Bei ya sembe juu: Mama ntilie wasitisha kupika ugali wa bei rahisi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Habari wakuu,

Bei za vyakula bei juu, gesi juu, mkaa juu,umeme juu... Twafaaa
mama ntilie.jpg

Mama ntilie sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam wameacha huduma ya chakula aina ya ugali kutokana na bei ya sembe kupanda. Awali bei ya sembe ilikuwa sh. 900 ambapo mama lishe waliweza kumudu ila sasa imependa mpaka 1800-2000 na kupelekea mama ntilie kusitisha.

Bei ya sahani ya ugali na mboga ilikuwa sh. 1000, kilo moja ilikuwa inatoa sahani 4 za ugali. Wateja wamekuwa wakikomalia bei ile ile ya zamani huku mama ntilie wakizidi kula hasara na kupelekea kusitisha huduma hiyo isipokuwa kwa oda maalum.
 
Hamna anaetaka biashara ya hasara so lazima wapandishe ikishindikana wanaacha hiyo biashara, na bado bidhaa zinapanda kila kukicha kama mahindi na mchele ndo vinapanda na ni nafaka zinazoliwa kwa wingi
 
Mkuu unajua wanaokula chakula cha buku ni wengi sana, tembelea maeneo ya viwanda, sites kubwa kubwa na hata ndogo ndio utaona. Na hawa watu ni wa kipato cha chini na chakula chao kikuu ni ugali. Bei za vyakula zinawaathiri sana, mama lishe pia maana wanaishi kwa kutegemeana. Mama lishe kupandisha bei sio solution.
 
Safi sana endeleni kudai vyeti feki vya Bullshit vitapunguza bei vikipatikana.
 
Mkuu unajua wanaokula chakula cha buku ni wengi sana, tembelea maeneo ya viwanda, sites kubwa kubwa na hata ndogo ndio utaona. Na hawa watu ni wa kipato cha chini na chakula chao kikuu ni ugali. Bei za vyakula zinawaathiri sana, mama lishe pia maana wanaishi kwa kutegemeana. Mama lishe kupandisha bei sio solution.
Mfano wewe ndo unafanya biashara ya chakula na una mgahawa wako unanunua unga kilo 2000.utakubali kuuza ugali kwa 1000 kisa wahitaji ni wengi? Na wewe lengo lako ni kupata faida na maisha mengine yaendelee
 
Biashara mbuzi hizo. Nasema suluhusho ni serikali kusimamia bei ya vyakula.
 
Sasa kama wamesitisha kutupikia ugali hao mama nntilie tutegemee kudhoofika watanzania,Mama nntilie ndo wanaotuweka mjini kwenye mishe zetu,
 
Back
Top Bottom