BAWASA, Babati kero ya maji chumvi mmeshindwa kuiondoa?

MfalmewaKiha

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
1,191
1,237
Ndugu zangu poleni kwa majukumu ya kila siku.

Leo naomba nitoe malalamiko yangu kwa Halmashauri ya mji wa Babati hasa upande wa idara ya maji. Hivi kweli Idara ya maji mmekosa kabisa namna ya kutibu maji kutoka katika hali ya chumvi na kuwa maji Matamu?

Mbaya zaidi wananchi wanaona kama hali ya maji kuwa chumvi ni jambo la kawaida.

Mbunge, Waziri mhusika hebu tusaidiane swala hii kama linawezekana, ili tupate maji salama na mazuri.

Mwisho:
Naombeni mtoe elimu kwa umma kuhusu usomaji wa mita zenu za maji, maana inafikia hatua kama vile mnakadiria bili.

Msiponipa majibu hapa kuhusu swala la maji ya chumvi wananchi hatutawaelewa.
 
Back
Top Bottom