- Thread starter
- #61
Mwanzilishi nipo hapa nakuchora unavyotetea hao kina BBC na DW SwahiliKwani thread inasemaje au unachangia bila kujua hata mwanzisha thread kauliza nini?
Swala langu kubwa lilikuwa kwanini yanayoendelea Marekani wanadonyoa donyoa tu na hawataki kuingia ndani kwa kutoa analysis ya kina kwa kinachoendelea huko?
Je, ingekuwa hayo yanayoendelea huko yametokea huku kwetu wangedonyodonyoa juu juu tu?
Sasa naona umejitahidi sana kuegemea kwamba wao wanajishughulisha zaidi na Maziwa makuu. Hapa hakuna anayebisha.
Hoja ni kwamba, sisi wamaziwa makuu hatustahili kuletewa kinachoendelea huko duniani kwa uzito ule ule na kwa mchambuzi wa kina?
Naona watu wanasema kwamba ni ushamba kusubiri BBC /DW Swahili watuletee kwa kina habari za huko duniani, twende kwa BBC/DW yenyewe ya Kiingereza.
Kwa hiyo kazi yao ni kutuchambulia habari zinazotokea hapa hapa ndani ya eneo letu la Maziwa makuu na kuwapelekea duniani jamii ya wanaoongea kiswahili lakini yanayoendelea huko duniani sio kazi yao kutuletea kwa undani zaidi