CNN Breaking news: Oil dips below $50 a barrel on New York exchange for the first time since reaching record high of $147 in July.
Over 50% ni taxes, wauza mafuta watapunguzaje bei kama taxes ziko juu namna hii?
Wakuu ebu naomba mnipe hesabu za kitu hiki maanake tusiwe tunazungmza tuuu na kulaumu sana wakati hatujaangalia vitu vinavyosababisha mafuta kuwa bei ghali kiasi hicho..
Kwanza kabisa Barrel moja la mafuta ilipokuwa ghali ilikuwa Usd. 150 (147), na lina lita kitu kama 116.. Hapa tu utaona bei ya mafuta machafu ni hiyo $150 gawa kwa hizo lita 116 upate kwa lita au sio!.. Ni bei ya njugu kabisa..
Sasa ikiwa tumeuziwa kwa bei ya sh. 2000/= kwa lita bila shaka hii imetokana na gharama nyinginezo..Gharama ya usafiri na kafaida, usafishaji na ka faida, Kodi, storage(kafaida) kisha bado kuna gharama za wenye station za mafuta na kafaida kao..
Hizi gharama za matumizi zote haziwezi kupungua hata kama mafuta ni dollar 30 au 150, zinasimama pale pale ama kuongezeka...
Hivyo basi ukweli unaangukia kwamba gharama kubwa ya mafuta ipo nje ya bei ya barrel na kama sikosei mwaka 2003 barrel moja lilikuwa likiuzwa kitu kama Us dollar 30 tu na watu walilipa sh. 1200/= kwa lita ya mafuta safi, sasa jaribu kupanda na hiyo bei ufikie bei mafuta yalipokuwa juu, hiyo 150 utaona ni mara mara 5 (toka 30 hadi 150)..Je, hivi kweli mnataka kunambia bei ya mafuta mwezi October ilitakiwa iwe Sh.1200/= mara 5?..
Sidhani!..Ni kweli Bongo wafanya biashara wanatulima kishenzi lakini wakuu zangu sidhani kama mmetazama upande mwingine wa shilingi..
Mag3,
Umezungumzia pia kupungua kwa bei kunamwezesha mnunuzi kununua mafuta mengi zaidi..Mkuu, biashara ya kibongo haiendi hivyo mbali na ukweli kwamba kiuchumi unaagiza mali (supply) kulingana na mahitaji (demand) kwa hiyo hata kama bei itakuwa chini bado utaagiza mafuta kulingana kiwango cha mahitaji ya matumizi..
Mkuu Ibrah,Hatimaye bei ya Petroli na Dizeli zimelingana huku Bara. Bei ya Petroli/Dizeli ni 1440/- kwa lita. Naamini kwa hali ilivyo kwenye soko la dunia kwa mafuta kushuka kwa zaidi ya 50% bado bei inaweza kufika hadi shs 1000/- kwa lita .
Kama huwa tunazingatia vigezo vya kupanda bei ya mafuta soko la duniani katika ku-justfy kupandisha bei hapa nchini inatupasa kutumia vigezo hivyo hivyo katika kushusha na si kupiga porojo kama tunavyofanya wengi wetu hapa JF kujaribu ku-justfy kwa nini bei ya mafuta nchini mwetu haishuki wakati wazalishaji wenyewe wameshusha!
Mkuu Ibrah,
Mimi mbona nanunua Tshs 1,600/= au Tshs 1,590/= per litre hapa Dar? Wapi huko mkuu, tupeane deal maana nahisi napigwa changa la Macho. Kituo gani hicho? Manake hata kile cha Mandela kati ya Buguruni na Tabata ambacho hujulikana kwa kuteremsha bei bado wamegomea Tshs 1,500/= per litre kwa petrol.
Halafu kuna vituo vinahisiwa kuchanganya mafuta, hili linanifanya nishindwe hata kujaza mafuta Big Bon, Camel na OilCom, unaweza kunipa dodoso ni vituo gani vinahisiwa kuchanganya mafuta?
Oil falls below $67 a barrel on demand worries
Thursday, October 23, 2008
Oil prices plunged to their lowest in 16 months Wednesday as global economic worries led investors to predict a further drop in energy demand.
The continuing slide in prices is good news for drivers. The nationwide average gasoline price is now the lowest in nearly a year and is set to fall further.
The price of a barrel of light, sweet crude trading for delivery in December fell $5.43, or 7.5%, to $66.75, the lowest since June 2007. Oil prices are now down 54% from the record close of $145.29 on July 3.
MY TAKE: Hii ni kwa ajili ya nchi zilizoendelea pekee kwa kuwa nyumbani bei bado zile zile?, au ni uongozi wetu na siasa zisizoeleweka?.
Tuijadili..
Makubwa haya, Arusha iwe bei pungufu kuliko Dar? Hii kwangu ni ajabu sana. Nini maanake?Huku ni Arusha mkuu. Sasa ndo ushangae kuwa hapa Dar bei ni juu kuliko huko Bara na bandari iko hapoa Dar! Wiki 2 zilizopita nilikuwa huko Dar na nikashangazwa na bei ya mafuta kuwa juu kuliko mikoani. Wakati nlipokuwa huko bei ya Dizeli ilikuwa 1600/-wakati Morogoro ilikuwa 1,200/- ! Ndo maana nikasema kuna ufisadi mkubwa katika biashara ya mafuta na hasu huko Dar!
...Hatuna pa kwenda mkuu labda ni pale Wakulu wa nchi wakiamua kutupa afueni na kutuaonea huruma, basi!
Hapo Dar ndo kwenye serikali na ufisadi umejikita hapo hapo, nini manaake? Nadhani kuna watu wame-engineer kamtandandao ka kushibisha matumbo yao kupitia biashara ya mafuta hapo Dar. Akili ya kawaida haiwezi kukubali kabisa kuwa Mafuta huku bara yawe bei ndogo kuliko Dar; kizingizio utachosikia ni kuwa kuna kukwepa kodi na njia za panya lakini si kweli maana mbona mafuta yalipoanda bei duniani huku Arusha bei ilikuwa juu kuliko Dar? Akili mukichwa!Makubwa haya, Arusha iwe bei pungufu kuliko Dar? Hii kwangu ni ajabu sana. Nini maanake?
BP nimekuwa nikiwatumia muda mrefu lakini kuanzia Februari mwaka huu nikajikuta nashindwa kuendelea nao kwani ukiwa na kasumba ya kununua mafuta sehemu moja tu kuna siku ukiwa mbali nao unajihisi kuwa na utumwa wa lazima kuwatafuta wao tu. Biashara hii ina wenyewe!