BBC Swahili: chanjo ya Ebola huenda isipatikane

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,458
3,209
Wanasayansi wanaoendelea na uchunguzi chanjo juu ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ebola wameoambia BBC kuwa, chanjo inayoweza kutumiwa kuzuia maambukizi ya virusi hivyo huenda isifumbuliwe.
Wiki chache zilizopitaidara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, ilisitosha ufadhili wake kwa kampuni mbili zilizokuwa zikiendesha utafiti huo. Kwa habari zaidi, ====================================


140801214335_sp_ebola_624x351_bbc.jpg

Mgonjwa wa ebola abebwa

Mkurugenzi wa shirika la afya duniani Margeret Chan amesema kuwa kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa Afrika kunaweza kusababisha janga baya iwapo hautazuiwa.

Akizungumza mjini Conakry baada ya kukutana na marais wa Guinea,Liberia na Sierra Leone,amesema kuwa ugonjwa huo unasambaa kwa kasi ikilinganishwa na juhudi za kuudhibiti,lakini akaongezea kuwa unaweza kusitishwa kutokana na usaidizi wa kimataifa.

Marekani imesema kuwa raia wawili wa taifa hilo wa kutoa msaada wanaougua ugonjwa wa ebola watasafirishwa hadi nchini Marekani mapema wiki ijayo ili kupewa matibabu katika eneo lililotengwa.

Kisa hicho cha ugonjwa huo kitakuwa cha kwanza kutibiwa marekani.

Afisa mwandamizi wa shirika la madaktari wasio na Mipaka Medicine San Frontiers ameelezea kuwa mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola katika mataifa matatu ya magharibi hauwezi kudhibitika.

Mkurugenzi wa Oparesheni katika shirika hilo Bart Janssens ameliambia shirika la habari la A.P kwamba ugonjwa huo utasambaa hadi katika mataifa mengine iwapo hakutakuwa na mwitikio wa kimataifa.

Ugonjwa wa Ebola tayari umesababisha vifo vya takriban watu 330 nchini Guinea,Sierra leone na Liberia.

Bwana Janssens amesema kuwa shirika la MSF limefikia kikomo cha uwezo wake wa kukabiliana na ugonjwa huo.

Chanzo: BBC
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom