Bei za vitu Kimara imekuaje, mbona kitu cha Shilingi 100 Temeke huku ni 200?

Chapati ya 200 hata huku chaugingi haipo
Chapati sasa hivi inaanzia 300. Tangu vita ya Ukraine ngano ilipanda bei, hata wale waliokuwa wanauza Chapati mbili kwa 500 wamepandish bei na Chapati wenyewe sasa kama gazeti ni nyepesi sana.

Nina kabinti kangu last born asubuhi chai yake anakula na Chapati mbili.

Yani huwa napenda ikipatikana mihogo inayoiva vizuri ndio kitu cha maana asubuhi wachemshiwe Watoto wanywee chai, otherwise kwa hizi Chapati basi ujuwe Watoto hawashibi.
 
fungua duka lako uza Kwa bei ya chini kama temeke..utapiga sana Hela .fursa hyo changamka
 
Temeke ni uswahilini,
Umenikumbusha mwaka 2015 hivi kama sikosei nilisahau kuongeza salio kwenye simu yangu nikapata safari ya ghafla kwenda kusini. Basi nilitafuta vocher ya shilingi 5,000/= kwenye maduka tangu Temeke mpaka Mbagala HAKUNA!!! Baada ya kuuliza maduka kama 10 hivi mwenye duka mmoja akaniuliza "wewe ni mgeni maeneo haya?" Nikamwambia ndiyo. Akasema vocha za bei hiyo utamuuzia nani huku??? Zilikuwepo za 500/= tu!!!
 
Ile barabara ilikuwa ktk bajeti na inaitwa Kikwete High way. Pesa yake ilitoka kipindi Cha Jk 2011 kama sikosei sema viongozi walilala fund ikahamishiwa maji chumvi.
 
fungua duka lako uza Kwa bei ya chini kama temeke..utapiga sana Hela .fursa hyo changamka
Watu hawajui au wanajitoa ufahamu. Chapati utakayokula uswahilini kama Temeke, na chapati utakayokula shehemu kama Kimara aliyosema na chapati utakayokula Masaki zote ni bei tofauti kwa sababu tofauti. Kuanzia ingredients zinazotumika kutengeneza chapati, namna na mazingira zinazovyokaangwa, jinsi zinavyouzwa nk ni tofauti. Mtu asikudanganye, rahisi ni hasara. Ukiona chapati inauzwa rahisi ujue kuna siri ndani yake.
 

 

Mtoa mada akiishi mbezi Beach/Mikocheni/Mbweni si ataandika insha humu ndani.
 

Viungo vile vile sema kiasi cha viungo ndio hutofautiana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…