Yah: Kukata rufaa juu ya uamuzi wa chaso ARU kunifukuza uanachama

MWAISEMBA CR

Member
Apr 21, 2014
86
78
YAH: KUKATA RUFAA JUU YA UAMUZI WA CHASO ARU KUNIFUKUZA UANACHAMA
Kichwa cha barua hapo juu chahusika.
Mimi naitwa Simon Rogasian Chrispini mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu ARDHI nasoma shahada ya mipango miji na viji.

Nakata rufaa hii Kwa sababu ya uamuzi uliofanywa na Kamati Tendaji ya CHASO ARU wa kunifukuza uanachama mnamo tarehe 11th Mei 2018 kwa vifungu walivyovieleza 5.4.3 na 7.2.11ya katiba ya chama ya chama ya mwaka 2006 toleo la 2016, ambavyo havielezi sababu za kunifukuza kwao kinyume na kanuni za chama zinavyoeleza katika ibara ya 6.5.1.

Sambamba na hayo bado sijapokea barua ya kunifukuza uanachama Zaidi ya kupewa taarifa ileile ambayo ilitumwa kwa umma ambayo ndiyo wao wamenipatia na kudai ndiyo barua rasmi ya kunifukuza uanachama.

Ukiachilia mbali na kutokupewa barua na sababu za kunifukuza,bado ninazo sababu za kuendelea kukata rufaa kutokana uamuzi mbovu wa kutokuzingatia sheria za katiba na kanuni za chama pamoja na uonevu na chuki dhidhi yangu ambao unafanywa na baadhi ya viongozi wasiokitakia mema chama chetu.

Kwanza; kikao cha maamuzi cha kamati tendaji ya tawi kutokuwa halali:hii nni kwa sababu ya kuwepo na wajumbe ambao walikuwa wameshajiuzulu nyadhifa zao kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi mkuu wa tawi ambao ulikuwa umepangwa kufanyika hivi karibuni. Mfano mnamo tarehe 04/05/2018 majira ya saa tisa na dakika 57 aliyekuwa Katibu mkuu wa tawi alitoa taarifa ya kujiuzulu kwake katika nafasi ya ukatibu wa tawi kupitia kundi la chama la whatsap linalojulikana kama CHASO ARDHI UNIVERSITY.lakini chakusikitisha na kushangaza majira ya saa moja na dakika tisa jioni ya tarehe 04/05/2018, mheshimiwa Mwenyikiti wa tawi alimrudishia Katibu mstaafu ukatibu wake na viongozi wengine wote waliojiuzulu kwa mujibu na katiba ya chama ibara ya 6.3.4(a). hivyo miongoni mwa vioongozi hao waliokwisha kujiuzulu nyadhifa zao ndio hao hao waliokutana na kufanya kikao hicho cha kamati tendaji cha kunivua uanachama siku ya ijumaa ya tarehe 11/05/2018.

Pili; kukiukwa kwa taratibu na kanuni za kunifukuza uanachama: katika kanuni ya 6.5.2(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili. Kulinngana na kifungi hicho tajwa hakuna mahala popote nilipojulishwa makossa yangu hata kwa maneno. Si tuu kwa maandishi kumbe huu ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni zetu.

Sambamba na ibara ya 6.5.2 (a) pia kipengele (b), (c) navyo kwa pamoja vimeathirika kutokana na ukiukwaji huu wa kanuni na taratibu zetu za chama ibara ya 6.5.2 (a).
Tatu; viongozi kukosa Maadili ya Viongozi, Sifa Mahususi za Viongozi na Maadili ya Wanachama kama inavyoelezwa katika kanuni ya 10(x).Kumekuwepo na tabia ya viongozi na baadhi ya wanachama kutoa tuhuma bila kuwa na uthibitisho na kuchukua maamuzi ya tuhuma zozote wanazoletewa.

Mfano,siku ya alhamisi tarehe 26/3/2018 aliyekuwa Katibu wa tawi mwaka 2016/2017 (Ndg. Fidelis Ndonghwe) alitoa tuhuma nzito dhidhi yangu kuwa natumika na CCM. Ghafla bila hata ya kutafakari viongozi walichukulia hatua ya kunitoa kwenye kundi la chama na kuendelea kunichafua kwa umma na wanachama kwa ujumla jambo lilopelekea kutokupewa hata sapoti wakati wa kugombea nafasi ya Uraisi ARUSO kwa tuhuma hizo. Wakidai kwamba wananichunguza wakiahidi watatoa ripoti ya uchunguzi kabla ya uchaguzi wa ARUSO kuanza.

Mbaya Zaidi pamoja na kuhojiwa sana na wanachama wakiomba majibu ya uchunguzi huo, bado viongozi walikataa kutoa majibu ya uchunguzi huo na mpaka hivi sasa na kuendelea kudai kuwa natumika na CCM hivyo siwezi kwenda pamoja na chama kwenye uchaguzi ulokuwa mbele yetu, isipokuwa wale tuu walioandaliwa na viongozi hao ambao walikuja kukatwa na tume ya uchaguzi wa Aruso hapo baadae,jambo lilopelekea chama kukosa wawakilishi kwenye uchaguzi huo. Ndipo tarehe 17/04/2018 majira ya saa nne na nusu usiku baadhi ya viongozi wa chama waliamua kunifuata nyumbani kwangu kama mbadala wa chama na mgombea niliyebaki katika kinyang’anyiro hicho baada ya wenzangu kukatwa.

Kinachonishangaza mimi niliweza kukubali kufanya kazi na chama katika kipindi kile cha uchaguzi licha ya kuwa ndio waliokuwa wamenituhumu kwa tuhuma nilizozitaja hapo awali. Nilishirikiana nao kwa hali na mali katika kampeni na masuala mengine yote ya uchaguzi katika kuhakikisha kwamba tunapata ushindi. Lakini ndo hivyo hatukushinda kama tulivyokuwa tunategemea.

Tuhuma nyingine ziliibuka kutoka kwa mwanachama JUVENALI SHIRIMA (Katibu CHASO mkoa wa Dar es salaam) kwamba mimi na mwanachama mwenzangu ndugu CHARLES RICHARD MWAISEMBA ndio tulioandika barua ya rufaa kushinikiza tume ya uchaguzi ARUSO kuwakata wagombea wa nafasi ya urais kupitia CHASO ili kutoa mwanya kwa mgombea kwa tiketi ya CCM Ndugu AMAN KIMOLA .H. kushinda kirahisi. Kimsingi tuhuma hizi hazikuwa za kweli na mpaka sasa mtoa tuhuma hajaweza kuzithibitisha ingawa alidai kuwa ushahidi usiotiliwa shaka anao. Hizi ni baadhi ya tuhuma zilizotolewa na baadhi ya viongozi na wanachama kwa nyakati tofauti.

Ninafahamu kwamba kukoma kwa uwanachama ibara ya 5.4.3 nikufukuzwa uanachama na kamati tendaji ya tawi husika.Kutokana na kifungu hiki ninakuja kwako Mwenyekiti wa BAVICHA kuomba ufafanuzi wa utaratibu wa wanachama kufukuzwa uanachama katika katiba ya chadema na mwongozo wake.

Katiba ya chadema ibara ya 6.5.2 kwa mujibu wa ibara ya 5.4.3na 5.4.4 ya katiba ya chama inasema.mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua zakinidhamu ama kuonywa amakuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza.
a) Kujulishwa makosa yake Kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wikimbili.

b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika
c) Mwaachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada yakusikilizwa.

Pia katiba ya chama: Haki za mwanachama ibara ya 5.2.4 kujitetea, kusikilizwa na kukata rufaa anaposhitakiwa ama kuchukuliwa hatua zakinidhamu kichama.
Kwa hiyo naomba ofisi ya Mwenyikiti iweze

1. kunipa ufafanuzi wa taratibu za Chaso ARU kunivua uanachama
2. kuingilia kati hili suala kwani halina Afya kwa Tawi na Chama kwa ujumla
3. BAVICHA na chama kwa ujumla wasimamishe uchaguzi wa tawi uliopo siku za usoni kwani mimi ni miongoni mwa wanachama waliochukua fomu na kukidhi matakwa ya chama.

4. Wahusika wachukuliwe hatua stahiki kulingana na kanuni na taratibu za chama na mabaraza yake.

5. Tawi na Chama kwa ujumla wafanye juhudi za makusudi kuhakikisha wanalisafisha jina langu nje na ndani ya chuo na chama kwa ujumla.
 
Attachments

  • BARUA KWA BAVICHA-1.pdf
    1.3 MB · Views: 74

Tutolee stress zako humu na chaso yako humu watu tunawaza vitu vya msingi..nyinyi mlitumwa kwenda kusoma.au kufanya siasa?? Kama hawakutaki si uwaachie chaso yao kwani unalipwa?? Au hao chaso wanakulipia ada?? Wanakufanyia mitihani?? Kama hayo yote hayapo sasa unalazimisha nini? Cha Msingi hamia ccm hapo chuo kawapige nondo ukiwa huko si shwari tu..acha kulia lia humu chama chenu hakina demokrasia kuanzia kwa mzee baba wenu hataki kuachia kitu sasa itakua kwa hao chaso...jitathmini chukua hatua.
 
Ebu fuata taratibu zote za kisheria kubadili jina ,jina jipya uitwe Eliimani Massawe then uombe uanachama upya.
 
Unatuhumiwa kutumika na ccm.!? Jisafishe upya ila nakuasa uache kutumiwa na chama ambacho kimekua hakipendwi hata na vyuo vingine, walioelimika hawakipendi!

Nmashauri kijana asome aachane na mambo ya siasa.kama anataka siasa asubiri amalize kwanza chuo ili aende jimboni akapambane huko.kwa sasa hivi ni mapema mno kwa kijana huyo kuanza siasa.
 
Back
Top Bottom