Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Misikiti yote imeagizwa kupeperusha bendera za kitaifa ili kuonyesha moyo wa uzalendo miongoni mwa Waislamu.
Kulingana na chama cha Uislamu China ambayo ni idadi ya kiserikali, bendera hizo zinafaa kupeperushwa mahali ambapo zinaonekana vyema Msikitini.
Hatua hii "itaimarisha zaidi uwezo wa kuelewa maadili ya kitaifa na ya umma, na kueneza moyo wa uzalendo miongoni mwa Waislamu wa makabila yote", kwa mujibu taarifa ya chama hicho.
Misikiti pia inahitajika kubadikwa wazi maelezo kuhusu misimamo ya chama tawala cha Communist, na kueleza waumini wao jinsi misimamo ya dini ya Kiislam ili ikite mizizi moyoni mwa waumini.
Chama cha Uislamu China ni shirika la kiserikali lililo na mamlaka ya kuidhinisha Maimamu. Barua hiyo ilizidi kusema kuwa wafanyakazi Msikitini wanafaa kuandaa mafunzo kuhusu katiba ya China na Sheria nyingine muhimu hasa Sheria mpya ya dini inayofanyiwa mabadiliko hivi majuzi.
Chama hicho kilidai kuwa lengo kuu ni kufanya Misikiti iwe maeneo ya elimu kuhusu chama tawala na Sheria za nchi mbali na kuwa maeneo ya ibada na hivyo basi kuwezesha Waislamu kuwa wazalendo.
Kuna Waislamu karibu milioni 23 nchini China na dini hiyo ni miongoni mwa tano zinazotambuliwa rasmi na chama cha Communist ambacho inahusisha na wasioamini Mungu.