Huyu Jaji Mutungu lazima ana tatizo. Msajili wa vyama vya siasa anajigeuza kuwa msemaji wa ikulu? Kama ofisi ya Rais imeona kuwa Rais ameeleweka vibaya au Rais mwenyewe anataka kufuta kauli yake, kuna wasemaji wa Ikulu.
Inakuwa ni vigumu sana kuamini kuwa huyu Jaji ana kiwango kweli cha jaji. Ni uelewa mdogo ndiyo unaowafanya baadhi ya watu kudhani wao wana masikio na akili kuwazidi watu wote. Hivi kuna mtu ambaye hakumsikia na kumwelewa Rais kiasi cha kuhitaji ufafanuzi toka kwa Mutungi?
Ofisi ya Rais ina watu wengi sana, na siamini kama inahitaji usaidizi wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.
Mutungi tulia na shughuli na majukumu yako uliyopewa kisheria, huko kwako kwenyewe bado kuna matatizo mengi unaenda kurukia hata yasiyo kuhusu. Ningekuona wa maana kama ungejishughulisha kuwakutanisha CCM na UKUWA ili kuleta utengamano mzuri Bungeni kuliko kujipa majukumu ya kuwa msemaji wa Ikulu. Haijalishi ulichosema ni sahihi au siyo sahihi, cha muhimu ni kwamba hiyo siyo kazi yako.