BAVICHA na BAWACHA vinafanya nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAVICHA na BAWACHA vinafanya nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WATANABE, Apr 20, 2012.

 1. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Toka kuchaguliwa kwao uongozi wa BAVICHA na BAWACHA wamekuwa kimya sana kiasi cha kutukatisha tamaa sisi wasahabiki wa CDM. Inashangaza sana kuona kila jambo hata la kuhakikisha CDM inajijenga wameachiwa viongozi wa kitaifa.

  Ni kutokana na BAVICHA na BAWACHA kutokuwa active CDM imeshindwa kutayarisha wagombea wazuri kugombea ubunge wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA), kama wenzetu NCCR walivyoweza kufanya.

  Hivi sasa nilitarajia BAVICHA
  na BAWACHA wangekuwa active sana nchi nzima kuwahamasisha wananchi waliowachagua wabunge katika majimbo mbali mbali kuwatumia salamu wabunge wao wakiwataka wabunge wao hususan kutoka CCM waafiki na kuweka sahihi zao katika hoja iliyotolewa na wabunge wa upinzani bungeni ya kutaka wabunge 70 kuweka sahihi kuunga mkono kuwasilishwa kwa hoja ya kutaka Waziri Mkuu ajiuzuru kutokana na wizi mkubwa unaoendelea Serikalini.

  Endapo hamasa ya iana hii inefanikiwa kujengwa nchi nzima ingewapatia fursa wabunge wa CCM kupata sababu ya kuweka sahihi katika hoja hiyo ikiwa kama shinikizo toka majimboni mwao.

  Cha kusikitisha BAVICHA na BAWACHA viko kimya kabisa kana kwamba havipo kabisa. Je huku ndio asasi hizi kusaidia kukijenga chama?

  Naomba kuwasilisha
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Inabidi nguvu ya UMA iwatembelee nao hawa kwa uzembe na hasa BAWACHA.

  Huku BAWACHA ndiyo kumezidi maana hata sijawahi kuwasikia wakizungumzia chochote kile.

  Itabidi Chadema ifanye uchaguzi haraka hata kama ni kwa kuwakatiza hawa viongozi waliopo sasa hivi maana watu wengi hatuna imani nao. Kama Pinda wanamtafutia sahihi wamuondoe, basi BAWACHA sasa umefika muda au mjiondoe wenyewe kwa kukabidhi madaraka au na nyie mtafutiwe sahihi mpumzishwe. IMETOSHA SASA kuwakumbusha uwajibikaji.
   
Loading...