--Wana JF, michezo ya Olympics 2008 huko Beijing China iko mlangoni tu, je Tanzania imejiaandaa vipi na michezo ya mwaka huu?
--Ni akina nani wanajiandaa kutuwakilisha na nikwenye michezo ipi?
--Je tunamatumaini gani safari hii?
SteveD.
Source: mwananchi.co.tzWanariadha Olimpiki kwenda Beijing keshokutwa
Na Sosthenes Nyoni
Date::7/17/2008
WANARIADHA Saba watakaoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Olimpiki Beijing, China mapema Agosti wataondoka nchini keshokutwa tayari kwa michuano hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania, (RT) Suleiman Nyambui alisema kuwa wanariadha hao bado wanaendelea na mazoezi katika kambi yao ya pamoja jijini Arusha.
Aliwataja wanariadha wanaounda timu hiyo kuwa ni pamoja na Samson Ramadhan, Fabian Joseph, Getuli Bayo na Mohamed Msenduki.
Pia wamo Dickson Marwa, Zakia Mrisho na Mwera Samwel.
"Kwa kweli maendeleo ni mazuri, wanariadha wote wapo kwenye safi na wanaendelea na mazoezi jijini Arusha, na tumeamua waondoke mapema ili waweze kuendelea na mazoezi na kuzoea hali ya hewa ya China kabla ya kuanza mashindano"alisema Nyambui.
--Wana JF, michezo ya Olympics 2008 huko Beijing China iko mlangoni tu, je Tanzania imejiaandaa vipi na michezo ya mwaka huu?
SteveD.
Jamani tusikate tamaa! Nadhani tulisha shinda miaka ya nyuma. Juma Ikangaa na Filbert Bayi (hope got the names right) Nadhani kama serikali itawapa makocha na wawakilishi motisha zaidi watashinda. Nani alikuwa anawa train hawa wakimbiaji?? Kuna mtu ameniambia kwamba Juma Ikangaa bado anakimbia kila wiki kutoka Dar mpaka Kibaha nakurudi!
Hakuna kitu wewe subili vijana ndo kwanza wameingia mzigoni utaona mambo yao.Wameondoka na hirizi za kibongo bongo kwa hiyo watashinda tu msihofu unafikiri tutakosa hata kamedal kamoja???
Hili halina mjadala. Tutaia aibu kama tulivyofanya kule Athens 4 years ago kwa sababu hakuna kilichorekebishwa after Athens