Be smart all the time, Siasa za Nchi hii ni ujinga

ZE WANNA

New Member
Apr 9, 2023
3
6
Wadau habari za easter,

Leo naandika kiufupi kabisa kuna siku nitaleta mzigo mzima humu.

Naomba niongee na vijana umri wa miaka 18-30, kundi hili halijachelewa kuamua ni wakati mzuri wa kuwa na tahadhari na lazima mjue siasa za Nchi hii ni gamble mfano wewe kijana uliyehitimu procurement pale UDOM leo hii bado unatabika kutafuta ajira na ufaulu wako mzuri lakini uliza kuhusu watoto wa dada yake Kasimu Majaliwa wapo wapi? uliza kuhusu ndugu wa karibu wa Samia Suluhu wapo wapi? (sina maana mbaya nimetolea mifano na ieleweke hivyo).

Baada ya utangulizi huo ngoja nijielekeze kwenye mada
Wote wakubwa na wadogo tunajua ripoti ya CAG imetoka na kuna upotevu wa zaidi 800B hizi ni kodi zinazotokana na makusanyo mbalimbali ikiwemo mikopo na tozo za miamala ya simu. Kiukweli moja ya jambo linaloumiza ni kuwa na sauti ya chini kwenye hili mwenye mamlaka anaongea as if we lost a piece of khanga kumbe ni jasho na damu ndio hizo pesa zipatikane hivyo kuna mashaka makubwa kwenye presidency.

Kila sehemu ni pesa zimeliwa kesho unaambiwa kuwa mzalendo na nchi yako lipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yako na watu wake. Nawaza kwa sauti ya chini maendeleo hayo ni yapi vitu vingi vilitakiwa kufanyika miaka mingi tumechelewa bado tunaendelea tena kuiba fedha za miradi kweli haya ndio maendeleo na Rais anaongea kama hana regulatory machinery mbona kuwatoa watu magereza anaweza kwa nini hili analalamika kama mimi Mzee wa Sanya Juu.

Leo Rais anataka Makatibu wakuu wa wizara wapitie ripoti ili wale waliofanya ubadhirifu sheria ifuatwe hivi chief accountant wa wizara sio huyo katiba mkuu na ana wajibu wa kupata maelekezo toshelezi ya mradi unaohitaji pesa na waziri ndio msimamizi wa sera na utekelezaji wa wizara anawajibu wa kufuatilia matumizi ya pesa kulingana na mahitaji ya miradi. Kama kuna shida hivi kujua mpigaji wa pesa hawa wasimamizi wa kuanzia wizara hadi kijiji wanajulikana kwa nini uzito wa kuchukuwa hatua kitete kianze.

Mwisho kwa leo iwapo bandiko hili litaendelea siku zijazo
Rais anabidi achukue hatua za kiwajibikaji na serikali yake yote na haya yote ni sababu ya kuingiza vijana wa deep state na watoto wa viongozi wa kitaifa kwenye siasa (kupewa vyeo vya kubebwa) hivyo kushindwa kuwapiga chini na kufikishwa mahakamani ili taratibu za kisheria zifuatwe ikiwemo pesa kurudishwa.

Nilitumia neno vijana kwa maana ni wakati wa kutumia akili kuliko kuwa na matarajio ya serikali kuleta maisha ya ndoto zenu ikiwemo mazingira rafiki ya kazi, mitaji na maeneo ya biashara.

Tumieni akili zenu vizuri kubuni namna ya kuishi ili kufikia ndoto zenu achana na siasa usikubali kudanganywa usipoteze muda kwenda kwenye makongamano ya kisiasa. Sisi wazee tumechelewa kutoa na kuwa msaada wa kimamuzi juu ya Taifa letu tumetengeneza Taifa la machawa ni mwendo wa kusifia.

Kila kiongozi anapambana kutimiza ndoto zake kataa ujinga wa kutimiza ndoto za watu wengine Tanzania ya leo ni Uingereza ya karne ya 12 miaka ya giza kwa sasa hata ukisema unafanya mapinduzi bado maisha yatakuwa yaleyale waingie Upinzani bado mambo ni yale yale kuletwe katiba bora sana bado hakuna jambo “MAARIFA KWA WATU WETU NDIO UKOMBOZI WA KWELI” tutumie muda mwingi kutafuta maarifa kwa ustawi wa Taifa letu ili angalau twende kwenye age of enlightenment ya Waingereza ya karne ya 16 AD baada ya hapo tuengelee mageuzi inaweza ikawa miaka 5 au 50 ijayo itategemea hali ya watu wetu.

Byee Byee
 
Baada ya utangulizi huo ngoja nijielekeze kwenye mada.

Amen.
 
Back
Top Bottom