BAVICHA wajifungia Siku Nne Kupanga Mikakati ya Kuikabili CCM 2020

Zapa RadioFm

Senior Member
Feb 12, 2016
112
171
Baraza la Vijana wa Chadema ( BAVICHA) wamejifungia kwa siku nne mfululizo ,kutathimini Uchaguzi mkuu uliopita na mikakati mipya ya Kuikabili na kuishinda Ccm katika uchaguzi mkuu ujao wa Mwaka 2020.

Kikao hicho kikali cha,kiliongozwa na M/kiti wa BAVICHA Taifa Patrobas Katambi na kuhudhuriwa na Viongozi wote wa Kitaifa wa BAVICHA.

Kikao hicho pia kili wakutanisha Bavicha na M/kiti wa Chama Taifa pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa chama kujadili mustakabali mpya wa mikakati ya BAVICHA na chama kwa miaka mitano.

Mambo mengi yamejadiliwa ikiwa ni pamoja na nini kifanyike ili BAVICHA iendelee kuwa Injini ya chama na kitivo cha kuandaa Viongozi wa chama na Taifa baadae.

Imetolewa na,

Edward SIMBEYE
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa
 

Attachments

  • IMG-20160213-WA0026.jpg
    IMG-20160213-WA0026.jpg
    132.9 KB · Views: 22
  • IMG-20160213-WA0022.jpg
    IMG-20160213-WA0022.jpg
    85.3 KB · Views: 38
Mngemualika baba wa ufisadi Tanzania Lowasa awape mbinu za kuwa mafisadi.
 
ni ulofa na upumbavu kuwaza uchaguzi wa 2020 wakati kuna uchaguzi wa 2019 mitaa ambao ndiyo picha ya 2020

waseme waenda kumalizia bajeti ya viroba vilivobakia 2015
 
Wote mliochangia kwa kubeza, kwa dharau, mipasho, na maneno mengine ya hovyo, mtakuwa hajitambui, for sure ni upofu wa uelewa.

Hata hivyo najiuliza kilichowafanya mjitokeze kwa haraka na kuchangia kwa aina isiyo na tija kwa taifa ni nini? Je ni posho mnalipwa kuandika uchafu huu usiopendeza kwa watanzania wapenda maendeleo!
Nilichojifunza ni kwamba mko nje ya mfumo wa maisha ya wanadamu duniani, maana hata hamjui siasa ndio zinaongoza nchi kwa chama kuunda serikali. ..Lkn hamjui kuwa mfumo wa vyama vingi hata Tanzania upo, na imedhihirika kupitia michango yenu kwamba hamjui vyama vingi Tanzania vimesaidia sana kubadilika kwa serikali hii. ....hamjui ni mambo gani yamesababishwa na uwepo wa vyama vingi ktk uendeshaji wa serikali na wananchi kujua na kutambua haki zao, imeonekana hamjui mchango wa vyama vingi Tanzania kwenye kueneza elimu ya uraia. ....

Na ndio maana mnabeza kikao cha BAVICHA, mnabeza kwa ulofa wa fikra. ...kama cha siasa kupitia taasisi yao ya vijana mlitaka wasikae vikao vya tathimini na kisha kupanga the way forward. ....Lakini vijana nyinyi wa Lumumba hamjui kuwa chama cha siasa duniani lengo lake ni kushika dola. ...sasa wasipojipanga mlitaka watekelezaje mambo yao?

Huu ni ulofa wa hali ya kiwango cha juu kuwahi kuonyeshwa wazi wazi na vijana hawa wa Lumumba. ...hakuna jambo linaenda bila mipango. ..

Nawashauri BAVICHA msikatishwe tamaa na mahafidhina hawa wasiojitambua. ....endeleeni kupanga mipango, tena mpange mipango inayotekelezeka kuelekea uchaguzi ujao maana mwisho wa uchaguzi ni mwanzo wa uchaguzi ujao. ...na walisema wahenga kwamba
"The Ealier The Better"
 
Du watu wengi wengine post zao uozo hadi zinanuka.makamanda pangeni mikakati kijani zimejaa Sana'a tu
 
Sisi wana UKAWA tutaanza kuyaamini mabadiliko chini ya magufuli endapo tu ataanza kushughulikia waizi wa ESCROW MEREMETA EPA bila kumsahau fisadi wetu mkuu LOWASA na lirichmond lake
 
Huyo katambi ubunge kashindwa atawezaje kuongoza mbio za kupeleka chadema ikulu
 
I feel sorry kwa Makamanda hawa,

Naona sare za chama zimeanza kuwa nzito mabegani mwao. Namuona Mkiti Vijana, Mwalim Salim na wengine wengi hapo hawajavaa sare za chama ikiwa wako kwenye shughuli rasmi ya kichama. Hali hii haikuwapo awali, Sare ya Chadema ilikuwa ni kitu adimu sana mitaani na vijiweni. Ilikuwa ni thamani ya kipekee kuonekana ukiwa ndani ya Gwanda iwe la kaki au jeusi... sasa sijui kimetokea nini?

Hii kwa mtu anayejua kusoma Saikolojia haijakaa vema. Kuna kitu cha ziada kinapaswa kifanyike ndani ya chama ili kuibua morali iliyokuwapo awali.

Ninaimani kubwa juu ya uwezo mkubwa wa Mkiti wetu nadhani ataliangalia hili. Kwasasa inaeleweka wazi nafasi ya Katibu mkuu inamuumiza kichwa.

BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom