Bei za mafuta zapanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bei za mafuta zapanda

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mpita Njia, Mar 6, 2012.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hii ni sehemu ya tangazo lililotolewa na Ewura leo

  Bei za jumla na rejareja kwa aina zote za mafuta zimebadilika ikilinganishwa
  na toleo lililopita la tarehe 01 Februari 2012. Katika toleo hili, bei ya
  rejareja kwa mafuta aina zote zimepanda kama ifuatavyo: Petroli
  imeongezeka kwa Sh 153/lita sawa na asilimia 7.67; Dizeli imeongezeka kwa Sh
  119/lita sawa na asilimia 6.01; na Mafuta ya taa yameongezeka kwa Sh
  104/lita, sawa na asilimia 5.35. Mabadiliko haya ya bei za mafuta hapa
  nchini yametokana na mabadiliko ya bei katika soko la dunia na kushuka
  kidogo kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani.
  Thamani ya shilingi imeshuka kwa asilimia 0.13 ikilinganishwa na thamani ya
  shilingi katika toleo lililopita. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya
  mawili zimebadilika kama ifuatavyo: Petroli imeongezeka kwa Sh 152.70/lita
  sawa na asilimia 7.97; Dizeli imeongezeka kwa Sh 118.77/lita sawa na
  asilimia 6.24; na Mafuta ya taa yameongezeka kwa Sh 104.49/lita, sawa na
  asilimia 5.57.
   
 2. Rocket

  Rocket Senior Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  MN nimekuelewa sana!!!!lakini si walisema wanaagiza bulkprocurement!!!!EWURA nao hawana jipya na tumeshawazoea
   
Loading...