Bei ya maziwa ya unga kupanda

Bei ya maziwa ya unga kupanda

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,158
Reaction score
162,576
Kuanzia sasa, wateja wa maziwa ya kopo watalazimika kuumia zaidi baada ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitisha kanuni zilizopaisha tozo ya kuingiza maziwa nchini kwa zaidi ya asilimia 1,200.

Agosti 18, 2018 Waziri wa wizara hiyo, Luhaga Mpina amesaini kanuni mpya za huduma za mifugo na bidhaa zake ambazo pamoja na mambo mengine, zimeongeza tozo ya maziwa yanayoingizwa nchini kutoka Sh150 kwa kilo moja mpaka Sh2,000 sawa na ongezeko la asilimia 1,233.

Kutokana na mabadiliko hayo, wateja waliokuwa wananunua kopo la lita moja kwa Sh3,200 sasa hivi watatakiwa kulipa takriban Sh6,000 kwa kiasi hicho.

Viwanda vya kusindika maziwa nchini, takwimu zinaonyesha vinahitaji lita 700,000 lakini uzalishaji uliopo ni asilimia 40 hivyo kulazimu kuagiza kiasi kikubwa kwa ajili ya uzalishaji.

Katika uagizaji huo, Tanzania hutumia zaidi ya Sh165 bilioni kuagiza maziwa kutoka sehemu tofauti duniani. Kabla ya mabadiliko ya kanuni za wizara, ilikuwa rahisi kufanya hivyo lakini mambo yamebadilika hivi sasa.

Mmoja wa wadau wa sekta ya maziwa nchini, Samuel Makubo anasema hili ni pigo si kwa waagizaji tu bali sekta nzima ya maziwa.

“Uzalishaji nchini haukidhi mahitaji. Viwanda vya maziwa vitashindwa kuagiza malighafi na vikilazimisha basi bidhaa zao zitauzwa kwa bei kubwa. Wananchi tutalazimika kunyang’anyana kiasi kidogo kinachozalishwa nchini,” amesema
 
Ubaya wa serikali yetu inapitisha sheria au kanuni mpya juu ya bidhaa au huduma bila kujiridhisha upatikanaji wake kama ni wa kujitosheleza au la, wao wakiwa pushed na wafanya biashara wanatekeleza.

Utapandisha bei maziwa ya nje, ya ndani yatahitajika zaidi kuliko kawaida, na kwa kua wafanya biashara wa kitanzania wamejaa uswahili wakijua hakuna bidhaa toka nje wanaficha kwenye magodauni ili bei ipamde wapige faida in the short run alafu baadae wanaishiwa mzigo tunabaki kulia tena.

Mambo mengi hii nchi hatujajitosheleza, wateja wapo ila uzalishaji hakuna, masoko ya nje yanajazilishia upungufu, serikali kuweka kodi kubwa maana yake itaathiri upatikanaji wa maziwa kwa kiasi kikubwa.

Subiri utaona matokeo yake.
 
Kuanzia sasa, wateja wa maziwa ya kopo watalazimika kuumia zaidi baada ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitisha kanuni zilizopaisha tozo ya kuingiza maziwa nchini kwa zaidi ya asilimia 1,200.

Agosti 18, 2018 Waziri wa wizara hiyo, Luhaga Mpina amesaini kanuni mpya za huduma za mifugo na bidhaa zake ambazo pamoja na mambo mengine, zimeongeza tozo ya maziwa yanayoingizwa nchini kutoka Sh150 kwa kilo moja mpaka Sh2,000 sawa na ongezeko la asilimia 1,233.

Kutokana na mabadiliko hayo, wateja waliokuwa wananunua kopo la lita moja kwa Sh3,200 sasa hivi watatakiwa kulipa takriban Sh6,000 kwa kiasi hicho.

Viwanda vya kusindika maziwa nchini, takwimu zinaonyesha vinahitaji lita 700,000 lakini uzalishaji uliopo ni asilimia 40 hivyo kulazimu kuagiza kiasi kikubwa kwa ajili ya uzalishaji.

Katika uagizaji huo, Tanzania hutumia zaidi ya Sh165 bilioni kuagiza maziwa kutoka sehemu tofauti duniani. Kabla ya mabadiliko ya kanuni za wizara, ilikuwa rahisi kufanya hivyo lakini mambo yamebadilika hivi sasa.

Mmoja wa wadau wa sekta ya maziwa nchini, Samuel Makubo anasema hili ni pigo si kwa waagizaji tu bali sekta nzima ya maziwa.

“Uzalishaji nchini haukidhi mahitaji. Viwanda vya maziwa vitashindwa kuagiza malighafi na vikilazimisha basi bidhaa zao zitauzwa kwa bei kubwa. Wananchi tutalazimika kunyang’anyana kiasi kidogo kinachozalishwa nchini,” amesema
Sukari yenyewe tuu inapatikana kwa manati sembuse maziwa? Wacha waongeze bei bhana urasimu wa kumwaga pesa nje upungue
 
Kwanini uagize maziwa toka nje ya nchi ilihali Tz inaongoza kwa kuwa na ng'ombe Afrika? Huoni kama kwa kuagiza maziwa unaua viwanda vya ndani kama vya Azam, Tanga fresh, Dar fresh na wengine? Napendekeza kodi ipandishwe mara 100 zaidi ili kuinua viwanda vya ndani. Ukiimport maziwa pia una export ajira
 
Hakuna kingine maamuzi yamekaa kisiasa zaidi,yakisukumwa na visasi dhidi ya wafanyabiashara wa Maziwa.

Mfanyabiashara wa leo, unahitaji kuwa na Moyo mgumu sana kukabiliana na changamoto toka kwa watawala wetu..

Mazingira kibiashara siyo rafiki kabisa kwa nyakati hizi tulizo nazo.
 
Back
Top Bottom