Habari zenu wadau . yaani nashindwa kuelewa mpaka sasa hii bei ya umeme Kigoma ni hapahapa Kigoma au Tanzania nzima .
Sasa hivi huku Kigoma wale ambao walikuwa wanatumia matumizi ya kawaida wote wamepandishwa kwenda matumizi ya juu.
Mfano kipindi cha nyuma nilikuwa nikinunua umeme wa elfu mbili napata unit 16.4 ila katika kipindi hiki tangia korona hii ianze elfu mbili napata unit 5.7 . yaan sijui kwanini au na mikoa mingine imepanda bei hii ya umeme?
Naona sasa tunaanza kurudi kwenye sola maana hali imekuwa ngum mno
[/Qmakuu. Kwanza nitangulize kwa kusema, Mimi sio Mfanyakazi wala agent Wa Tanesco lakin kwa mtazamo wangu mabadiliko ya bei za units kwa mkoa wetu yanaweza sababisha na mambo kadhaa.
1:Mkoa haujaunganishwa na grid ya taifa hivyo kutumia mitambo yake michache kufua umeme Wa mjin mpaka vijijin.
2: Ongezeko la wateja(watumiaj) hii inaweza kupelekea ongezeko LA gharama kwa units kwasababu mwanzo huduma ilitolewa sehemu chache( mjini) lakin kwa sasa umeme umeunganishwa mpaka vijijin (Lea).kwahiyo lazma gharama za kuiendesha mitambo yafulia umeme ipande ukizingatia tuna mashine chache za kufulia umeme huo.
3:Asili ya umeme wetu, kiukweli hapa ndo panatukwamisha mkoa wetu kupiga hata kwan tumekuwa tukitegemea MAFUTA kuendesha mashine za kufulia umeme. Hii ina sababisha kukosa wawekezaji Wa viwanda kwakuwa hatuna umeme Wa uhakika,Ipo haja ya selikali ya mkoa wetu kuangalia njia mbadala ya kuzalisha umeme Wa ziada kama vile , Maporomoko ya mto Malagalasi,Soral power nk.
4: Janga la Covid19, Kutokana na chi nyingi kuchukuwa hatua za kufunga mipaka ili kuzuia maambukiz ya ugonjwa huu imepelekea kukosekana kwa kwa mafuta ya kutosha kutokana na usafirishaj wake kuwa Wa taabu.
IPO haja ya shirika husika kufanya mikakati na kuhakikisha inatatua changamoto hii ili upatikane umeme Wa uhakika, ukizingatia mkoa wetu ni miongon mwa mikoa michache yenye rasilimali rukuki za kuwavutia wawekezaji kikwazo kinakuja, Watawekeza viwanda pacpo umeme wa uhakika?.Inashangaza sana pale unapo litazama ZIWA TANGANYIKA kwa ukubwa na kila aina ya samaki waliomo lakin hatuna kiwanda hata cha kuchakata minofu!!.Pia ina shangaza kuona mji umezungukwa na kushehen MICHIKICHI ila hatuna kiwanda cha kuzalisha KORIE!!
Ipo haja ya viongozi wetu kujitafakari upya nin na niwapi wanakosea,Mkoa wetu ulipaswa kuwa miongon kwa majiji ya kibiashara ukizingatia tumezungukwa na nchi Tofaut za maziwa makuu