BBC na DW kinachoendelea Marekani hamkioni?

Kingjr2

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2018
Posts
644
Reaction score
1,276
Hivi vyombo vya habari vya kimataifa viko bize na update za korona wakati huo huo Mataifa mengi yakiwa bize na maandamano na mikusanyiko ya kuwasapoti wamarekani weusi wanaodai haki ya kutonyanyaswa na polisi wa kizungu ambapo hakuna social distance wala barakoa.

Hivi vyombo vya habari huu ndio muda sahihi wa kujitafakari. Wakigusia kinachoendelea huko wanadonyoa donyoa wala hata hawaingii ndani kwa kuhoji wachambuzi.

Tuseme hawataki kulikuza, lakini tujiulize ingekuwa yanatokea Afrika wangedonyoa donyoa juu juu tu au ndio ingekuwa ajenda kuu?

DW leo habari yao kubwa ilikuwa Chadema kuanza mchakato wa Urais, habari ambayo imetafutiwa mchambuzi wakati tulishaichambua hapa JF.
 
Kasikilize BBC ile ya kingereza, muda mwingine muwe mnatafuta muda kujiabarisha tofauti kati ya hizi idhaa na malengo yake.
Kwa hiyo hizi idhaa malengo yake ni kutafuta habari mbaya mbaya za Afrika na kuzipeleka duniani ila kutuletea kinachoendelea duniani kwa lugha yetu tuelewe sio malengo?
 
Kwa hiyo hizi idhaa malengo yake ni kutafuta habari mbaya mbaya za Afrika na kuzipeleka duniani ila kutuletea kinachoendelea duniani kwa lugha yetu tuelewe sio malengo?
Ndio kinachoonekana Sasa kuna vitu vinajitokeza siku hadi siku
 
Kwa hiyo hizi idhaa malengo yake ni kutafuta habari mbaya mbaya za Afrika na kuzipeleka duniani ila kutuletea kinachoendelea duniani kwa lugha yetu tuelewe sio malengo?
Kama ya Afrika ni mbaya, ni mbaya tu, haitakuwa nzuri kwa kuripoti mbaya ya Marekani
 
Hivi nyie huko bado hamjafanya maandamano kabisa!
 
Embu tuambie America kunaendelea nini, niko hapa Getens, Minnesota na hakuna shida watu tunafanya shughuli zetu as usual
 
Kama ya Afrika ni mbaya, ni mbaya tu, haitakuwa nzuri kwa kuripoti mbaya ya Marekani
Hakuna jamii utamulika mabaya na uyakose. Wakija Afrika watamulika negative na kweli zitaonekana. Huko kwingine hawayamuliki ndiomaana hatuyaoni. Kutoyamulika sio kwamba hayapo.
 
Kwa hiyo hizi idhaa malengo yake ni kutafuta habari mbaya mbaya za Afrika na kuzipeleka duniani ila kutuletea kinachoendelea duniani kwa lugha yetu tuelewe sio malengo?
Hizo habari mbaya mbaya za Afrika wanazotangaza BBC swahili na DW wanamtangazia nani kama siyo waaafrika wanaoongea hizo lugha? Ukitazama BBC ya Kingereza uwa unaona habari nyingi ni za Afrika?
 
Hakuna jamii utamulika mabaya na uyakose. Wakija Afrika watamulika negative na kweli zitaonekana. Huko kwingine hawayamuliki ndiomaana hatuyaoni. Kutoyamulika sio kwamba hayapo.
Kwani maandamano ni habari mbaya? Labda mbaya kwa nchi za kwetu, lakini kwa taifa lenye demokrasia, hiyo ni habari nzuri. Sasa kama hawajatangaza, tafuta chanzo kingine, hapo ni sawa na kulilalamikia gazeti la Uhuru kwa kutoonyesha mkutano wa wapinzani
 
Tukio hilo la mmarekani mweusi ndio litakalo futa kabisa habari ya corona duniani.
 
Wewe una shangaa BBC na DW, mimi mpaka sasa wanaharakati wa haki za binaadamu sijawasikia kabisa au labda Ulaya hawapo.

Wala viongozi wa mataifa makubwa wakikemea uvunjivu wa haki za binadamu au labda mkubwa mwenzao.
 
Hiyo BBC unayoongelea ni kwa ajili ya Maziwa Makuu. Ndio maana wanaongelea mambo ya Maziwa Makuu na lugha zake ni Kiswahili, Luganda na Kinyarwanda. Sisi tunaoangalia BBC na DW za Kimombo tunakwambia kuwa wanaongelea yanayotokea Marekani siku nzima mpaka ina-bore. Acha ushamba. Tune in BBC News English Service. Kama Umombo haupandi, endelea kusubiri Salim Kikeke, uangalie habari za CHADEMA, ule, ukalale.
 
Kinachoendelea Marekani kingekuwa kinatokea Tanganyika basi kwa sasa waandamanaji karibia wote wangekuwa na majeraha , wengine wangekuwa mahabusu, wengine wangeshazikwa.
 
Wameuwawa watu kwenye maandamano na polisi hapa.

Wameuwawa wauza madini hapa, mambo ya ile kesi ya Zombe.

Je DW au BBC walishadadia hayo kuliko la George Floyd?

Hayo si ndiyo yalikuwa na ulinganifu wa kulinganishwa zaidi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…