eliasy
JF-Expert Member
- Nov 9, 2012
- 455
- 54
Blackberry kwa sasa haifanyi vizuri katika soko la smart phones japo wametoa simu kadhaa mpya, lakini bado Blackberry inasikika kutokana na huduma yake ya Blackberry Messenger (BBM). Jana kampuni ya RIM imetangaza kuwa inaleta huduma ya BBM kwa watumiaji wengi zaidi mwisho wa juma hili, kampuni itazindua application kwa ajili ya Android na iOS.
Katika blog yao, wamesema kuwa itakayoanza itakuwa ni app Android ambayo itapatikana kwenye Google Play Store kuanzia septemba 21. Jumapili Septemba 22, toleo la iOS litapatikana kwenye app store.
App hizi zitawawezesha watumiaji kuchat kwenye Mtandao wa BBM na watumiaji wengine mamilioni ambao tayari wamekuwa wakitumia kupitia simu zao za blackberry.
Pia blackberry wameahidi kuwa katika matoleo yajayo, wataongeza huduma za voice na video chat.
reblogged by C6 from: http://tanganyikan.co.tz/blackberry-messenger-app-kwa-ajili-ya-ios-na-android-inatoka-wikendi-hii/
source 2; http://blogs.blackberry.com/2013/09/bbm-for-android-iphone/?CPID=SOC_C_ZA_FB1379596207