo mingi.

Jinamizi hili la Tanzania kushiriki michezo michache, linazidi kuiandama tena mwaka huu, kwani ingawa muda wa mwisho wa kuthibitisha bado, lakini kuna kila dalili kwa mwaka huu tena kuwakilishwa na michezo michache.

Hadi sasa ni takribani wanariadha watano pekee ambao ndio tayari wamefikia viwango vya kushiriki Olimpiki, huku mchezo wa ngumi ukiwa unahaha nao kuhakikisha mabondia wao wanafikia viwango.

Michezo ambayo tumewahi kushiriki ni riadha, ngumi, baiskeli na magongo katika miaka yote hiyo ya ushiriki, na hii inatokana na michezo mingine kushindwa kufikia viwango ambavyo ndio vigezo vinavyowezesha kushiriki.

Mpira wa magongo na baiskeli, Tanzania ilishiriki mara moja tu mwaka 1980 katika mashindano yaliyofanyika katika Jiji la Moscow, Urusi ya zamani huku ngumi ikishiriki mara sita na riadha ikiongoza kwa kushiriki mashindano yote ya Olimpiki iliyoshiriki ndani ya miaka hiyo 44.

Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) ambayo ni mwanachama wa kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) yenye makao yake makuu jijini Athens, Ugiriki, ndiyo mratibu mkuu wa michezo hiyo hapa nyumbani.

Kwa mara ya kwanza, Tanzania ilitinga katika Olimpiki mwaka 1964, katika mashindano ambayo yalifanyika katika Jiji la Tokyo, Japan ambako iliwakilishwa na mchezo wa riadha pekee.

Timu iliwakilishwa na wanariadha sita katika mbio za mita 400, 800, 1,500 na 10,000 sambamba na kiongozi mmoja na matokeo iliambulia patupu na kurejea bila medali.

Kwa mara ya pili, Tanzania ilitinga mashindano hayo 1968 katika michezo iliyofanyika Mexico City nchini Mexico na kwa mara ya kwanza ngumi ilishiriki.

Timu iliundwa na wachezaji watatu ikiwa ni wanariadha wawili na bondia mmoja, huku viongozi wakiwa wawili, ambako pia iliambulia patupu.

Katika michuano hiyo ya Mexico, ngumi haikushiriki licha ya mchezaji kwenda huko, huku wanariadha wakishiriki katika riadha mita 400 na marathoni.

Hata hivyo, mmoja wa wanariadha wa Tanzania, John Steven Akhwari alimaliza mbio hizo akiwa wa mwisho na alipoulizwa, alisema: “Nimetumwa na Tanzania kumaliza mbio na si kuishia njiani.”

Hiyo ilimpa heshima na katika michezo ya Olimpiki ya Sydney, Tanzania ilipata tuzo maalum ya Olimpiki ya Akhwari, ambayo IOC iliahidi kujenga kituo cha michezo kama kumbukumbu yake na kutambuliwa na kamati hiyo.

Mwaka 1972, timu za ngumi na riadha ziliiwakilisha tena nchi katika michezo iliyofanyika Munich, Ujerumani Magharibi ya wakati huo, ikiwa na kikosi cha wachezaji saba na viongozi watatu, ambako ngumi walishiriki katika uzito wa Light Middle na Bantam na kurudi bila medali.

Tanzania tangu ianze kushiriki Olimpiki mwaka huo wa 1964 hadi mwaka huu, 2008 imeikosa michezo hiyo mara moja tu, mwaka 1976 huko Montreal nchini Canada, kutokana na sababu za kisiasa.
Serikali haikuruhusu kupeleka timu huko, sababu kubwa ilikuwa kupinga hatua ya IOC, kuiruhusu timu ya rugby ya New Zealand kwenda Afrika Kusini, ambayo tayari ilikuwa imetengwa kisiasa kutokana na ubaguzi wa rangi.

Baada ya kuikosa michezo ya Montreal, ilijitosa katika Olimpiki ya Moscow, USSR (Urusi ya zamani) 1980 ambako ilishiriki katika michezo ya riadha, magongo, ngumi na baiskeli.

Mashindano hayo ya Moscow ni ya kihistoria, kwani kwa mara ya kwanza ndipo jina la Tanzania lilipoingia katika rekodi ya nchi zilizowahi kunyakua medali katika historia ya mashindano hayo.

Katika mashindano hayo, Tanzania kwa mara ya kwanza na ya mwisho hadi hii leo, iliibuka na medali mbili za fedha, kupitia kwa wanariadha wake Filbert Bayi na Suleiman Nyambui katika mbio za mita 3,000.

Mashindano ya Moscow yalifuatiwa na yale ya Los Angeles, Marekani mwaka 1984 ambako tuliwakilishwa na wachezaji wawili bila kiongozi katika michezo ya ngumi na riadha na kurudi kwenye uvurundaji na kurejea mikono mitupu.

Riadha na ngumi ziliibeba Tanzania tena, katika michezo ya mwaka 1988 huko Seoul, Korea Kusini na kuwakilishwa na kikosi cha wachezaji 17 na viongozi saba katika ngumi na riadha na kumaliza bila medali.

Jinamizi la kuwa ‘watalii’ katika kinyang’anyiro cha Olimpiki ya Kimataifa, liliendelea kuikumba Tanzania tena katika mashindano ya Barcelona, Hispania mwaka 1992 tulikowakilishwa na timu ya riadha pekee iliyokuwa na wachezaji 15 na viongozi saba.

Mwaka 1996, Tanzania iliwakilishwa na mchezaji wa kike kwa mara ya kwanza katika michezo ya Olimpiki huko Atlanta, Marekani.

Timu iliundwa na wachezaji 11 na viongozi watano. Michezo ilikuwa ni riadha na ngumi. Katika riadha ilishiriki mita 800 wanawake na wanaume, mita 10,000 na marathon na kutoka tena kapa.

Tanzania ilishiriki tena michezo ya Olimpiki mwaka 2000, jijini Sydney, Australia na kuwakilishwa na wachezaji watatu katika riadha pekee, ambako walishiriki katika mbio za mita 10,000, 5,000 na marathon.

Baada ya Olimpiki ya Australia, iliyofuata mwaka 2004 ilikuwa ni Athens Ugiriki Athens, yalikoasisiwa na kufanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1894. Tanzania iliwakilishwa na riadha pekee, wakiwemo wanariadha wawili wa kike; Restituta Joseph katika mita 1,500 na 5,000 na Banuelia Brighton ‘Mrashani’ kwenye Marathon, ambako pia iliambulia patupu.

Agosti mwaka huu, Tanzania inatimiza miaka 44 ndani ya Olimpiki ya Kimataifa na mashindano yake ya kumi, yanafanyika katika Jiji la Beijing China.

Hadi sasa wenye tiketi mkononi na kuwa na uhakika wa kushiriki ni takribani wanariadha sita tu wakiwamo Dickson Marwa, Samson Ramadhani na Msenduki Mohammed, huku mchezo wa ngumi wakihaha wachezaji wao wafikie viwango, ambako umebaki mtihani wa mwisho katika mashindano ya kufuzu yatakayofanyika Namibia, Machi, mwaka huu.

Mbali ya ushiriki wa Tanzania katika michezo ya mwaka huu, pia imebahatika kuwa na tukio la kihistoria duniani linalokwenda sambamba na michezo hiyo, nalo ni Mwenge wa Olimpiki ambao utakimbizwa jijini Dar es Salaam, Machi, mwaka huu.

Mwenge huo ambao utakimbizwa miji takribani 59, Dar es Salaam ndilo jiji pekee katika bara la Afrika kupewa hadhi hiyo.

Kasumba ya Tanzania kuwakilishwa na michezo michache inayojirudiarudia, imeendelea tena mwaka huu na kuacha maswali miongoni mwa wapenda michezo na taifa kwa ujumla. Je, kupitia riadha pekee, au na ngumi endapo nao watafanikiwa kupenya, tunaweza kuandika historia tena na kutukumbusha yale yaliyofanywa na Bayi na Nyambui 1980 kule Moscow?

Hii ni changamoto kubwa kwa serikali, TOC na wanariadha wanaounda timu ya taifa kwa vigezo vya kihistoria. Riadha ndiyo inayotuweka katika ramani na rekodi za medali katika michuano hii.

Mtanzania wa kwanza kuleta medali nchini, mwaka 1980, Meja mstaafu Filbert Bayi, ndiye kinara wa TOC, ambaye ndiye katibu wa TOC na mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF). Nini tutarajie huko Beijing, je historia itaandikwa?

Hilo ni swali ambalo ni gumu kulijibu, lakini ukweli kwa takwimu, ni vigumu kuleta medali kwa uchache wa michezo ambayo Tanzania inashiriki, hali iliyosababishwa na kutojipanga na kukosa maandalizi ya muda mrefu katika michezo mbalimbali.

Source:TZ Daima
 
attachment.php


HARARE (Reuters) - Zimbabwe President Robert Mugabe on Friday handed the country's only Olympic medalist in Beijing a $100,000 cash reward for her performance at the games.

Mugabe handed the U.S-based swimmer the cash at a ceremony in Harare carried live on state television.

"Our national spirit must exude joy and pleasure and say you have done well, daughter of Zimbabwe. We are proud of you, we wish you well. She's our golden girl ... take care of her," he said at the ceremony.

The U.S. dollars, scarce in a country struggling with an economic crisis marked by a severe shortage of foreign currency, were carried in a briefcase by Zimbabwe's central bank governor.

Other members of Zimbabwe's Olympic team received between $2,000 and $10,000 each.
 

Attachments

  • mugabe.jpg
    mugabe.jpg
    22.4 KB · Views: 116
Last edited:
CHAMA cha Riadha Tanzania (RT), kimepigwa faini ya dola 160,000 za Marekani baada ya kwenda kinyume cha mkataba wa wadhamini wao Kampuni ya vifaa ya Li Ning ya China wakati wa michezo ya Olimpiki.

Hatua ya RT kudaiwa kiasi hicho cha fedha, ni baada ya kushindwa kutumia vifaa vya mdhamini huyo wakati wa michezo ya Olimpiki, iliyomalizika hivi karibuni jijini Beijing, China.

Kushindwa huko kwa RT kutumia vifaa vya mdhamini, kulitokana na kutokea kutoelewana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), ambao walilazimisha timu hiyo kutumia vifaa vya Puma, ambao ndio wadhamini wa kamati hiyo.

Habari kutoka ndani ya Kampuni ya Li Ning, zinaeleza kuwa RT ambayo ilikuwa na wanariadha wanane katika timu ya Tanzania iliyokuwa na wachezaji kumi, tayari imeishajulishwa juu ya adhabu.

Chanzo hicho, kilizidi kutanabaisha kuwa, mbali ya faini hiyo, pia mkataba huo uko kwenye hati hati ya kuvunjika.

Juhudi za kuwatafuta viongozi wa TOC na RT kuzungumzia hali hiyo, jana zilishindikana.

Malumbano hayo ya matumizi ya vifaa, kati ya TOC na RT yalichukua mkondo mkubwa hadi serikalini, lakini ufumbuzi ulishindwa kupatikana.

RT inadhaminiwa na Li Ning kwa dola 50,000 za Marekani huku TOC ikidhaminiwa na Puma kwa dola 15,000.

Source:Tanzania Daima
 
hao viongozi wa vyama vya michezo wanaona jinsi viongozi wa serikali wanavyoiba wakiwa madarakani na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa baada ya kosa.
sasa wao wafanye nini?
 
Back
Top Bottom