plan z
JF-Expert Member
- Jun 10, 2019
- 1,395
- 1,443
ILIPOISHIA.
Beat Box alifanikiwa kuingia mjini na kuduwaa kwa ufahari wa mjini pamoja na mademu wakali aliowaona huko mjini. Beat Box baada ya kugundua kumbe kuwa msanii ni dili kubwa sana mjini, alipanga kuwa msanii na yeye.
SASA ENDELEA:
Beat Box aliondoka baada ya tamasha lile kumalizika na kuelekea stand eneo alilokuwa akijilaza kwani bado alikuwa hajapata makazi baada ya kutoka kijijini vilevile hakuwa na ndugu wa kufikia. Beat Box alijiwazia mambo kadha wa kadha pamoja na jinsi ambavyo atafanikiwa kuwa msanii ili mpango wake wa kula totoz utimie, kisha baada ya mawazo ya kina usingizi ulimpitia.
Siku inayofuata Beat Box alianza kuzunguka huku na kule akitafuta chochote ilimradi mkono uende kinywani akawaona wapiga debe wa mabasi ya mikoani jinsi walivyopata chochote kupitia kazi hiyo hivyo ilikuwa ni fursa kwake kuanza kujihusisha na kazi hiyo.
Baada ya mahangaiko ya siku kadha wa kadha Beat Box aliweza kubahatika kupata kazi kwa mtu aliyemsaidia kumpakia mizigo kwenye gari yake na baada ya mahojiano mtu yule aliamua kumwajiri katika kampuni yake kuipokea na kupakia mizigo iliyokuwa inanunuliwa na kuuzwa katika kampuni hiyo. Beat Box alifurahi sana na kumshukuru bosi wake huyo kwa dhati na kuanza kazi huku akijituma huku akiamini kazi hiyo ndiyo itamweka mjini aishi vizuri.
Siku zilizidi kusonga huku Beat Box akiendelea na kazi ile hatimaye kuzoeana na wafanyakazi wenzake na kutokana na tabia yake ya kupenda mademu, wafanya kazi wa kike walimwona sio mtu mwenye future kwani kwa kipindi hicho kifupi alikuwa ameshawatongoza karibu wote hivyo walijitenga naye kiaina jambo ambalo lilimweka Beat Box katika wakati mgumu na kushindwa kuelewa kwanini wanamtenga, aliamua kupotezea na kuendelea na kazi.
Baada ya siku kadhaa walipata wafanyakazi wengine wageni waliojumuika nao na Beat Box alifanikiwa kuopoa mwanadada kati ya hao aitwaye Esther. Beat box alikuwa amepanga chumba hivyo alimpeleka Esther kwake na baada ya kula na story za hapa na pale Beat Box alifanikiwa kugongea mzigo na kwa vile alikuwa na afya kwa vyakula alivyokula kijijini, mbio za kupanda mlima zilianza na hatimaye wakafika juu kabisa ya kilele cha mlima huo. Esther hakuamini na alizidi kumpenda Beat Box mpaka kuwafanya wafanyakazi wawe na wivu hata wale ambao walijitenga wakaanza kujileta ilimradi wamwaribie mwenzao. Wanawake bana!
Kwa vile Beat Box alikuwa na tamaa aliwachangamkia lakini safari hii alipunguza kwa sababu ya Esther. Bosi aliwaita wafanyakazi wote na kuwapongeza kwa umahiri wao na akamfanya Beat Box kuwa msimamizi wa mizigo yote iliyoko store inayotoka na inayoingia. Beat Box alifrahi sana na siku hiyo aliamue akale bata na mtoto Esther ili kujipongeza, wivu ukazidi kuwaingia na wakaanza kumchukia Esther. Siku inayofuata Beat Box aliingia kazini kama kawaida na kuendelea na majukumu. " Habari yako Beat Box?", ilikuwa ni sauti ya kike iliyomwita huku akimgusa begani.
"nzuri, aah Linda, ni wewe?"
"yah, vp kwani nimekuwaje mpaka unaniuliza kama ni mimi"
"hamna, ni kushangaa tu kwa sababu unakuwaga bize sana na mambo yako"
"hahah, acha zako bwana, ubize gani sasa mimi mbona nipo kawaida tu"
"oh sawa karibu"
" nshakaribia, hivi nikuulize, umempendea nini Esther mtu mwenyewe shape hana, sura hana, hebu niangalie mimi nilivyo", alimwambia huku akigeuka geuka ili Beat Box amwone vizuri. Hapo Beat Box alikuwa amejawa na mate mdomoni hadi udenda ulikaribia kumtoka. "aah mbona me kwangu namwona mzuri tu"
"hamna bana achana naye huyo chukua vyombo hivi"
"na yeye akijua je?"
"hawezi kujua tutafanya siri, halafu leo nataka twende wote kwako badae tukitoka kazini"
"aya poa".
Waliagana na kisha kuendelea na kazi. Ilipofika mchana Esther akampitia Beat Box wakaenda kula huku wakipiga story za hapa na pale huku wakipanga mipango yao mbalimbali. Linda aliwaona kwa mbali alisonya kisha akaendelea na mambo yake. Jioni ilifika Esther akaenda nyumbani kwao na Beat Box na Linda walielekea magetoni kwa Beat Box. Wakiwa katika story za pale Linda alipika na wakaanza kuchezeana wakishikana sehemu mbali mbali hatimaye kumaliza mchezo.
Kesho yake tena walipanga kwenda tena kwani show ya jana iliwanogea. Jioni ilifika kisha wakaenda. Wakiwa katika harakati za maandalizi, mara mlango ukagongwa. Beat Box akamwacha Linda kitandani na kwenda kuufungua mlango. Uso kwa uso waligongana macho na Esther.
Je nini kitaendelea? Je atamruhusu Esther kuingia ndani?
Usikose toleo lijalo.