BBC yazindua blog juu ya mauaji ya Albino

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Uchunguzi umeanika uovu ambao umekita mizizi.

Hii imekuwa wiki yenye shughuli muhimu katika harakati za serikali ya Tanzania kupambana na vitendo vya mauaji ya Albino katika maeneo ya kanda ya Ziwa Victoria.

Uovu huo umejikita katika mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga na Kagera.

Maeneo hayo ya historia ya kisirani cha kuwaua vikongwe katika miaka ya 1970, hasa kutokana na macho yao mekundu.

Mauaji hayo ya Albino, vikongwe na wanaume wenye upara yalichochewa na imani za kishirikina.

Uhalifu huu umekuwa ukiendelea kana kwamba serikali haina uwezo au mbinu mwafaka za kuuangamiza.

Mapema mwaka uliopita, Mwandishi wa BBC, Vicky Ntetema alianza kudadisi kiini cha mauaji ya Albino katika maeneo hayo ya Ziwa Victoria.

Albino wanaishi kwa hofu

Ilikuwa safari ndefu, nyeti, yenye utelezi na hatari huku ikihitaji subira na ujasiri.

Siku baada ya siku, Vicky alikutana na wahusika mbalimbali katika biashara hiyo ya kiza.

Ukitaka kujua ni nani anawaua Albino, kwa nini wanauawa basi soma Blog ya Vicky. Una uhuru wa kuchangia mada.

Soma Blog ya Vicky Ntetema

Source BBC
 
Mkuu;

mbona nimeshindwa kubofya na kuingia kwenye blog? any link or something? or do i have to go to BBC

Any link?
 
BBC wameshatusaidia kilichobaki ni vyombo vya usalama kutumia mbinu ya Vicky Ntetema kuwapata hao wagnga na wanunuaji wa mifupa ya Albino ili kupunguza hii zahama la sio Serikali yaCCM ifungashe virago 2010
 
Back
Top Bottom