BBC: Ugonjwa wa Ebola waripotiwa DR Congo

BBC: Ugonjwa wa Ebola waripotiwa DR Congo

Troll JF

Platinum Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
10,438
Reaction score
15,239
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kwamba kumetokea mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Shirika la habari la AFP limesema WHO imechukua hatua hiyo baada ya virusi vya ugonjwa huo kusababisha vifo vya watu watatu eneo hilo tangu Aprili 22.

WHO imesema mlipuko huo unaathiri maeneo ya msituni katika mkoa wa Bas-Uele karibu na mpaka wan chi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mwaka 2014, mkurupuko wa ugonjwa huo Congo ulidhibitiwa kwa haraka ingawa watu 49 walifariki.
 
Idara ya afya kinga..mipakani..nadhani washaiona hii kazi kwako..tushirikiane nao ili huu ugonjwa usituangamize..
 
Na Dr Mwele ndie Mkurugenzi wa WHO anaeratibu kila kitu kwenye masuala ya magonjwa ya milipuko Kusini mwa Afrika.
 
Ukiibuka Tz na kulivyo na msongamano wa watu watakatika kama kuku mwenye mdondo
 
Daaah huo nizaidi ya AIDS aiseeh ....unakufa apo apo ....tuzidi kuomba wakuu
 
Back
Top Bottom