Behewa za SGR zimekamilika

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, ametembelea nchini Korea katika kampuni ya SSRST kuona ukamilishaji wa utengenezaji wa behewa
Sisi kama nchi pamoja na kuwa na wasomi wengi ila wasomi wetu wametusaidia nini tuna vyuo vingapi vya ufundi .

serikali tukufu mbona mumetupimisha sana barabara kwenye geography alaf leo hii tenda munawapa wachina

kwahiyo tumeshindwa hata kutengeneza mabehewa ?
 
Hii treni ya mwendokasi na lile ngarangara la dizeli hayana utofauti kama ndiyo behewa zenyewe ninavyoziona!
Umughaka, ebu kamalizie ile story ya noti fake aisee, huku mwachie mpwayungu.
 
mabehewa kwa ndani nayaona yako poa kiasi, changamoto maintenance na namna ya kuwasaidia wasafiri wabebao mizigo, bata, kuku, etc kuwapelekea waishio mjini
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, ametembelea nchini Korea katika kampuni ya SSRST kuona ukamilishaji wa utengenezaji wa behewa.
 
Wakenya watanuna kweli na ule mnganja nganja wao unaotumia mafuta ya dizeli, halafu wakaambiwa eti ni treni ya mwendokasi!

Mchina ni mtu mbaya sana.
 
Wakenya watanuna kweli na ule mnganja nganja wao unaotumia mafuta ya dizeli, halafu wakaambiwa eti ni treni ya mwendokasi!

Mchina ni mtu mbaya sana.
Wakenya wakigundua tunayo ya kisasa zaidi, utaona watakavyohaha kufanya upgrading......kunyaland wanapenda sana mashindano.
 
Mbona hawatuonyeshi beheea Zima linaonekanaje?!
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, ametembelea nchini Korea katika kampuni ya SSRST kuona ukamilishaji wa utengenezaji wa behewa.View attachment 2398341
Mkuu Musa Kadiko , asante kwa taarifa hii

Kwenye mambo ya SGR, Watanzania tunapaswa kuambiwa ukweli wa kila kitu!, serikali yetu lazima iwe very transparent see through kwenye kila kitu including mikataba na financial maters kufuatia kuwahi kupigwa huko nyuma kwenye rada, kwenye ndege, kwenye meli na sasa kwenye reli
Maswali haya yajibiwe kikamilifu
Maswali haya yanahitaji majibu ya kina na sio blah blah!.
Kama mtu kuuliza maswali kama haya, kutapelekea kuhojiwa uzalendo wake, mimi naomba kutumia kinga ya kihabari na kanuni ya kwanza ya mwandishi wa habari no seek the truth, and write nothing but the truth!, kuna kitu ninadhamiria sio tuu kuandika bali kukitengenezea a video documentary ya safari ya SGR ya Tanzania, tulipotoka, tulipo na tunapokwenda, ili huko mbele, likija kujitokeza liji white elephant fulani hivi ambalo sijui kama ni mimi tuu naliona, angalau dhamira yangu isinisute, niliona kabla, nikasema kabla, nikaandaa documentary kabla, nikaonyesha kabla, ili angalau jamii ya Watanzania wajue kuna watu waliona kabla na walisema kabla!.

Na labda kuwasaidia Watanzania wenzangu wasio jua, kwenye ile kashfa ya rada, BAE walikiri kutoa mlungula wa kickbacks, lakini sheria yao inawaruhusu non disclosure ya waliowapa mlungula, ilo usipoteze wateja wapya wapenda mlungula, kibiashara mlungula wa 10% ni halali!, ila ikijulikana kuwa umetoa mlungula, unapaswa ama uwataje uliowapa mlungungula, wakamuliwe wautapike huo mlingula, ama uwahifadhi usiwataje, na badala yake utozwe faini kwa uliowapa mlungula, na kuurejesha ule mlungula, na hicho ndicho kilichofanywa na BAE, kuwahifadhi waliowapa mlungula, na badala yake ikakubali kulipa faini na ndipo tukarejeshewa ile chenji ya rada.

Hii maana yake, kuna viongozi wetu walikula mlungula BAE akawakingia kifua kuwahifadhi kwa kulipia faini na ule mlungula ukarudishwa nchini kama chenji ya rada, endapo BAE wasinge wakingia kifua kuwahifadhi na kuwalinda, amini usiamini, hayo majina ya waliopokea mlungula na kuzihifadhi fedha zao kule Credit Suisse, yangetoka, Watanzania msinge amini macho na masikio yenu!.

Kashfa hii iliobuka kwasababu tuu kulitokea lijinga limoja, mgao wake yeye ukauhifadhi visiwa fulani ambavyo viko chini ya milki ya Uingereza, ndipo Muingereza akabaini, lakini kama wote wange bank Swiss banks, kule fedha zao ni very secure, hata bank manager, hajui majina ya customers na clients ni secret codes tuu zinatembea, hivyo wala kashfa ya rada isinge ibuka!.

Hivyo watu tunaoulizia kuhusu haya mabenewa, naomba mtuelewe ni wazalendo wa kweli wa nchi hii!.

Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…