nope, haitawezekana, yaani hata gadafi si alimwambia kuwa "a true revolutionist does not retire or loose"; so kupiga kura ni maigizo tu wajameni kwa nchi zetu nyingi za Afrika-a laughing stocknauliza wana jf hivi kweli hata kura zipigwe museveni asipate kura hata moja ataondoka madarakani?
BBC wanajua kuhusu Daniel Arap Moi wa Kenya? Kuhusu Abdou Diouf wa Senegal ? Kuhusu John Kufuor wa Ghana ? Kuhusu Thabo Mbeki wa South Afrika ? Kuhusu Seaka Stevens wa Sierra Leone? Kuhusu Julius Nyerere wa Tanzania? Kuhusu Nelson Mandela wa South Afrika? Kuhusu Kenneth Kaunda wa Zambia ?
Au wote hao hawakuwa marais wa Afrika ? Wame/ watafia madarakani wote hawa ?
BBC Kiswahili walitangaza leo jioni kwamba inaonekana marais wa Afrika wamebuni mfumo mpya wa demokrasia. kwamba waliopo madarakani wakishindwa kwenye uchaguzi hukataa matokeo. Lengo ni kukaribisha wasuluhishi ambao hupendekeza serikali ya pamoja kati ya rais aliyeshindwa na yule aliyeshinda. Imetokea Kenya, Zimbabwe, na inaonekana inaweza kutokea Ivory Coast.
Zanzibar wao waliwahi kuiweka mapema kwenye katiba kabla ya uchaguzi, ili kupunguza muda na gharama za usuluhishi wa kimataifa. Lakini, uchakachuaji je?
BBC Kiswahili walitangaza leo jioni kwamba inaonekana marais wa Afrika wamebuni mfumo mpya wa demokrasia.
Marais nani na nani? wamebuni mfumo mpya wapi?
Jamani Africa kubwa na ina nchi nyingi, kuilundika yote pamoja ni insulting.
Pia nashindwa kutokukubaliana nao kwa sababu najiuliza hapa kwetu Dr.Slaa angenga'ngania kingetokea nini?
Issue ya Ivory Coast kidogo ni tofauti na Zimbabwe au Kenya ambapo either tume ya uchaguzi ILIAMUA/ILIAMRISHWA kuwa bubu au kutangaza matokeo favouring the incumbent. Ivory Coast ile tume huru ilithubutu kutangaza matokeo ''halali'' yaliyoonyesha kuwa current president ameshindwa uchaguzi.
Wanachofanya umoja wa Africa (Mbeki kama mwakilishi) ni upuuzi tu. Anakwenda kusuluhisha nini sasa? kwa nini Gbagbo asiamrishwe kuachia ngazi haraka iwezekanavyo?
Afadhari UN, France na USA wameshatangaza bila kumung'unya maneno kwamba Gbagbo kapigwa chini na aheshimu maamuzi ya wananchi. Sina uhakika kama kuna Rais yeyote kutoka Africa ambaye kasimama hadharani na kutoa tamko lolote. Wanajua itakuwa zamu yao kung'ang'ania madaraka muda si mrefu
Tatizo la BBC ni ku-generalize kuwa Africa nzima imekuwa ovyo..
Dr. Slaa asingeweza kung'ang'ania kwa sababu:
1. Tume ya uchaguzi haikusema yeye kashinda. JK ndo alitangazwa mshindi.
2. Katiba ya nchi inasema kwamba matokeo ya urais yakishatangazwa na ''mshindi'' akaapishwa ndani ya siku 7, ndo mwisho wa mchezo. Hakuna mahakama yoyote yenye uwezo wa kupokea kesi kupinga matokeo hayo.
Kama Dr. Slaa angeamua kung'ang'ania, angeishia kukamatwa tu na possibly kufunguliwa mashtaka kkwa ''kuhatarisha amani'' ya nchi.
Ndio maana CHADEMA na wadau wengine wanapiga kelele ya kuanzishwa mkakati wa kuandika katiba mpya na uteuzi wa tume HURU kabisa ya uchaguzi. CCM wanajua hii ikipita, mwisho wao utakuwa umefika
Pamoja na kwamba tume haikutangaza, Mugabe alishindwa Uchaguzi wa mwisho. Mataifa yalimwambia yakiwemo ya afrika walimtaka akabidhi madaraka. Alipokataa wakaleta upatanishi (Mbeki) na serikali ya pamoja ikafuata.
Wanasema ''kama huna data (evidence), huna haki ya kusema. Issue kwamba Mugabe ALISHINDWA ni debatable. Tume ya Uchaguzi ilimtangaza yeye kama mshindi na yule Tsvangirai hakuwa na ''data'' za uhakika kuonyesha kwamba ameshinda!
Upatanishi wao uliamuliwa baada ya watu kuanza kuchinjana
Hilo la overgeneralization nakubaliana na wewe, ila nilitaka pia utambue kwamba wanazungumzia marais walio madarakani sasa na wala siyo wastaafu.
Pia nashundwa kutokukubaliana nao kwa sababu najiuliza Hapa kwetu dr Slaa angenga'ngania kitokea nini?