Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,353
- 26,194
Ni ushauri tu.Suala la akina Juliana Shonza limejadiliwa na kutolewa maamuzi. Waliofukuzwa,wamefukuzwa;waliokanywa,wamekanywa.Wote wameshapokea barua zao za kufukuzwa au kukanywa. Haki ya rufaa imeelezwa bayana kwenye barua husika. Nadhani yatosha.Mwenye kukata rufaa atakata.Aliyeridhika na maamuzi,atachukua hatua zake stahiki na kusonga mbele na maisha yake.
Si vyema ima hapa JF au mahali pengine kuendeleza mabishano,kejeli,tuhuma na mazungumzo yasiyo na msingi.Muendelezo huu iwe kwa waathirika wa maamuzi au hata Viongozi waliopitisha maamuzi una tafsiri moja:dharau kwa Katiba na Kanuni za chama.
Umefika wakati kwa BAVICHA na wanachama wake kuheshimu maamuzi yaliyofikiwa na kufuata taratibu za chama. Kila mmoja na aisome Katiba ya CHADEMA na Kanuni zake na ajiridhishe na taratibu zitakazomsaidia kusonga mbele.
BAVICHA sasa ijikite kwenye suala lingine. Ni muda wa kubadili ajenda. Ni muda wa kushughulikia uimarishaji wa chama na utekelezaji wa maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA ya kikao chake cha mwisho mwaka jana. Ukimya ni dawa tosha sana katika kadhia kama hii.Kila la kheri BAVICHA!
cc Molemo Crashwise Mungi eli, Ben Saanane Juliana Shonza Mchange Mtela Mwampamba Burton Gwakisa Exaud Mamuya TUNTEMEKE

Last edited by a moderator: