Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,716
- 9,051
Kwa ufupi
Ewura imesema bei za jumla na rejareja za petroli, dizeli na mafuta ya taa zimepanda.
Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (Ewura) imetangaza ongezeko la bei za rejareja na jumla ya mafuta ya taa, dizeli na petroli.
Katika ongezeko hilo kuanzia leo Novemba Mosi, 2017 kwa bei ya rejareja, petroli imeongezeka kwa Sh55 kwa lita sawa na asilimia 2.69, dizeli Sh46 sawa na asilimia 2.43 na mafuta ya taa kwa Sh81 sawa na asilimia 4.35.
Taarifa kwa umma iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Mhandisi Godwin Samwel imesema bei ya jumla nayo imeongezeka ikilinganishwa na bei ya mwezi uliopita.
Amesema hilo linatokana na ongezeko la bei ya mafuta katika soko la dunia.
Kwa bei ya jumla, petroli imeongezeka kwa Sh55.49 kwa lita sawa na asilimia 2.84, dizeli kwa Sh46.36 sawa na asilimia 2.58 na mafuta ya taa kwa Sh80 sawa na asilimia 4.63.
“Ongezeko la bei ya mafuta kwenye soko la ndani imetokana na ongezeko la bei za mafuta hayo katika soko la dunia na kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani, fedha inayotumika kununulia mafuta,” amesema Samwel
Amesema bei za rejareja kwa mafuta ya aina zote katika Mkoa wa Tanga nazo zimeongezeka ilikinganishwa na toleo la Oktoba 4,2017.
Samwel amesema kwa mwezi huu, bei za rejareja za petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa mikoa ya Kaskazini zimeongezeka.
Petroli imeongezeka kwa Sh112 kwa lita sawa na asilimia 5.60, dizeli Sh122 sawa na asilimia 6.52 na mafuta ya taa Sh128 sawa na asilimia 7.10.
Amesema kulinganisha na bei za mwezi uliopita, bei za jumla zimeongezeka pia. Petroli kwa Sh111.57 kwa lita sawa na asilimia 5.93, dizeli Sh122.44 sawa na asilimia 6.93 na mafuta ya taa kwa Sh128.49 sawa na asilimia 7.56.
“Ongezeko la bei za mafuta mkoani Tanga limetokana na ongezeko la bei za mafuta hayo katika soko la dunia na kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani, fedha inayotumika kununulia mafuta,” amesema.
Kaimu mkurugenzi mkuu huyo amesema kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani lakini zisivuke bei kikomo kama ilivyotolewa na kanuni iliyopitishwa na Ewura.
“Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika,” amesema Samwel.