Bei mpya za umeme hizi hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bei mpya za umeme hizi hapa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 29, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Bei mpya za umeme hizi hapa


  na Chalila Kibuda


  [​IMG] SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO) limeainisha gharama mpya kwa watumiaji wa umeme zitakazoanza kutozwa kuanzia mwezi Januari mwakani. Taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari na Ofisi ya Uhusiano wa Tanessco jijini Dar es Salaam jana ilianisha kuwa gharama hizo mpya zimegawanyika katika makundi matatu kulingana na mahitaji ya matumizi ya umeme.
  Makundi hayo ni pamoja na watumiaji wa nishati hiyo kwa matumizi ya majumbani ambapo gharama ya chini kutoka 0-50 kWh/mo utauzwa kwa gharama ya sh 60 badala ya sh 49 ya sasa, tofauti yake ikiwa sh 11.
  Kwa upande wa matumizi ya umeme ya kawaida bei ya matumizi kwa gharama za nishati kwa uniti imepanda kutoka sh 129 hadi kufikia Sh 157 ikiwa imeongezeka kwa sh 28.
  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kadhalika kwa upande wa mahitaji ya juu ya msongo mdogo, gharama za nishati kwa uniti imepanda kutoka sh 85 hadi sh 94 ikiwa imepanda kwa sh 9 zaidi.
  Kadhalika mahitaji ya juu ya msongo mkubwa, gharama za nishati kwa uniti ambao ulikuwa ukiuzwa sh 79 sasa utauzwa sh 84 tofauti ikiwa ni sh tano.
  Kwa upande wa Shirika la Umeme Zanzibar gharama za nishati kwa uniti kwa gharama mpya ya umeme itakuwa ni sh 83 badala ya sh 75 gharama hizo zikiwa zimepanda kwa sh 8.
  Watumiaji ambao wameonekana kuumizwa katika gharama hizi mpya ni wale wa matumizi madogo madogo ya nyumbani na wenye matumizi ya kawaida ambao wamepandishiwa kwa zaidi ya Sh 10.
  Kwa muhibu wa taarifa za TANESCO, hatua hiyo ya ongezeko la gharama imefikiwa baada ya gharama hizo kuidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Umasikini wetu umepanda kwa wastani ya asilimia 18.5%

  Kweli haya ndiyo maisha bora kwa kila Mtanzania ambayo JK na CCM yake walituahidi..................are we really not a cursed nation?
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Yaani pamoja na kuilipa Dowans bado umeme mgao so why paying them at first place??????
   
 4. k

  kituro Senior Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  jamani tusichukie wawekezaji hawa ndiyo wanaoleta ajira!. Dowans ni miongoni mwa wawekezaji!.
   
 5. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Naomba nitukane. Ah acha tu. Ila manina hawa tanesco walitaka 34%! Ninahasira ova mtu katembea na mke wangu! Eti Upungufu wa nishati Tanzania. GOD curse us,I wnt complain!
   
Loading...