Before you upgrade think twice

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Ullimwengu tuliopo ni wa sayansi na Teknolojia.Kila kukicha teknolojia mpya ya kufanya mambo, kutengeneza bidhaa inagunduliwa na kuanzishwa.

Uwepo teknolojia na misamiati ukichanganya na ubunifu wa wataalmu wa marketing kwenye makampuni unawaacha watumiaji wakiwa hawana cha kufanya na kujikuta wakihamasika kufuata teknolojia fulani bila kuwa na mwanga ni kitu gani hasa wamenunua.

Nitajikita zaidi kwenye teknolojia za IT
Mfano Microsoft walitoa Desktop OS ya XP. Then wakaja na Vista. Na sasa wako na Window 7.

Katika Matangazo sasa hivi inakuwa promoted Windows 7. Je mtumiaji ana haja ya kuharakisha kwenda kwenye Window 7? Je Mtumiaji alikuwa ana haja ya kubadilisha kutoka XP kwenda Vista bila kujiridhisha.

Binafsi Nashauri watumiaji wanataka kufanya upgrade ya OS wazingatie haya.

Usifanye upgrade ya kutoka OS kwenda nyingine kabla OS mpya haijamaliza japo hata mwaka Mmoja toka izinduliwe

Binafsi natumia Windows XP hadi sasa hivi . Nakumbuka Vista iliipoingia watu walikimbia kuupgrade. lakini baada ya mwaka hata Microsoft wenyewe walisema Vista ni kituko. Kwa mfano huu unaweza kuona kuwa the more u upgrade earlier the more unakuwa umeajiriwa na kama tester bila kujua. Kwa hiyo ni muhimu kutoa muda japo wa mwaka kujiridhisha kuwa OS fulani imekuwa stable. Huu ushauri ni kwa wale wanataka kukimbilia kuupgrade kwenye Window 7.

Usifuate Mkumbo wala kusikiliza watu wa Masoko. Kuna neno Linaitwa Technology fever. watu wengi tunapenda kuonekana tuko latest na tunakwenda na wakati. Ni bora ujue kwa nini unatumia Kompyuta yenye window 7 na sio XP au Vista. Style hii ya tecnology fever kwa mtazamo wangu Iphone wanaitumia kuwakamata watu japo iphone ina mapungufu mengi. Mfano kwangu one key feature ya simu ni camera. iphone is weak kwenye hii> je watu wangapi wanatumia hizo application za iphone.

kingine kwenye hii techonology fever watumiaji wengi inabidi wakumbukekwa jinsi Window Vista ilivyokuwa na matatizo hawatakiwi kuwa wepesi wa kuapgrade. Unless kompyuta inakuja iko preinstalled.

Kwa hiyo tuwe tunajiuliza maswali haya na mfano wa majibu nimeyaweka kwenye mababo.

kwa nini nihame kutoka teknolojia hii kwenda ile?( Imepitwa na wakati, haiwi supported na wasambazaji? imenivutia kwa muonekako, its talk of the town)
Kwa nini ninunue Iphone na si Nokia, samsung au motorolla.( Recommedation, Matangazo unayoona yamekuvutia, Mazoea, Specification ilizonazo ndio hasa unataka na unazitumia na haziko kwingine)

kwa hiyo kwenye maamuzi ya kununua vifaa vya tekonoljia tusikubali watu wa masoko watuchagulie bidhaaa kwa kutuyajia streghts za bidhaa hiyo waulize pia weakness ya hiyo bidhaa.

Nawasilisha kwa mjadala.
 
I actually prefer Ubuntu, it is more efficient and the price can't be beat, it is free.

Hata nikinunua computer yenye Microsoft Windows tayari, na partition na kuweka Ubuntu, nitaweza vyote utakavyofanya kwenye MS Windows na zaidi.Ukija na Microsoft Office nitakuja na OpenOffice itakayoweza kufanya yote ya MS Office na mengine MS Office isiyoweza kufanya, kwa bure.

Windows 7 ni nyanya kichizi, at least according to my exprerience.
 
Kiranga,

Unajua mara kibao nilipania kudownload UBuntu, halafu katikati nikifuata instructions inanizingua naamua kughairi. Link gani ambayo haina shobo niende ku-download bila chenga.?
 
Kiranga,

Unajua mara kibao nilipania kudownload UBuntu, halafu katikati nikifuata instructions inanizingua naamua kughairi. Link gani ambayo haina shobo niende ku-download bila chenga.?

Ubuntu downloads zao ziko hapa

Download | Ubuntu utapata 32 bit desktop

Netbook edition iko Download | Ubuntu

Download *.iso file, burn to CD, from there the installation is a breeze, ukipata issue wana bonge la user community ambayo ina documentation zote za kukusaidia.
 
Point ndo ipi hapo kwamba tusiwe tester? kwamba upgrading holds nothing in it?

Point ni kwamba, unaweza kufanywa zumbukuku ulimwengu uko huku, ukawafanyia Microsoft kazi ya kutest software, halafu hapo hapo ukawalipa.

Au hata usipowalipa, wanakutumia kupata faida and still wanasambaza OS mbovu kama Windows 7.
 
Ubuntu downloads zao ziko hapa

Download | Ubuntu utapata 32 bit desktop

Netbook edition iko Download | Ubuntu

Download *.iso file, burn to CD, from there the installation is a breeze, ukipata issue wana bonge la user community ambayo ina documentation zote za kukusaidia.

Hiyo Ubuntu nimeweka kwene flash bado inazingua tu, haitaki ku-install..Ngoja niachane nayo vya bure aghali.
 
Hiyo Ubuntu nimeweka kwene flash bado inazingua tu, haitaki ku-install..Ngoja niachane nayo vya bure aghali.

In this case ughali wake unakuja in the form ya kufuata instructions na ku dot the i's na ku cross the t's.

Hey, come to think of it, si kila machine inaweza ku boot from flash, na hata zinazoweza ku boot from flash kama BIOS haiko set up ku boot kwenye flash kwanza kabla ya hard drive, unaweza kukuta booting yako inatoka kwenye hard drive instead of the flash drive.You need to check your BIOS.

Mimi nishainstall Ubuntu kutoka flash na CD. Kama flash inakuzingua, changing BIOS settings and boot order sounds like ancient Greek, na una blank CD na CD writer unaweza kutumia ImgBurn au software yoyote inayoweza ku burn iso image kwenye CD. From there unaweza ku install kutoka CD.

Lakini itakuzingua tu.
 
upo sahihi mkuu kukimbilia sana kuupgrade kuna hasara zake sometime mm nipo comfortable na xp kulingana na kazi zangu za kila siku nilikimbiliaga vista nikatoa siku hiyo hiyo kwani aikuwa compatible na drivers za vitu ninavyotumia
 
Ullimwengu tuliopo ni wa sayansi na Teknolojia.Kila kukicha teknolojia mpya ya kufanya mambo, kutengeneza bidhaa inagunduliwa na kuanzishwa.

Uwepo teknolojia na misamiati ukichanganya na ubunifu wa wataalmu wa marketing kwenye makampuni unawaacha watumiaji wakiwa hawana cha kufanya na kujikuta wakihamasika kufuata teknolojia fulani bila kuwa na mwanga ni kitu gani hasa wamenunua.

Nitajikita zaidi kwenye teknolojia za IT
Mfano Microsoft walitoa Desktop OS ya XP. Then wakaja na Vista. Na sasa wako na Window 7.

Katika Matangaoz sasa hivi inakuwa promoted Windows 7. Je mtumiaji ana haja ya kuharakisha kwenda kwenye Window 7? Je Mtumiaji alikuwa ana haja ya kubadilisha kutoka XP kwenda Vista bila kujiridhisha.

Binafsi Nashauri watumiaji wanataka kufanya upgrade ya OS wazingatie haya.

Usifanye upgrade ya kutoka OS kwenda nyingine kabla OS mpya haijamaliza japo hata mwaka Mmoja toka izinduliwe

Binafsi natumia Windows XP hadi sasa hivi . Nakumbuka Vista iliipoingia watu walikimbia kuupgrade. lakini baada ya mwaka hata Microsoft wenyewe walisema Vista ni kituko. Kwa mfano huu unaweza kuona kuwa the more u upgrade ealrie the more unakuwa umeajiriwa na kama tester bila kujua. Kwa hiyo ni muhimu kutoa muda japo wa mwaka kujiridhisha kuwa OS fulani imekuwa stable. Huu ushauri ni kwa wale wanataka kukimbilia kuupgrade kwenye Window 7.

Usifuate Mkumbo wala kusikiliza watu wa Masoko. Kuna neno Linaitwa Technology fever. watu wengi tunapenda kuonekana tuko latest na tunakwenda na wakati. Ni bora ujue kwa nini unatumia Kompyuta yenye window 7 na sio XP au Vista. Style hii ya tecnology fever kwa mtazamo wangu Iphone wanaitumia kuwakamata watu japo iphone ina mapungufu mengi. Mfano kwangu one key feature ya simu ni camera. iphone is weak kwenye hii> je watu wangapi wanatumia hizo application za iphone.

kingine kwenye hii techonology fever watumiaji wengi inabidi wakumbukekwa jinsi Window Vista ilivyokuwa na matatizo hawatakiwi kuwa wepesi wa kuapgrade. Unless kompyuta inakuja iko preinstalled.

Kwa hiyo tuwe tunajiuliza maswali haya na mfano wa majibu nimeyaweka kwenye mababo.

kwa nini nihame kutoka teknolojia hii kwenda ile?( Imepitwa na wakati, haiwi supported na wasambazaji? imenivutia kwa muonekako, its talk of the town)
Kwa nini ninunue Iphone na si Nokia, samsung au motorolla.( Recommedation, Matangazo unayoona yamekuvutia, Mazoea, Specification ilizonazo ndio hasa unataka na unazitumia na haziko kwingine)

kwa hiyo kwenye maamuzi ya kununua vifaa vya tekonoljia tusikubali watu wa masoko watuchagulie bidhaaa kwa kutuyajia streghts za bidhaa hiyo waulize pia weakness ya hiyo bidhaa.

Nawasilisha kwa mjadala.

Acha mambo yako wewe. Sasa unataka nani awe tester ya wa technologia mpya inayoingia sasa hivi sokoni? Ni wewe na mimi. Kuna mtu amekuuliza; mbona hutumii MS-DOS mpaka sasa?
Watu wengi wanaotumia office 2003 wanapata shida sana wanaletewa docs zimefanyiwa kazi office 2007. Kuna haja gani ya kukomalia old technology wakati mpya ipo sokoni?!

Kila kizuri na kipya kina ubata na uzuri wake. Hata hivyo ulivyokalia mpaka sasa once upon a time vilikuwa vipya na bado vipo sokoni. Na vitakuwa phased out pia!
 
Mtazamani Umeanza vyema sana hoja yako lakini Conclusion imekuwa very poor kiasi kwamba sijategemea u had all the time to write and finish like that..Maswali uliyosema tujiulize na ukatoka majibu kwenye mabano....majibu hayo very constructive kihivyo...this mean unaweza kuwa sio experiance user wa Operationg system.

Umeangalia window 7 vyema ndugu?Kitu kidogo tafuta mtu mwenye window seven kaangalia calculator yake na fuction zake.Nenda kwenye stick note...ambayo kwenye window XP ingebidi ununue snagit...wao hiyo future wameweka within window.DVD player....XP na Vista U had to buy lucky ije na power dvd kwa ajiri ya wewe kucheza dvd tofuati...wao wamekuja nayo.Tuje kwenye upgrade ya RAM..Je wajua kuwa unawez akutumia flash yako ya 2GB.Na kuiconvert kuongeza nguvu ya ram yako kama ulinunua ikiwa na 1GB RAM na una flash ya 2GB ukaifanya kuwa na 3GB RAM?Umeona feature ya kuweka quick program zako kwenye task bar hapa chini rather that kwenda kuzitafuta uko kwenye all program?

Sijatumia sana vista kwa ajiri ya mambo yake mengi mengi ambayo hayana tija na errors kibao ndio maana window 7 ime solve almost 80% ya matatizo ya vista..
 
Kama unapenda vya zamani mbona hutumii MS-DOS!

bahati mbaya mimi siyo mwandishi ila sijasema napenda vya zamani ni ushauri tu kuwa before u migrate or upgrade inabidi ujiulize na kujirizisha

I actually prefer Ubuntu, it is more efficient and the price can't be beat, it is free.

Hata nikinunua computer yenye Microsoft Windows tayari, na partition na kuweka Ubuntu, nitaweza vyote utakavyofanya kwenye MS Windows na zaidi.Ukija na Microsoft Office nitakuja na OpenOffice itakayoweza kufanya yote ya MS Office na mengine MS Office isiyoweza kufanya, kwa bure.

Windows 7 ni nyanya kichizi, at least according to my exprerience.

Mkuu lakini kwa mawazo yangu ni kuwa ubuntu sasa hivi nadhani iko kwenye version 10.01. sasa je ni vizuri kuupgarde haraka au kama version yako ya 9.000 inafanya kazi unatulia nayo wakti unacheki upepo kwanza?

Point ndo ipi hapo kwamba tusiwe tester? kwamba upgrading holds nothing in it?

Point ndugu yangu ni kuwa usifanye upgrade au usi migrate bila kujua kwa nini unafanya hivyo. Ni features gani umemiss katika version uliyopo unakwenda kule. je ni features gani utamiss unakohamia kwenye current version unazo. Any way this is an open debate.

Acha mambo yako wewe. Sasa unataka nani awe tester ya wa technologia mpya inayoingia sasa hivi sokoni? Ni wewe na mimi. Kuna mtu amekuuliza; mbona hutumii MS-DOS mpaka sasa?
Watu wengi wanaotumia office 2003 wanapata shida sana wanaletewa docs zimefanyiwa kazi office 2007. Kuna haja gani ya kukomalia old technology wakati mpya ipo sokoni?!

Kila kizuri na kipya kina ubata na uzuri wake. Hata hivyo ulivyokalia mpaka sasa once upon a time vilikuwa vipya na bado vipo sokoni. Na vitakuwa phased out pia!

Duh mkuu hakuna aliyeniuliza nimefikiria kuandika sijasema kuwa watu wasi upgrade au kumigrate from one version to aother from one teknology to another. Nimesema we should think twice. siyo tu kwa kuwa imekuw aintoduce iwe changed.

Kuhusu kutumia kufungua Doc za Ms 2007 kwa 2003 inawezekana ndio maana nasema application sofware za windows zinaruhusu backward compatibility. Unaweza kufungua doc ya 2007 kwenye application ya 2003 na unaweza kufungua doc ya 2003 kwenye 2007. it depend on your comptency na knowlege.

But all ni all ni HOJA yangu ni kuwa watu wasiwe wepesi kupgrade au kumigrate bila kujiridihisha.
 
Mtazamani Umeanza vyema sana hoja yako lakini Conclusion imekuwa very poor kiasi kwamba sijategemea u had all the time to write and finish like that..Maswali uliyosema tujiulize na ukatoka majibu kwenye mabano....majibu hayo very constructive kihivyo...this mean unaweza kuwa sio experiance user wa Operationg system.

Umeangalia window 7 vyema ndugu?Kitu kidogo tafuta mtu mwenye window seven kaangalia calculator yake na fuction zake.Nenda kwenye stick note...ambayo kwenye window XP ingebidi ununue snagit...wao hiyo future wameweka within window.DVD player....XP na Vista U had to buy lucky ije na power dvd kwa ajiri ya wewe kucheza dvd tofuati...wao wamekuja nayo.Tuje kwenye upgrade ya RAM..Je wajua kuwa unawez akutumia flash yako ya 2GB.Na kuiconvert kuongeza nguvu ya ram yako kama ulinunua ikiwa na 1GB RAM na una flash ya 2GB ukaifanya kuwa na 3GB RAM?Umeona feature ya kuweka quick program zako kwenye task bar hapa chini rather that kwenda kuzitafuta uko kwenye all program?

Sijatumia sana vista kwa ajiri ya mambo yake mengi mengi ambayo hayana tija na errors kibao ndio maana window 7 ime solve almost 80% ya matatizo ya vista..

Buswelu Windows7 sijaingalia lakini nitaaanza kuivalute binafsi soon kwa sas anasoma reviw nyingi za watu online kwenye technical forum ila nashukuru kwa kunihabarisha kwenye hizi faida chache za win7

Lakini downside moja nayojua ya Window7 ni kama unapirated versiion Microsoft can corrupt you OS easily kwa kutuma vitu vinaitwa Security update. Kuna forum niliona user wenye pirated version wanatahadharishwa wasifanye update fulani kwa kuwa ilikuwa ni update ya kucheki validity ya OS.

Kwenye XP na Vista This was not an issue Microsoft hawana policy ya kublock upadtes kwa pirated version kwa OS hizi.

Windos 7 pia ni Very memory hungry OS sasa kwa mtumiaji ambaye PC yake ilikuwa originally desinged for XP akiweka Window 7 au VIsta anaweza asi enjoy the said advatages

But Najua somewhere before the end of this year nitaanza kutumia window 7. Sababu najua kwa Toshiba Niliyonayo na specs zake kuweka Windows7 itakuwa naidhulumu. Ni sawa na kumbebesha mtoto wa mdogo ndoo ya maji kichwani. Mwisho wa siku naweza kuona windows 7 haifai kumbe nilifanya upgrade before thinking twice

Kuhusu nilivyoandika unajua tena sometime hatuna taaluma ya uandishi wa habari kwa hiyo story inaweza kukosa mpangilio mzuri lakini nadhani hoja umeisoma.
 
Kiranga,

Unajua mara kibao nilipania kudownload UBuntu, halafu katikati nikifuata instructions inanizingua naamua kughairi. Link gani ambayo haina shobo niende ku-download bila chenga.?

kwa nini usidownad kutoka kwenye official lin ya ubuntu tena wana instructi nzuri kabisa

ulingana na mashine yako kama ni 32 bit au 64 bit na step by step guidlines
Download | Ubuntu
 
Windows Seven this, Windows Seven that, watu wanakutangazia mi fancy feature kibao na vi cosmetic ambavyo hata hutumii.

Kitu muhimu kama responsiveness hawakwambii, kwa uzoefu nilioupata kutoka kwa Windows Seven, it is a worse resource hog than either XP or Vista.

And no matter how fancy an OS is, if it can't respond timely and it hogs resources, it is not that fancy.
 
Huo ni mtazmamo wa kwako! So far I enjoy dirisha la 7! Siwezi kuwa shabishi simply because ni os mpya au ni version mpya! By the way umeshajaribu Office 2010! Simply Magic!!!!!!!!!!!!!
 
Huo ni mtazmamo wa kwako! So far I enjoy dirisha la 7! Siwezi kuwa shabishi simply because ni os mpya au ni version mpya! By the way umeshajaribu Office 2010! Simply Magic!!!!!!!!!!!!!

As I said, that was my experience. OS moja inaweza kufanya kazi namna tofauti depending on hardware, RAM na hata internet connection speed. My thing is my hardware is certified for Windows 7 and actually the machine came with it, but you would think it was some bootleg install.

I don't use Microsoft Office anymore, it is vendor specific and does not provide the interoperability needed by a power user.I'm into OpenOffice where I can create files that can be opened by my friends in the MS Windows world as well as the Linux/ UNIX geeks.

See the thing that everybody needs to understand is, different users have different needs, and in your case for example, you may not need the interoperability because all your friends and family are using windows.Your IT skills may not be adequate to use Linux and far from being an enhancement, Linux will actually daunt you and prove counterproductive.

Kwa hiyo hii habari ya "this is best" au "that is best" is largely subjective and must be followed by "best for what?"

Ms Windows is best for ease of use and most people are familiar with it, but horrible when it comes to security.

Something like Ubuntu is robust and secure, but the user interface takes some learning, and you may end up going into the terminal to do quite a few sudo apt-get by command line, although it is now streamlined to dumb down the installation and interface to the extent that the installation is better than windows and the interface is almost as easy.

Despite the specification detailed above, you cannot argue that you will have security concerns with Ubuntu as you have with that Swiss cheese like holed Windows.
 
Huo ni mtazmamo wa kwako! So far I enjoy dirisha la 7! Siwezi kuwa shabishi simply because ni os mpya au ni version mpya! By the way umeshajaribu Office 2010! Simply Magic!!!!!!!!!!!!!

what are the magic of Ofiice 2010 for limited comparison with Office 2007 or 2003. Kama alivyosema Kiranga unaweza kuwa na features fulani ambazo hata hazitumiki sana. Kwangu kama mtu anafanya kazi vizuri na Offfice 2003 kwa nini asiendelee nayo> mtu anahamia kwenye 2007 thena anakutana na interface tofauti. ule muda wa ku cope na new layout ya interface unampunguzia utendaji.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom