Bayport-Oneni huruma kwa wazazi wetu

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Wana JF
kiukweli hawa BAYPORT hawana huruma kabisa hususani kwa wazazi wetu wasioelewa nini maana ya mkataba,

BAYPORT wamemrubuni mzazi wangu(MWANAHEWA HASSAN MTOLERA) ambaye ni mwalimu pale MPWAPWA-DODOMA na kumfanya akope laki moja unusu(150,000),lakini cha kushangaza BAYPORT wanamkata mzazi wangu laki nane (800000) yaani analipa mara tano ya ile pesa aliyokopa,sasa je huko ni kumsaidia ama kumwibia?

kwanini BAYPORT msitafute pesa zenu kiharali kabisa pasi kuwaibia wazazi wetu kwa kuwapa mikataba isiyo onekana?


wanasheria naomba msaada wetu,nahitaji kuwapeleka mahakamani BAYPORT kwani wakifanyacho ni unyonyaji na hakitakiwi kufumbiwa macho


LEO NI MZAZI WANGU,KESHO ATAKUWA MZAZI WAKO
 
Daa sasa Eng umeshindwa kweli kumsaidia 150k? Hzi financial institutions ndogo ndogo ni wezi ajabu,kuna platnum credit nayo ni nomaaaaa!
 
Daa sasa Eng umeshindwa kweli kumsaidia 150k? Hzi financial institutions ndogo ndogo ni wezi ajabu,kuna platnum credit nayo ni nomaaaaa!

kaka huwezi amini,yaani leo nampigia simu mama na kumwuliza kuhusu habari za yeye kwenda DODOMA,mwanzo alikuwa akinificha lakini mwishowe ndipo alipo nieleza kuwa alikwenda DOdoma kufuatilia na kuwauliza BAYPORT kwanini wanamkata 50,000 kwa kila mwezi wakati tayari deni alisha lipa na ktk deni inaonekana anatakiwa kulipa laki nane

majibu kutoka kwa BAYPORT hayakueleweka na ndipo mama alipo amuwa kuwaacha wakate hadi wamalize deni lao,lakini nikamwambia kuwa wanakuibia hao,akasema kuwa hata mkurugenzi alisha waandikia barua kusitisha makato hayo,lakini bado wanaendelea kumkata

hakika tanzania inahitaji mabadiriko,tumenyonywa na weupe,sasa tunanyonywa na weusi tena bila huruma,shida zetu ndio zinazo tuumiza
 
Mkataba aliousaini amepewa(ana copy?) kama anacopy peleka wezi hao mahakamani. Vibaka hao.
 
nasikia bayport inamilikiwa na kigogo hapa mjini,wamefikia hadi kuwa na kesi za kufoji maelezo ya watu na kuwadai mikopo hewa...sanasana walimu..fuatilia kaka
 
nasikia bayport inamilikiwa na kigogo hapa mjini,wamefikia hadi kuwa na kesi za kufoji maelezo ya watu na kuwadai mikopo hewa...sanasana walimu..fuatilia kaka

watafute pesa kwa njia sahihi na si kulazimisha na kuwaonea walimu tena kwa kuwalazimisha kuwakata madeni wasiofaidika nayo.

Wanasheria naomba msaada wenu

lakini pia mbunge wa mpwapwa,huyo ni mpiga kura wako anaenyanyaswa naomba ulifuatilie hilo na mwalimu huyo apewe haki yaki
 
Mkuu natumaini umesoma
naamini ungekuwa msaada mzuri kwa mama kabla ya kuleta mamalalamiko huku..sijui kipato chako lakini hata kumpa wazo tu
hakuna wahuni ama wezi kama hao jamaa na wale wa blue..kwa ambao awajui hi ni taasisi ya wahuni kadhaa mmoja alikuwa waziir anaongoza bandari yetu hivisasa na mwingine ni waziri mshenzi namwita mshenzi maana ametuibia uda sasa amekutwa ameiba hata manispaa sijui ni nani ...hawa waliongozwa na vijana wa lioba pesa pale baclays kwa kukusaidia pesa nyingi hizo kuanzisha hayo matakataka ni mali za baclays wakapewa pekekwa kesi maahakamani wazee wakasimamia sidhan kama ipo tena ..ni huzuni kubwa kama ni mpenzi wa hizo takataka
pole kwa mama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom