BAWACHA kuhamasisha maandamano ya wanawake nchi nzima

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Baraza la wanawake mkoa wa Mbeya , limetishia kuhamasisha maandamano ya wanawake nchi nzima kulishinikiza bunge kuwaondoa Bungeni, wabunge 19 wa viti maalumu wanaodaiwa kutokana na CHADEMA, wakidai uwepo wao Bungeni ni kinyume Cha katiba.

Akizungumza leo katika ofisi za CHADEMA jijini Mbeya , baada ya mkutano, mwenykiti wa BAWACHA mkoani humo, Bi. Elizabeth mwakimomo amesema (nanukuu) ;
"Tunaomba Mh. Raisi Samia Hassan aangalie kwa macho mawili , Ndugai anatakiwa kujiuzuru, Tulia Akson aombe radhi mbele ya watanzania, Kama haya hayatafanyiwa kazi, Tutaandamana nchi nzima, tutawashawishi, tutaenda mpaka Dodoma kuhakikisha wale wabunge wanatoka ndani ya Bunge.

Source : ITV
 
Wivu wa kishamba sana, serikali haifanyi kazi kwa mihemko ya walioahidiwa ubunge wa viti maalum baada ya kulalwa na Dj.
 
Bawacha bwana....wale wamama wametoa bonge la "shoo" eti: "Spika Ndungai ajiuzulu, na Tulia Akson aombe msamaha..."
Wabaguzi wakubwa hawa, mwanamke mwenzao aombe msamaha, mwaume ajiuzulu...taratibu tutafika tu!
 
Kiutaratibu kwakua CHADEMA hawautambui uchaguzi mkuu uliopita na hawawatambui wabunge hao basi hawana mamlaka yakuendelea kuwabughuzi.

Labda waende mahakamani wapate tafsiri yakisheria toka kwa spika kwanini kawaweka bungeni watu wasio wanachama, lakini nje ya hapo kelele zitaendelea mpaka 2025 wanapomaliza muda wao.
 
Baraza la wanawake mkoa wa Mbeya , limetishia kuhamasisha maandamano ya wanawake nchi nzima kulishinikiza bunge kuwaondoa Bungeni, wabunge 19 wa viti maalumu wanaodaiwa kutokana na CHADEMA, wakidai uwepo wao Bungeni ni kinyume Cha katiba.

Akizungumza leo katika ofisi za CHADEMA jijini Mbeya , baada ya mkutano, mwenykiti wa BAWACHA mkoani humo, Bi. Elizabeth mwakimomo amesema (nanukuu) ;
"Tunaomba Mh. Raisi Samia Hassan aangalie kwa macho mawili , Ndugai anatakiwa kujiuzuru, Tulia Akson aombe radhi mbele ya watanzania, Kama haya hayatafanyiwa kazi, Tutaandamana nchi nzima, tutawashawishi, tutaenda mpaka Dodoma kuhakikisha wale wabunge wanatoka ndani ya Bunge.

Source : ITV
Hasira za kuhama viongozi wao nyalandu & Co. Halima Mdee siyo size yenu. Ndiyo maana prof Jay kaimba utaniambia nini.
 
Kwa tabia hizi kama taifa tunakazi sana sasa wakeshatolewa nyie mnapata nini? Mbona mnanipa wakati mgumu
 
Waende Barabarani
Vijana wao watawavunja Miguu
Mama zetu tulieni ndani
Mpike Vyakula
 
Kiutaratibu kwakua CHADEMA hawautambui uchaguzi mkuu uliopita na hawawatambui wabunge hao basi hawana mamlaka yakuendelea kuwabughuzi.

Labda waende mahakamani wapate tafsiri yakisheria toka kwa spika kwanini kawaweka bungeni watu wasio wanachama, lakini nje ya hapo kelele zitaendelea mpaka 2025 wanapomaliza muda wao.
Madai ni kwamba hao wabunge 19 walishavuliwa uanachama wa CHADEMA, kwa hiyo kikatiba walishapoteza sifa ya kuwa wabunge, Sasa wanauliza ni kwa nini spika wa Bunge Bw. Job Ndugai anavunja katiba ya nchi kwa kuwakumbatia?
 
Hata hao wanaoomba kukutana na Raisi hawana hoja utakuta wanamweleza tunataka maandamano sasa hivi watu wapo bise kuzalisha mali boda boda na wamachinga mliokuwa mnawatumia sasa hivi hamuwapati kwani hawabugudhiwi tena kwenye shughuli zao
 
Madai ni kwamba hao wabunge 19 walishavuliwa uanachama wa CHADEMA, kwa hiyo kikatiba walishapoteza sifa ya kuwa wabunge, Sasa wanauliza ni kwa nini spika wa Bunge Bw. Job Ndugai anavunja katiba ya nchi kwa kuwakumbatia?
Spika alishasema kuwa hajapokea barua ya kuwavua uanachama, hata wewe kama unayo barua tutumie jukwaani.
 
Hatare! Kama ndivyo, kwa nini wanalalamika? Au spika hajawaandikia barua kuwajulisha hajaipata barua ya kuwavua uanachama?
 
Walitakiwa wao wajiridhishe kuwa barua imefika na sio kupayuka payuka. Nje ya mada; CHADEMA hawautambui uchaguzi na hawajapeleka watu bungeni na walioenda wamewavua uanachama hapo ilitakiwa watulie au wateue wengine kama waliopo hawawatambui.

Kuna utoto mwingi unaendelea pale CDM.
 
Sawa mkuu! Ngoja tuone mwisho wa haya utakuaje.

Muda utaongea!
 
Back
Top Bottom