Beijing, China: Misikiti yaagizwa kupeperusha bendera kufunza waumini kuhusu chama tawala

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Misikiti yote imeagizwa kupeperusha bendera za kitaifa ili kuonyesha moyo wa uzalendo miongoni mwa Waislamu.

Kulingana na chama cha Uislamu China ambayo ni idadi ya kiserikali, bendera hizo zinafaa kupeperushwa mahali ambapo zinaonekana vyema Msikitini.

Hatua hii "itaimarisha zaidi uwezo wa kuelewa maadili ya kitaifa na ya umma, na kueneza moyo wa uzalendo miongoni mwa Waislamu wa makabila yote", kwa mujibu taarifa ya chama hicho.

Misikiti pia inahitajika kubadikwa wazi maelezo kuhusu misimamo ya chama tawala cha Communist, na kueleza waumini wao jinsi misimamo ya dini ya Kiislam ili ikite mizizi moyoni mwa waumini.

Chama cha Uislamu China ni shirika la kiserikali lililo na mamlaka ya kuidhinisha Maimamu. Barua hiyo ilizidi kusema kuwa wafanyakazi Msikitini wanafaa kuandaa mafunzo kuhusu katiba ya China na Sheria nyingine muhimu hasa Sheria mpya ya dini inayofanyiwa mabadiliko hivi majuzi.

Chama hicho kilidai kuwa lengo kuu ni kufanya Misikiti iwe maeneo ya elimu kuhusu chama tawala na Sheria za nchi mbali na kuwa maeneo ya ibada na hivyo basi kuwezesha Waislamu kuwa wazalendo.

Kuna Waislamu karibu milioni 23 nchini China na dini hiyo ni miongoni mwa tano zinazotambuliwa rasmi na chama cha Communist ambacho inahusisha na wasioamini Mungu.
FB_IMG_1527307930841.jpg
 
Eti "kueneza moyo wa uzalendo miongoni mwa Waislamu wa makabila yote" utadhani waislamu sio wazalendo. Vipi dini na jamii zingine hiyo kitu haiwahusu?
 
Hakuna lolote hapo zaidi ya kutafuta namna ya kuwabana Waislamu..ndo sera za baadhi ya Serikali duniani kote.

Ni kuhakihisha Waislamu hawafurukuti pale walipo, na mifano ipo.
 
Mkuu, kumbe na wewe ni muislamu wa China?
China sijawahi kukanyaga Mkuu sembuse kuwa raia wa huko lakini sio vibaya kujua yanaoendelea kimataifa - dunia ni kijiji nowadays. Sio ajabu yanayofanyika huko leo, kesho yakawa imposed kwingine pia. Nimekuwa interested na mambo machache;

"waislamu wa huko sio wazalendo"? kama ndio, "kwanini"? "Dini na jamii nyingine za huko ni wazalendo"? Kama ndio "kwanini"? Kama sio "kwanini hawakulengwa na utaratibu huo"?

Ni hayo tu Mkuu wangu.
 
Hata hivyo muislamu ndugu yake muislamu
 
Hakuna lolote hapo zaidi ya kutafuta namna ya kuwabana Waislamu..ndo sera za baadhi ya Serikali duniani kote.

Ni kuhakihisha Waislamu hawafurukuti pale walipo, na mifano ipo.
Ila kumbuka China ndio taifa rafiki kwa jamii na nchi za kiislamu duniani kuliko west kwa makafir Mkuu. Imekuwaje tena wanawekewa masharti ya ajabu ajabu na kudhalilishwa eti "kuenezewa moyo wa uzalendo" ndani ya nchi yao wenyewe? Yale ya jamii ya Rohingya hata kututoka vichwani bado, yanazuka tena mengine yasiyoeleweka.
 
Mimi nilikuwa sijui kama china kuna waislamu,na je majina ya kiislamu wanayotumia ni yapi au ni kama ya kwetu kibongo bongo
 
Sio kwamba binadamu ndugu yake binadamu? Kumbe ni tofauti?
Kwa mujibu wa dini ya Kiislam iko hivi..muislamu ndugu yake ni muislamu (kwa maana waumini wa dini ya Kiislam). Na undugu wa Kiislam ni mkubwa kuliko wa kuzaliwa. Ndo maana katika ahadi ya Allah inasema Muumini wakiume na wa kike wanakuwa katika pepo inapita chini yake mito.

Hapa hakuna cha baba wala mama au mtoto wala rafiki, undugu huu unaishia hapa duniani. Ila watakapo kamilisha uchamungu wao hivyo wote huitwa waumini.

Ama asiyekuwa muislamu sheria imetoa ruhusa ya kushirikiana katika mambo yote ya kijamii muda wakuwa hakuamrishi kumuasi Mungu. Hivyo ndo ufafanuzi kwa ufupi mkuu.
 
Anyway, kuna hiyo habari ya April 2017. Source: China bans religious names for Muslim babies in Xinjiang
***

Many couples fret over choosing the perfect name for their newborn, but for Muslims in western China that decision has now become even more fraught: pick the wrong name and your child will be denied education and government benefits.

Officials in the western region of Xinjiang, home to roughly half of China’s 23 million Muslims, have released a list of banned baby names amid an ongoing crackdown on religion, according to a report by US-funded Radio Free Asia.

Names such as Islam, Quran, Saddam and Mecca, as well as references to the star and crescent moon symbol, are all unacceptable to the ruling Communist party and children with those names will be denied household registration, a crucial document that grants access to social services, healthcare and education.

A full list of names has not yet been published and it is unclear exactly what qualifies as a religious name.

China blames religious extremists for a slew of violent incidents in recent years that have left hundreds dead. It has launched a series of crackdowns in Xinjiang, home to the Muslim Uighur minority and one of the most militarised regions in the country.

Uighur rights groups complain of severe restrictions on religion and freedom of expression, and say the attacks are isolated incidents caused by local grievances, not part of a wider coordinated campaign. Young men are banned from growing beards in Xinjiang and women are forbidden from wearing face veils.

Rights groups were quick to condemn the name ban, which applies to dozens of names deemed by Communist party officials to carry religious overtones.

“This is just the latest in a slew of new regulations restricting religious freedom in the name of countering ‘religious extremism,’” Sophie Richardson, China director at Human Rights Watch, said in a statement. “These policies are blatant violations of domestic and international protections on the rights to freedom of belief and expression.

“If the government is serious about bringing stability and harmony to the region as it claims, it should roll back – not double down on – repressive policies.”

Authorities in Xinjiang passed new legislation last month expanding a host of restrictions, including allowing staff at train stations and airports to deny entry to women wearing face veils and encouraging staff to report them to the police.

The new law also prohibits “abnormal beards” and “naming of children to exaggerate religious fervour”. Various cities in Xinjiang previously had rules banned women wear face veils and men with long beard from public transportation, but the new law applies to the entire region.

A Communist party village chief and ethnic Uighur was demoted last month for not having a “resolute political stance” after he refused to smoke in front of Muslim elders. The state-run Global Times newspaper quote another local official as saying cadres should push against religious convention to demonstrate “their commitment to secularisation”.
 
Mimi nilikuwa sijui kama china kuna waislamu,na je majina ya kiislamu wanayotumia ni yapi au ni kama ya kwetu kibongo bongo
Ukiacha majina ya kizungu, ambao wengi wanakariri kuwa ni wakristo, majina yote yaliyosalia iwe ya kikabila au kawaida hakuna tatizo.

Ndo maana waliokuwa wakisilimu enzi hizo toka Adam hadi Nabii Muhammad S. A. W. walikuwa wakibakia na majina yao walikuwa nayo kabla ya kuingia katika Uislamu.

Ijapo kuwa yapo majina ya Kiislam
 
Kwa mujibu wa dini ya Kiislam iko hivi..muislamu ndugu yake ni muislamu (kwa maana waumini wa dini ya Kiislam). Na undugu wa Kiislam ni mkubwa kuliko wa kuzaliwa. Ndo maana katika ahadi ya Allah inasema Muumini wakiume na wa kike wanakuwa katika pepo inapita chini yake mito.

Hapa hakuna cha baba wala mama au mtoto wala rafiki, undugu huu unaishia hapa duniani. Ila watakapo kamilisha uchamungu wao hivyo wote huitwa waumini.

Ama asiyekuwa muislamu sheria imetoa ruhusa ya kushirikiana katika mambo yote ya kijamii muda wakuwa hakuamrishi kumuasi Mungu. Hivyo ndo ufafanuzi kwa ufupi mkuu.
Shukrani kwa ufafanuzi Mkuu. Swali dogo tu nipanue uelewa wangu; hivi kafir aliyemsaidia mwislamu katika matatizo au mwislamu aliyemsababishia mwislamu mwenzie majanga ni yupi wa muhimu zaidi kwa mwislamu huyo aliyesaidiwa au kusababishiwa matatizo?
 
Nakujibu kwa mujibu Kiislam; Undugu wa Kiislam haukatiki kwa muislamu kusababishia majanga muislamu mwenzake. Hayo yote ni maasi atahesabiwa ametenda dhambi.

Ama Kafir akikusaidia katika matatizo atalipwa hapa dunia kwa wema wake. Akhera hana chake. Na utamwitwa ndugu na rafiki kiubinadamu kwa kuwa mko jamii moja duniani, lakini Kiislam hata iweje hakuna undugu.

Ni hivyo mkuu. Kama kuna zaidi uliza
 
Shukrani kwa ufafanuzi Mkuu. Swali dogo tu nipanue uelewa wangu; hivi kafir aliyemsaidia mwislamu katika matatizo au mwislamu aliyemsababishia mwislamu mwenzie majanga ni yupi wa muhimu zaidi kwa mwislamu huyo aliyesaidiwa au kusababishiwa matatizo?
"Kafiri akufaaye si Islam asiyekufaa".
 
Back
Top Bottom