Pistol
Senior Member
- Oct 13, 2015
- 194
- 86
Wakati bei ya sukari ikiendelea kuwa juu na serikali kupandisha bei elekezi ya bidhaa hiyo hadi kufikia 2300, Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage amesema upatikanaji wa sukari utaongezeka kwani baadhi ya viwanda vya ndani vimeshaanza uzalishaji.
Akizungumza katika mahojiano na redio moja hapa nchini, Mwijage amesema uzalishaji wa sukari umeanza tangu Mei 18 katika kiwanda cha Kagera Sugar ambacho kilianza uzalishaji wa tani 150 na sasa wanazalisha hadi tani 200 kwa siku,
“Kilombero Sugar pia imeshaanza na inazalisha tani 230 kwa siku na tunategemea itafikia tani 500 kwa siku hapo baadaye,” alisema Mwijage.
Mwijage aliongeza kuwa, kiwanda cha TPC kilichopo mkoa wa Kilimanjaro, kinategemewa kuanza uzalishaji June 18 na kinategemewa kuzalisha tani 150 kwa siku na baadae kuongezeka hadi tani 400.
Mwisho wa mwezi wa saba Kiwanda cha Mtibwa ambacho kwa sasa kipo katika matengenezo nacho kitaanza kazi.
Mwijage alisema uzalishaji utakapokuwa mkubwa bei ya sukari itashuka kwa kiwango kikubwa hivyo kuwataka wananchi kuwa na subira.