Bei juu " Wagosi wa kaya"

Bei juu " Wagosi wa kaya"

NGAYANIMO

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
39
Reaction score
55
MKOLONI FT JITA MAN - BEI JUU.

Mkoloni amewataka wasanii kuimba nyimbo za kuelimisha kama walivyokuwa wanaimba zamani ili kuweza kuiweka jamii sawa na siyo kuimba mambo ambayo ukiyasikia mpaka unashangaa wakati anapokaa huyo msanii akipita ni lazima avue viatu kwa kuwa kuna matope sana.

Vipi mdau wa Ukwaju Wa kitambo vol. 2 je unakumbuka wimbo wa wagosi wa kaya Unaoitwa bei juu " mkoloni ft jita man - bei juu " mkoloni anasema hivi.

*Kila mtu ni shahidi kwenye hii karne ya sasa maisha hayana unafuu labda ujiunge na Siasa/
Haiwekani kabisa eti Mbunge wa Dodoma Bosho yake ije kuwa sawa na Mbunge kutoka
Kigoma/
Wakati pale Dodoma hata kwa Miguu anaingia Bungeni/
Bosho yake ya Usafiri Bora iende mashuleni/
Matumbo yamekomaa kwaajili ya kula Mlo mmoja/
Ninavumilia sana naonyesha vionja /
Watu wanaiba Pesa Baadae tunaambiwa wanazirudisha/.................................
its every kusikitisha..!!
Hivi kuna mtu anaejua kirefu cha "EPA"..??
"EP" Maanake Ni Eleza pesa Alipozificha..!!
Na kama kweli hizo pesa mmeamua kuzirudisha/

Acount ya wagosi hiyo Rudisheni Upesi...*

Fredrick maliki a.k.a mkoloni..

Maana ya neno " EPA" ni Mkataba wa Ubia wa kiuchumi kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Umoja wa Ulaya (EU) unaojulikana kwa kifupi EPA..
Pale mwishoni mkoloni kwenye Outor anasema..
"Mkoloni anasema kirefu cha B.O.T

"Sio BANK OF TANZANIA 🇹🇿"
bali ni
"BONGO ONGEZA TAABU"

Maneneo " B.O.T ni " BANK OF TANZANIA..

Kwanini gharama za maisha zinazidi kupanda nchini Tanzania na kupelekea umaskini kuongezeka? ...

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
Wagosi-wa-Kaya-235_1.jpg
 
Umenikumbusha wimbo wa wauguzi, kero (umeme na maji), traffic. Ni nyimbo za kitambo ila zinaishi kwenye uhalisia mpaka leo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom