Tetesi: Bei ya chakula kwa wasafiri

wisewriter

Senior Member
Mar 26, 2015
106
62
Leo nilienda kumsindikiza jamaa yangu kwenye hotel moja hapa Dodoma njiani kuelekea Singida.Sehemu hiyo jina sijalishika lakini abiria wa mabasi hupata huduma mbali mbali kama chakula,vinywaji na nyingine muhimu.Kilichonishangaza ni soda ya Pepsi 500ml (take away) kuuzwa shs 1,500 wakati bei yake halisi haizidi 1,000 Mimi nadhani hiki si sawa kwa sababu hii si hotel ya nyota tano.Sijui Wanda jf mnalionaje hili lakini haya ni baadhi tu ya mambo mdogo yanayoongeza ugumu wa maisha kwa mwananchi wa kawaida bila sababu.
 
Kwa kweli bei za vinywaji na vyakula kwenye hotel ambazo mabasi ya abiria usimama uwa ni za juu sana. Na abiria uwa hawana njia mbadala zaidi ya kulazimika tu kununua au kujinyima kwani ndiyo hotel pekee ambayo madereva uamua kusimama ili kuruhusu abiria kupata chakula ndani ya dakika chache.
 
Pale yanaposimama mabasi ya Kilimanjaro express maji madogo ya kilimanjaro sh 1000
 
Mimi huwa sinunui ng'o huwa nafungasha bite zangu kutokea home au nifunge kabisa. Mara nyingi tukishushwa hapo naenda kujaza vyoo vyao.
Alafu madereva nao nadhan wanalipwa na wenye hotel hzo kama siyo hotel za matajiri yao.
 
kuna watu wanajifanya wanatetea abiria lakini hili jambo wanafumbia macho bei za vyakula ni kubwa mbaya zaidi madereva kwa sababu wanapewa chochote wanapeleka basi na kuwapa abiria muda mchache wa kula sumatra wafatilie hili ikiwezekana watangaze tenda hotel zishindanishwe
 
Sasa tunauza saa mabasi yanapopita tu. Yakiisha tunafunga hotel kwa hiyo tuna compensate.
 
Sasa tunauza saa mabasi yanapopita tu. Yakiisha tunafunga hotel kwa hiyo tuna compensate.
Kama ndivyo hivyo basi mabasi yasimame na kuruhusu abiria kushuka na kula chakula kwenye hotel ambazo hazitegemei wateja ambao ni abiria tu wa hayo mabasi. Ili kusiwe na kisingizio cha ku compensate. Kwanza hizo hotel yanaposimama hayo mabasi ndizo zinazouza zaidi kupita hotel zisizotegemea abiria kama wateja. Hivyo hilo suala la compensation halina mashiko.
 
Back
Top Bottom