BAVICHA: Tupo nyuma ya Dr Slaa hadi mwisho

BAVICHA: Tupo nyuma ya Dr Slaa hadi mwisho

Serayamajimbo

Senior Member
Joined
Apr 15, 2009
Posts
191
Reaction score
40
Bavicha Mkoa wa Singida, wameibuka na kuwaunga mkono wenzao wa Mwanza kwa kusema kuwa watasimama nyuma ya Katibu Mkuu huyo hadi mwisho wa mapambano.

SIKU chache bada ya Baraza la Vijana wa Chadema Mkoa wa Mwanza kutamka kuwa hawako tayari kuunga mkono maandamano ya kumpinga Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa,Bavicha Mkoa wa Singida, wameibuka na kuwaunga mkono wenzao wa Mwanza kwa kusema kuwa watasimama nyuma ya Katibu Mkuu huyo hadi mwisho wa mapambano.

Kupitia taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari na Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Singida, Josephat Isango, vijana hao wameeleza kusikitishwa kwao na wenzao wanaompinga Dk Slaa, huku wakidai kuwa wenzao hao wanatumiwa na wanasiasa wa upande wa CCM.

Walidai kuwa huo ni utekelezaji wa propaganda kutoka Idara ya Uenezi ya CCM.
Katika siku za karibuni vyombo vya habari viliripoti hatua iliyoelezwa kuwa ya Bavicha, kumshinikiza Dk Slaa kuachia ngazi kwa madai ya kumiliki kadi ya CCM, madai yaliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

Isango katika taarifa hiyo ya jana alidai kuwa, baadhi ya vijana waliofukuzwa na Chadema kutokana na utovu wa nidhamu, ndiyo wamekuwa wakiendeleza mapambano hayo ili kukichafua Chadema, kionekane kuwa na migogoro wakati ukweli ni kwamba hakuna hali hiyo.

Alisema kuwa Vijana wa Singida walifanya uchunguzi na wabaini kuwa baadhi ya vijana wenzao ndiyo wanaotumiwa na Nape kwa masilahi ya CCM.Kutokana na hilo, Isango alimtaka Nape kuachana na kile alichokiita kuwa ni siasa za maji taka, akieleza kuwa siasa hizo zinalenga kuwarubuni na kuwaaminisha Watanzania kuwa CCM peke ndicho chama bora wakati siyo kweli.

"Hata hivyo, vijana waliosimamishwa uongozi ndani ya Chadema ni vyema wakajiunga na CCM wazi ili wakasaidie mafisadi waliosababisha maisha magumu kwa Watanzania. Watanzania wanajua hali yao ya maisha na ndiyo waamuzi sahihi wa Tanzania wanayoitaka, tusiwalishe maneno ya uongo kurutubisha ufisadi nchini," alisema. Isango aliongeza:

"Ni imani yetu kuwa, kila jambo linalofanywa ndani ya Chadema linakuwa na baraka njema kwa ajili ya ukombozi wa nchi yetu, lakini yako yanayofanywa kwa mashinikizo mabaya kama hili hayana nia njema kwetu."

Mwenyekiti huyo aliwatuhumu baadhi ya viongozi wa ngazi za juu ndani ya CCM kuwa wamekuwa wakitumika kwa ajili ya kukisambaratisha Chadema kwa mashinikizo yao binafsi na kwamba watu hao wanatamani kuona siku moja Chadema kikisambaratika.
 
Very good, mimi mwenye, niko nyuma ya Dr Silaa, kadi ya CCM kumilikiwa na Dr Silaa siyo hoja. After all hakupewa bure na ccm na wala siyo lazima kuirudisha kwani alikuwa anailipia, Kadi yangu ya CHADEMA, ni mali yangu na siyo mali ya chama na siku nikiondoka CHADEMA nitabaki nayo.

KEEP UP Dr. SILAA, TUKO PAMOJA KATIKA UKOMBOZI WA PILI WA TAIFA HILI
 
kifo cha CDM kimewadia ..hehehehe! ilikuwa ni upepo ... tu ule
 
Tupo pamoja dr.wewe mwenyewe unajua wananchi tulivyo na imani na wewe,usikate tamaa,chapa kazi tupo pamoja..
 
Nnauye Jr., Le Mutuz, na makamanda wengine wa CCM sasa hivi wanachekelea tu.
 
Kabla ya Uchaguzi wa mwaka 2015 tutasikia mengi. Lakini wenye akili watasimama.
Kama Nape anaweza kuwarubuni vijana hao, hawafai kuwa kundini.
 
Kweli hata mimi yanayoendelea Ni wehu kusapoti upuuuzi wa ccm kwani wao wameshindwa kusimamia maamuzi yao ya vikao halali.....wanatafuta kutupotezea
 
CCM hawawezi salimika hata kwa CDM dhaifu.Sasa kma Slaa alikuwa CCM mbona wao ndo wanashida na yeye kuwa upinzani?
 
SIKU chache bada ya Baraza la Vijana wa Chadema Mkoa wa Mwanza kutamka kuwa hawako tayari kuunga mkono maandamano ya kumpinga Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa,

Bavicha Mkoa wa Singida, wameibuka na kuwaunga mkono wenzao wa Mwanza kwa kusema kuwa watasimama nyuma ya Katibu Mkuu huyo hadi mwisho wa mapambano.

Kupitia taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari na Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Singida, Josephat Isango, vijana hao wameeleza kusikitishwa kwao na wenzao wanaompinga Dk Slaa, huku wakidai kuwa wenzao hao wanatumiwa na wanasiasa wa upande wa CCM.
Walidai kuwa huo ni utekelezaji wa propaganda kutoka Idara ya Uenezi ya CCM.

Katika siku za karibuni vyombo vya habari viliripoti hatua iliyoelezwa kuwa ya Bavicha, kumshinikiza Dk Slaa kuachia ngazi kwa madai ya kumiliki kadi ya CCM, madai yaliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

Isango katika taarifa hiyo ya jana alidai kuwa, baadhi ya vijana waliofukuzwa na Chadema kutokana na utovu wa nidhamu, ndiyo wamekuwa wakiendeleza mapambano hayo ili kukichafua Chadema, kionekane kuwa na migogoro wakati ukweli ni kwamba hakuna hali hiyo.

Alisema kuwa Vijana wa Singida walifanya uchunguzi na wabaini kuwa baadhi ya vijana wenzao ndiyo wanaotumiwa na Nape kwa masilahi ya CCM.

Kutokana na hilo, Isango alimtaka Nape kuachana na kile alichokiita kuwa ni siasa za maji taka, akieleza kuwa siasa hizo zinalenga kuwarubuni na kuwaaminisha Watanzania kuwa CCM peke ndicho chama bora wakati siyo kweli.

“Hata hivyo, vijana waliosimamishwa uongozi ndani ya Chadema ni vyema wakajiunga na CCM wazi ili wakasaidie mafisadi waliosababisha maisha magumu kwa Watanzania. Watanzania wanajua hali yao ya maisha na ndiyo waamuzi sahihi wa Tanzania wanayoitaka, tusiwalishe maneno ya uongo kurutubisha ufisadi nchini,” alisema.

Isango aliongeza: “Ni imani yetu kuwa, kila jambo linalofanywa ndani ya Chadema linakuwa na baraka njema kwa ajili ya ukombozi wa nchi yetu, lakini yako yanayofanywa kwa mashinikizo mabaya kama hili hayana nia njema kwetu.”

Mwenyekiti huyo aliwatuhumu baadhi ya viongozi wa ngazi za juu ndani ya CCM kuwa wamekuwa wakitumika kwa ajili ya kukisambaratisha Chadema kwa mashinikizo yao binafsi na kwamba watu hao wanatamani kuona siku moja Chadema kikisambaratika.

source: mwananchi
 
Wako nyuma wanatafuta nini? Waseme wako bega kwa bega.
 
Ni aibu kwa CCM kuja na hoja za ajabu ajabu. Mapandikizi yao nayo yameshindwa, mipango ya akina Wassira, Nape, Mwigulu, Kinana nayo imefeli.......JK sijui yu hali gani muda huu maana hiki chama lazima kimfie tu
 
He! Kuna jamaa angu alinambia kuwa bavicha ni "Balaza la vichaaa" sasa naanza kuamini, kila kukicha vituko
 
safi vijana waadilifu wa Bavicha.
CCM kwa ajili ya maslahi yao wanatamani Chadema isambaratike lakini haiwezekani, Mungu ni mwema.
 
Dr Slaa Daima!

Huyu ndiye mtu pekee anayewatia homa CCM.

Wengi wa viongozi Wa CCM wamashapata ugonjwa Wa CHADEMAPHOBIA na baadhi Yao Kama kina Nape, Kinana, Nchemba, nk (list ni ndefu) wameshapatwa Na Slaaphobia-ugojwa unaomfanya mtu anachanganyikiwa, kuongeaongea hovyo na hatimaye hupoteza fahamu Na mwisho wake ni kifo

Gari ya Chadema inaenda sawa kwa kuongozwa Na Mh Freeman Mbowe.

Nguvu ya umma Daima
 
Back
Top Bottom