Bei ya mafuta duniani yashuka baada ya sitisho la Vita

Bei ya mafuta duniani yashuka baada ya sitisho la Vita

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
419
Reaction score
553
Bei ya mafuta duniani imepungua kwa kiasi kikubwa kufuatia tangazo la Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa wiki mbili.

1775626124771.png
Mapema Jumanne, pipa moja la mafuta katika soko la kimataifa lilikuwa likiuzwa kwa dola 103.42, huku mafuta ya Marekani yakifikia takribani dola 103.25 kwa pipa. Hata hivyo, bei hizo bado ziko juu ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya mzozo kuanza Februari 28.


1775626185638.png

Mtaalamu wa uchumi wa nishati kutoka Japan, Ichiro Kutani, amesema kushuka kwa ghafla kwa bei kunahusiana moja kwa moja na tangazo hilo. Hata hivyo, ameonya kuwa bei huenda zisishuke hadi kufikia kiwango cha awali cha takribani dola 70 kwa pipa kutokana na uharibifu wa miundombinu katika baadhi ya maeneo ya Mashariki ya Kati.

Wakati huohuo, masoko ya hisa barani Asia yameonesha kuimarika, ambapo Nikkei 225 ya Japan imeongezeka kwa takribani asilimia 4 na ASX 200 ya Australia kwa karibu asilimia 3.

=============== For English Audience ==============​

lobal oil prices have fallen sharply and stock markets have jumped after the US and Iran agreed to a conditional two-week ceasefire deal that includes the reopening of the key Strait of Hormuz waterway.
The price of benchmark Brent crude fell by about 13% to $94.80 (£70.73) a barrel, while US-traded oil was more than 15% lower at $95.75.

But oil prices remain higher than before the conflict started on 28 February. At the time, it was trading at around $70 a barrel. The cost of energy has jumped as oil and gas supplies from the Middle East have been severely disrupted after Iran threatened to attack ships trying to use the strait in retaliation to US and Israeli airstrikes.

Major stock indexes in the Asia-Pacific region rose on Wednesday morning. Japan's Nikkei 225 gained by 5% while South Korea's Kospi jumped by nearly 6%. Hong Kong's Hang Seng was up by 2.8%, while the ASX 200 in Australia gained 2.7%.

US stock market futures also pointed to a higher open for Wall Street. Futures contracts are an agreement to buy an asset for a set price at a later point in time. In the case of US stock stock futures they can indicate the direction of the market before it opens.

In a social media post on Tuesday evening, Trump said: "I agree to suspend the bombing and attack of Iran for a period of two weeks... subject to the Islamic Republic of Iran agreeing to the COMPLETE, IMMEDIATE, and SAFE OPENING of the Strait of Hormuz".

He had set a deadline for 20:00 EDT on Tuesday (00:00 GMT on Wednesday), threatening that "a whole civilisation will die tonight" if no deal was reached.

Iranian Foreign Minister Abbas Araghchi said on social media that Tehran will agree to a ceasefire "if attacks against Iran are halted", adding that safe passage through the Strait of Hormuz "will be possible".​

Chanzo: BBC
 
Nimeona hapa jf wamesema wasafirishaji wasipandishe bei kabla ya kuelekezwa, labda tutarudi kwenye mfumo!

Maisha ni magumu ila yatakuwa magumu zaidi kama tukiendelea hivj..
Tunarudije kwenye mfumo wakati bei za mafuta zipo juu na vitu vmepanda bei? Mambo yatazidi kuwa magumu, na hata bei zikishuka, hazirudi kama mwanzo tena.
 
Uongozi wa juu kushikwa na mwanamke ni laana kuu haijapata kutokea duniani,ni vichekesho vitupu wametangaza kukutana leo kujadili kupandisha nauli na amekaa kimya hajui hata aseme nini.
Kwani huwa anajua anasema nini? Si anasubiri kuandikiwa aseme nini! Naona walikuwa wanasubiri tarehe 8 ngoja tuone!
 
Zitashuka tu mkuu pakitulia kule.
Kirahisi tu! Miaka yote serikali ilituambia nchi ina hifadhi ya mafuta ya kuanzia miezi 3 na kuendelea! Vita ya Marekani na Israel dhidi ya Iran ilianza Februari 28 mwaka huu wa 2026!

Ndani ya Mwezi mmoja tu (ilipofika April) tukapandishiwa bei kwa kiwango cha kutisha! Sababu eti ni vita ya Mashariki ya Kati! Sasa ile hifadhi ya mafuta tuliyo aminishwa miaka nenda ilipotelea wapi?

Na kinachosikitisha kuna baadhi ya maeneo wamiliki wa vituo vya mafuta walisitisha kuuza mafuta kwa bei ya zamani, ili itakapotangazwa bei mpya wauze kwa faida kubwa zaidi!

Hii iko sawa kweli?
 
Back
Top Bottom