Habari kutoka ILEMELA zinasema kuwa BAVICHA wamejipanga kusafisha wasaliti wote ndani ya baraza na chama kwa ujumla. Wa kwanza kushughulikiwa ni Mwenyekiti wa BAVICHA wa Wilaya SABINI RICHARD. Huyu Bw anatuhumiwa kumsindikiza Chagulani kwenda kufungua kesi dhidi ya chama, pia alimsindikiza Matata kwenye mkutano wake na waandishi wa habari baada ya [MATATA] kuwa amefukuzwa uanachama.
Tena inasemwa amekuwa akivuruga vikao vya kamati ya wilaya kwa kulazimisha rafiki yae J. ANAJUS arejeshwe kwenye nafasi ya ukatibu wa Wilaya ya Ilemela.
Juzi kwenye kikao alipobanwa alijitetea kuwa Matata ni rafiki wa mjomba wake aitwaye Costantine Kanyasu [DC wa Ngara] ambapo alisema hawezi kumsaliti Mjomba wake kwa ajili ya BAVICHA kwani BAVICHA sio baba wala mama yake. Kauli hiyo iliwaudhi wajumbe na wakaazimia uitishwe mkutano muu ili wakamg'oe yeye na wenzake akiwemo John Anajus.
Sisi tunatega masikio.