Bei ya maziwa ya unga kupanda

maranyingine unajigeuza akili, hivi ng'ombe wa kimasai, kisukuma, kigogo nk wana msaada gani ktk uchumi zaidi ya nyama mbovu?
 
Ni fursa kwa wafugaji wa ng'ombe wa maziwa na wazee wa viwanda.Tanzania tumechelewa sana yaani viwanda vya usindikaji maziwa vikiwa vya kutosha watu tutaanza kufuga kwa kasi kama Kenya.
Kabisa, wasio elewa watabaki kulalamika na kulia lia tuu
 
Tena waongeze zaidi mkuu
 

Ungejua hata Azam hiyo tozo mpya inamhusu usingesifia huu ukurupukaji wa serikali.
Serikali ilitakiwa kwanza kuhamasisha unywaji wa maziwa nchini, consumption ya maziwa nchi per capita ni ndogo na hii inadhihirishwa na ziara ya makamu wa rais huko Mbeya. Takwimu zinaonyesha mkoa wa Mbeya unaongoza watoto kudumaa pamoja na kwamba ndio miongoni mwa mikoa inayozalisha Chakula kingi nchini. Hapa maana yake ni kwamba watoto wetu hawapati virutubisho , maziwa yakiwemo.
So nj muhimu kwa serikali kuhamasisha unywaji wa maziwa pamoja na ufugaji wa kibiashara.
Tanzania inasifika kuwa na ng'ombe wengi but hatuna mazao bora toka kwa mifugo hiya, ng'ombe anaetembezwa toka shinyanga hadi Morogoro, Dar au Mbeya kutafuta marisho hawezi toa nyama bora au maziwa ya kutosha tuache kujifariji. Maziwa hayatoshi, Azam anazalisha maziwa kutumia powder milk, Asas anatamba na Yoghurt tu tena ni zao la powder milk,yule wa Darfresh na Tangafresh hawawezi tosheleza mahitaji.
Tunatengeneza ukiritimba kwa gharama ya mlaji.
Nakumbuka Magufuri alipokuwa waziri wa mifugo aliwahi toa Takwimu ya unywaji maziwa kwa nchi yetu kwa siku ni kama kijiko kimoja kwa kila mtanzania, sijui leo takwimu zinasemaje.
Serikali isikwepe jukumu na kuwaumiza walaji, ijitose, itengeneze sera , mifumo na vivutio ili kuvuta watu wawekeze, wenzetu wanafananisha maziwa na gold kiasi kwamba maziwa wanayaita 'Whitegold'
 
Hii nchi sijui imepigwa mtama na nani ?
 
Umasikini wa kufikiri na Elimu mbovu na roho mbaya ndio inapelekea Nchi kuwa na sheria za kukandamizana kila kukicha...
 
Tatizo lako huoni picha kubwa, look at the big picture, tunachofanya kwa sasa ni kuvunja ile ' vicious cycle'. Tutakapoweka hivi vikwazo ni kwamba watu wengi sasa watahamasika kufuga kisasa (Zero grazing) ili kuweza kuziba pengo kubwa litakalojitokeza (demand ndio asset kubwa iliyopo),kweli mwanzoni tutaumia kwani kutatokea upungufu mkubwa wa maziwa na yalipo yatauza bei kubwa sana ( demand vs supply) na bila shaka kila mti mwenye mtaji atavutiwa sasa kujitosa katika ufugaji bora wa kisasa ( sio wa kienyeji) ambao utazalisha maziwa bora na kwa wingi ili kuzina pengo kwenye soko, kiwango cha supply na demand kikisha stabilize basi bei itashuka na tutakuwa 1.) tumeongeza ajira kwa kiasi kikubwa 2.) Tutakuwa tumeokoa hizo bilionj 160 pesa ya kigeni kuagiza maziwa 3.) Tutaongeza ukusanyaji wa kodi 4.) Tutapunguza utapiamlo kwa watoto 5.) Uchumi kwa ujumla wake utakuwa. Hivi mnawekaga konokono humo vichwani au huwa mnajitoa akili kwa makusudi?
 
maranyingine unajigeuza akili, hivi ng'ombe wa kimasai, kisukuma, kigogo nk wana msaada gani ktk uchumi zaidi ya nyama mbovu?
Maziwa yatakapopanda bei, wafugaji watahamasika sasa kufuga kisasa na kutoa maziwa bora kwani kutakuwa na soko kubwa na la uhakika na la bei nzuri, tofauti na sasa ambapo tunaingiza maziwa cheap artificial kwa wingi kiasi tunawaumiza wafugaji na wanakosa uwezo wa kujiboresha ili kufuga kisasa, demand ikiongezeka hata mabenki yatawakopesha kwani soko ni la uhakika, tumia akili kidogo basi.
 
Labda Tanzania ina Ng'ombe Dume wengi.
 
Unachokisema kinaweza kuwa na ukweli in the long run, but ili kufanikisha hayo uliyoyasema ni lazima sasa serikali iweke mazingira mazuri ya uwekezaji kuvutia watu kuwekeza katika sekta husika. Sikumbuki vizuri Tz ipo nafasi gani katika Doing business report.

Maana changamoto kubwa katika uwekezaji Tanzania kwa my humble views ni pamoja na unpredictable Policy changes pia access to Finances ni tatizo.

Sasa kama tunataka kutengeneza demand kuvutia locals kujiingiza katika uwekezaji nadhani sasa ni wakati wa kutengeneza mazingira mazuri ili muwekezaji apate comfort na kile anachowekeza
 
Nakubaliana na wewe 100%
 
Wadau kodi ya maziwa ya kutoka nje Ume panda kwa asimia 1200,
He ni Gilda kwa wafugaji wetu na kweli wanauwezo wa Kukidhi mahitaji?
Binafsi naona ni fulsa kwa wanaotaka kujiajili kwenye shughuli ya ufugaji
 
Wadau kodi ya maziwa ya kutoka nje Ume panda kwa asimia 1200,
He ni Gilda kwa wafugaji wetu na kweli wanauwezo wa Kukidhi mahitaji?
Binafsi naona ni fulsa kwa wanaotaka kujiajili kwenye shughuli ya ufugaji
Vita ya tariffs imehamia Tanzania
 
Ujue ng'ombe wetu wengi ni wa kienyeji hawatoi maziwa mengi, hata nyama zao sio standard kwa ajili ya export! Ni kama pua kuonekana kubwa lakini makamasi kama ya pua ndogo tu!
 
Bila kubadilika namna ya ufugaji wa watanzania walio wengi tutegemee bei kupanda tena na tena
Kuna wakati unashindwa kujua hivi wafugaji wanchi hii wanafuga kwa purpose ipi.
Nyama au maziwa au breed ya Mbegu.
Kiukweli ufugaji wao haupo Katika lengo la kuleta mazao yeyote kati ya hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…