Na kwa upande wa pili.
Nyinyi jamaa ambao mliowatelekeza Watoto wenu, ambao ni Damu yenu, hivi nafsi zenu haziwasuti?
Unampa MIMBA Demu kisha ukishasikia anaujauzito, wewe Njemba unalala mbele.
Halafu hutaki tena kusikia chochote/lolote kutoka kwa yule uliompachika MIMBA.
Au kuna wale ambao wanavumilia mpaka Mtoto atakapozaliwa, na Mtoto akishazaliwa tu, wakishaanza kuona gharama za hapa na pale basi kinachofuata ni kukimbia majukumu.
Sasa kwanini unayakimbia majukumu!
Kwanini uwe Mwoga wa Maisha!
Na cha kushangaza Watu wa Sampuli yenu Mtoto atakapokua na kuwa na Unafuu wa Kimaisha, Mtoto huyo huyo uliemtelekeza/uliemkimbia unamfuata na kuanza kudai,
"Huyu ni Mwanangu".
"Huyu ni DAMU yangu"
Sasa Siku zote ulikuwa wapi?
Damu yako baada ya kuona mambo ya Mbolea!
Hivi nyie Watu mbona mnakuwa vigeugeu!
Acheni hizo.
Usikimbie majukumu.
Majukumu kabiliana nayo.
Maisha ndivyo yalivyo.
Hayo ndio Maisha.
Na hizo ndio changamoto zenyewe.
Bila ya changamoto Maisha hayawezi kwenda.
Kwani unavyosema natafuta, unafikiri unamtafutia nani?
Kutafuta maana yake ni kwa ajili ya wewe, na kwa ajili ya Kizazi chako.
Pata Watoto.
Lea Watoto.
Watoto wanatakiwa wafurahie Matunda ya Mzazi wao.
Watoto wanatakiwa WADEKE mbele ya Mzazi wao.
Watoto wanatakiwa wafurahie Maisha pale Mzazi wao anapokuwepo.
Watoto wapewe maadili mema.
Usikubali Watoto wako waishi kinyonge hata siku moja.
Hata kama unakula BATA hakikisha MIZANI inashabihi.
Sio wewe unakula BATA Watoto wanachapika.
Kama unaona mambo hayaendi sawa, ua BATA halafu zingatia kwa Watoto wako.
Mambo yakitiki basi ni BATA kwa kwenda mbele.
Na kama upo/umo kwenye NDOA basi wewe achana na BATA, na cha kufanya ni kufurahia MAISHA na FAMILIA yako.
Watoto wana raha sana.
Napenda sana Watoto.
WATOTO!
Acha tu