Bei ya mafuta duniani imeripotiwa kupanda kufuatia tahadhari kali kutoka Iran dhidi ya uwezekano wa uvamizi wa kijeshi wa ardhini kutoka Marekani, licha ya Rais Donald Trump kusema kuwa mazungumzo bado yanaendelea ili kumaliza vita hiyo.
Mafuta aina ya Brent, ambayo ni kipimo cha bei ya mafuta duniani, yalipanda kwa asilimia 2.47 na kufikia dola 107.92 kwa pipa, huku mafuta ghafi ya Marekani yakipanda kwa asilimia 2.94 hadi dola 102.57 kwa pipa.
Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa vikosi vya nchi hiyo “viko tayari” kusubiri wanajeshi wa Marekani, ikiwa uvamizi utafanyika. Kauli hiyo imekuja baada ya Trump kusema kuwa “mazungumzo yanaendelea” na kuongeza muda wa masharti yake ya kuitaka Iran kufungua tena Mlango wa Hormuz.
Katika jitihada za kumaliza mgogoro huo, Mawaziri wa mambo ya nje kutoka Pakistan, Saudi Arabia, Misri na Uturuki wamekutana na kueleza kuwa mazungumzo yao yamekuwa na mafanikio.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, Ishaq Dar, amesema nchi yake itasaidia kuwezesha mazungumzo kati ya Marekani na Iran katika siku zijazo.
Vita ya Marekani na Israel dhidi ya Iran imesababisha usumbufu mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika usambazaji wa mafuta duniani, hasa kutokana na kufungwa kwa Mlango wa Hormuz, ambapo takribani asilimia 20 ya mafuta ya dunia hupita. Mashambulizi dhidi ya miundombinu ya mafuta na gesi pia yamechangia kupanda kwa bei.
Nchini Marekani, wastani wa bei ya petroli umefikia dola 3.98 kwa galoni, hali inayoonyesha athari za moja kwa moja za mgogoro huo kwa Wananchi.
Wataalamu wanaonya kuwa mataifa madogo, hasa ya Asia, yataathirika zaidi, huku ongezeko la bei ya mafuta likiathiri uchumi wa dunia kwa ujumla.
Aidha, wataalamu wanasema kuwa hata baada ya vita kumalizika, bei ya mafuta haitashuka mara moja. Hii itategemea kufunguliwa tena kwa mlango wa Hormuz na ukarabati wa miundombinu iliyoharibiwa, ikiwemo kituo kikubwa cha gesi cha Ras Laffan kilichopo Qatar.